Msikiti mkubwa wa Answar
Sunna uliopo barabara ya saba mjini Dodoma umewaka moto mchana
huu ikiwa ni muda mfupi baada ya swala ya mchana
kumalizika....
Akiongea kwa njia ya simu na Mpekuzi wetu, mmoja wa mashuhuda walioshuhudia tukio hilo amedai kuwa chanzo cha moto huo ni moto wa JIKO la wakazi wa ghorofa ya juu ya jengo la msikiti huo...
Hata hivyo, shuhuda mwingine aliyeongea na mtandao huu amedai kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme iliyoanzia ghorofa ya juu ya jengo hilo.
Kwa
mujibu wa mashuhuda hao, moto huo umefanikiwa kudhibitiwa na
jeshi la zima moto na kwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha
kutokana na moto huo.
Akiongea kwa njia ya simu na Mpekuzi wetu, mmoja wa mashuhuda walioshuhudia tukio hilo amedai kuwa chanzo cha moto huo ni moto wa JIKO la wakazi wa ghorofa ya juu ya jengo la msikiti huo...
Hata hivyo, shuhuda mwingine aliyeongea na mtandao huu amedai kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme iliyoanzia ghorofa ya juu ya jengo hilo.
No comments:
Post a Comment