KIKUNDI
cha waasi cha M23 kinachopambana na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC), kimeripotiwa kupigwa vibaya na kutikisa nguvu za kikundi
hicho kutokana na baadhi ya wapiganaji wake kuripotiwa kupoteza maisha.
Mapigano
baina ya M23 na Jeshi la Serikali ya DRC linalosaidiwa na Kikosi
Maalumu cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO), yameibuka upya
ndani ya wiki hii.
Habari za kiintelijensia zinasema kuwa, kutokana na shambulio hilo,
Serikali ya Rwanda imelazimika kuingilia kati kusaidia waasi hao kwa
kupeleka bataliani mbili zenye jumla ya askari 1,700 huko DRC,
ili waweze kukabiliana na nguvu ya majeshi ya JWTZ, DRC, Monusco na
Brigedi ya Majeshi ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa yenye mamlaka ya
kujibu mapigo (FIB).
Kwa
mujibu wa vyanzo hivyo vya habari, Rwanda imepeleka bataliani hizo
mbili zenye askari 850 kila moja saa 48 zilizopita na kwamba wamevuka
mpaka kuingia DRC katika eneo la Kibumba, lakini wanashindwa kusonga
mbele.
Habari
zaidi zinasema sababu ya Rwanda kupeleka askari wake hao ni kusaidia
M23 ambao walipigwa sana Agosti 23 na 27, mwaka huu katika eneo la
vilima vya Kibati na kuikimbia ngome yao.
“M23
walitandikwa sana Agosti 23 na 27 katika eneo la vilima vya Kibati, na
kulazimika kuikimbia ngome yao, ndio maana sasa hivi Rwanda imepeleka
batalioni zao kuwapa nguvu, lakini wanashindwa kusonga mbele maana
hawajielewi kwa sababu ya kipigo walichopata,” kilisema chanzo kimoja
cha habari.
Kwa
mujibu wa vyanzo hivyo vya habari, eneo la Kibati ndilo eneo kubwa la
M23 ambalo wamekuwa wakitumia kuhifadhi silaha zao za kivita, lakini
wakati wa mapambano majeshi ya JWTZ , DRC, MUNUSCO na FIB
yalisambaratisha kabisa ngome hiyo ya waasi.
FIB
inaundwa na askari wengi wa Afrika Kusini na Tanzania. Habari zaidi
zinasema kwa sasa majeshi ya DRC, Monusco na FIB yanawasubiri kwa hamu
askari hao wa Rwanda kuingia uwanja wa vita ili kukabiliana nao kama
walivyokabiliana na waasi wa M23.
“Taarifa
tulizonazo hivi sasa Rwanda inajiuliza iwapo isonge mbele kupambana au
irudi nyuma, ikifikiria pia kipigo walichopata M23,” kilisema chanzo kimoja cha habari.
Inaelezwa
kwamba, kutokana na kipigo walichopata M23 siku chache zilizopita
kimepelekea Rwanda kujikuta ikikiri na kusema ukweli juzi kuwa
inakisaidia kikundi hicho cha waasi.
No comments:
Post a Comment