Unique model Catherine akiwa katika pozi na Judie Sangu kipindi cha kambi ya shindano la unique model 2012.
Mandhali tulivu katika fukwe za hoteli ya Giraffe ocean view iliyopo jiini Dar es salaam.
Pages
BRAND NEW MUSIC
metty magese
Listen & Download
http://mdundo.com/a/32626
Thursday, January 31, 2013
WEMA SEPETU ALIVYOJIMWAGA KWA SERENGETI BOY WAKE
Wema Sepetu ameamua kuhamishia majeshi yake kwa kiserengeti boy ili kulipiza kiasi kwa X wake wa zamani, DIAMOND.....
Huyu ni Haidary Cavilla ambaye ni mchumba wa miss Tanzania namba 2 ,mwaka 2000, aitwaye Mercy Galabawa....
Kama kawaida, jamaa ni mdogo kiumri akilinganishwa na Wema, lakini inasemekana kwama Haidary anamiliki mkwanja mrefu ulioichanganya akili ya Wema Sepetu hasa baada ya kununuliwa gari aina ya Audi Q7.....
Picha hizi zilipigwa nyumbani kwa wema sepetu na hatimaye kuvuja mitandaoni,hali inayoashiria kulipiza kisasi kwa Diamond baada ya kunaswa akiwa na Penny....
Wema sepetu ni mrembo anayekabiliwa na skendo chafu ya kubadiliwanaume kama nguo.Alianza na..
Huyu ni Haidary Cavilla ambaye ni mchumba wa miss Tanzania namba 2 ,mwaka 2000, aitwaye Mercy Galabawa....
Kama kawaida, jamaa ni mdogo kiumri akilinganishwa na Wema, lakini inasemekana kwama Haidary anamiliki mkwanja mrefu ulioichanganya akili ya Wema Sepetu hasa baada ya kununuliwa gari aina ya Audi Q7.....
Picha hizi zilipigwa nyumbani kwa wema sepetu na hatimaye kuvuja mitandaoni,hali inayoashiria kulipiza kisasi kwa Diamond baada ya kunaswa akiwa na Penny....
Wema sepetu ni mrembo anayekabiliwa na skendo chafu ya kubadiliwanaume kama nguo.Alianza na..
KITALE KUFUNGA PINGU ZA MAISHA JUMAPILI HII
Kwa mujibu wa Kitale alisema japokuwa amepitia katika changamoto mbalimbali za ki maisha na amejifunza mengi na ndiyo sababu ya kuvuta jiko.
Wednesday, January 30, 2013
Tuesday, January 29, 2013
MAITI YA KICHANGA YAGEUKA JOGOO HOSPITALI YA MWANANYAMALA
BADO tupo mwanzoni mwa mwaka lakini tukio la maiti ya kichanga kugeuka jogoo ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti kwenye Hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam linaweza kuongoza mengine yote ya ajabu yanayoweza kujiri ndani ya 2013.
Asubuhi ya Jumatano iliyopita, ilikuwa kizaazaa pale jokofu lililotumika kuhifadhi maiti ya kichanga cha mtoto, kukutwa kuna jogoo.
Mshangao zaidi ni kwamba ndani ya lile jokofu, pembeni ya yule jogoo, kulikuwa na hirizi pamoja na tunguri.
Habari kutoka vyanzo vyetu, zimewekwa wazi kuwa Jumanne iliyopita, saa 7 mchana, polisi walipigiwa simu, wakataarifiwa kuhusu maiti ya mtoto iliyokuwa imetelekezwa eneo la Kigogo, Mbuyuni, Dar es Salaam.
Vyanzo vyetu vimebainisha kuwa polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kukuta maiti hiyo ya kichanga ikiwa imefunikwa kwa kuzungushiwa sanda.
Kwa mujibu wa Moses Madilu, mkazi wa Kigogo, aliyedai kushuhudia tukio hilo, polisi walipofika eneo la tukio waliikagua maiti hiyo na kubaini kwamba ni ya kike.
Chanzo chetu kikaeleza kuwa baadhi ya mashuhuda, hususan wanawake, walitokwa na machozi kwa masikitiko kwamba itakuwa mtu alijifungua halafu akakinyonga kichanga hicho kabla ya kukitelekeza eneo hilo.
“Baada ya kujiridhisha kwa kazi yao, polisi waliichukua maiti hiyo ya kichanga, wakaipakia kwenye ‘difenda’, wakaipeleka Hospitali ya Mwananyamala,” kilieleza chanzo chetu.
HOSPITALI YA MWANANYAMALA
Ndani ya hospitali hiyo, mwandishi wetu alielezwa kuwa polisi walipofika, walishusha maiti hiyo na kumkabidhi mganga wa zamu aliyejulikana kwa jina moja la Dk. Liwa.
“Dk. Liwa aliwaambia wale polisi wapeleke maiti hiyo mochwari.
“Polisi walifanya hivyo lakini kule mochwari walimkuta msimamizi mkuu, Omar Buyoya aliyekataa kuipokea kwa vile daktari hakuthibitisha kama kile kichanga kilikufa au kilikuwa hai.
“Polisi na Buyoya walivutana kwa muda mrefu, alitokea mhudumu mwingine wa mochwari aliyekuwa akijuana na polisi mmoja aliyebeba ile maiti, alikubali kuupokea mwili huo na kuingiza ndani kwenye jokofu la kuhifadhia maiti.”
Muuguzi huyo aliendelea kusema kuwa siku iliyofuata, Dk. Liwa alifika mochwari na alipofungua jokofu na kufunua sanda, badala ya kukuta maiti ya kichanga, alikuta jogoo, tunguri na hirizi.
“Dk.Liwa alipatwa na mshangao mkubwa huku jasho likimtoka kutokana na uoga, aliwaita wafanyakazi ambao walijazana hapo mochwari kushuhudia.
“Baadhi ya wafanyakazi walipigwa na butwaa huku wengine wakicheka hadi kudondoka chini na wakawa wanajiuliza kama kweli polisi wanaweza kupeleka jogoo hospitali au ni mambo ya kishirikina,” alisema muuguzi huyo.
Dk. Liwa na wafanyakazi wenzake waliondoka mochwari na kuacha hilo jogoo katika chumba cha maiti huku wakishindwa la kufanya.
KAULI YA MGANGA MKUU.....
Uwazi ilimtafuta Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk. Sophinias Ngonyani ambaye alikiri kuonekana kwa jogoo badala ya maiti ya kichanga.
“Polisi walituletea kifurushi wakiamini kuwa ni maiti ya kitoto kichanga ambapo tulikipokea lakini ilipotazamwa na daktari, tulikuta jogoo, hirizi na tunguri, tuliamua kumchoma moto kwa sababu kile ni chumba cha kuhifadhi maiti siyo cha kuhifadhia mizoga ya kuku, ng’ombe au mbwa,” alisema Dk. Ngonyani.
KAULI YA POLISI ...
Naye Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela alipoulizwa juu ya sakata hilo alisema kwamba wao kama jeshi la polisi walipigiwa simu na raia mwema kuwa kuna maiti ya kichanga ambapo askari waliondoka hadi eneo la tukio na kuichukua mpaka Hospitali ya Mwananyamala.
“Polisi waliichukua hadi Hospitali ya Mwananyamala kwa wataalamu na baada ya kuikabidhi waliondoka na kuendelea na shughuli nyingine, nami nashangaa kusikia kwamba madaktari walikuta jogoo,” alisema Kenyela.
MASWALI MATANO
Je, ni kweli polisi waliikagua maiti na kugundua ni kichanga cha kike?
Kama ndiyo, ilikuwaje kikageuka jogoo?
Kwa nini daktari hakuipima ile maiti, badala yake akaelekeza ipelekwe mochwari?
Je, au polisi walibeba mzoga wa jogoo, wakampakia kwenye difenda wakidhani ni maiti ya kichanga?
Mkweli nani, polisi wanaodai kupeleka maiti ya kichanga, au hospitali wanaosema walipelekewa mzoga wa kuku, tunguri na hirizi?
Na Mpekuzi
RICK ROSE ANUSURIKA KUPIGWA RISASI ZA TUMBO
Imeripotiwa kwamba nyota Rick Ross, anusurika kujeruhiwa baada ya mtu mmoja aliyekuwa na silaha kurusha risasi kadhaa kwenye gari yake aina ya Rolls Roys
Ndani ya gari hilo aliyekuwemo yeye na msichana mmoja na kusababisha kugonga nyumba akijaribu kuongeza mwendo,taarifa zilizotolewa na mashahidi
Taarifa za polisi zinasema kuwa asubuhi ya leo (jumatatu) wamepokea simu nyingi kutoka kwa wakazi ambao wanaishi maeneo ya Las Olas baada ya kusikia mlio wa risasi
polisi wanasema gari lingine lilisimama karibu na gari la nyota huyo na mtu mmoja aliekuwa ndani ya gari hilo kuanza kurusha risasi kwenye gari la Ross
Nyota huyo hakupatwa na risasi hata moja wakati wa tukio hilo na hakuna mtu yoyote aliyejeruhiwa ndani ya gari hilo.
Mpaka sasa hakuna alietuhumiwa, kugundulika wala kushikiliwa juu ya tukio hilo, polisi wanaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo
Thursday, January 24, 2013
WANANCHI WACHOMA NYUMBA ZA ASKARI POLISI MKOANI PWANI
KUNDI
la wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira, wamevamia kituo cha Polisi cha
Kibiti Wilayani Rufiji na kufanya vurugu kubwa baada ya raia mmoja kufa
kwa kile kilichodaiwa kipigo cha Polisi.
Chanzo
chetu cha Habari kutoka Kibiti kinaipasha kuwa kijana aliyefariki
kutokana na kipigo hicho ni Hamis Mpondi, ambaye mauti yamemfika wakati
akipatiwa matibabu Hospitali ya Muhimbili.
Habari
zaidi zinapasha kuwa hivi sasa wananchi hao wanaendelea kuteketeza
nyumba za Askari Polisi hao zilizopo jirani na kituo hicho, licha ya
Polisi kuendelea kufanya juhudi za kuwatawanya kwa mabomu katika eneo
hilo.
Aidha
wananchi hao wameanza kufunga barabara kuu ya Kilwa iendayo Mikoa ya
Kusini, Lindi na Mtwara kwa mawe, magogo na kuchoma matairi ikiwa ni
umbali wa kama kilometa moja kutoka kituo cha Polisi Kibiti.
Hali
inaelezwa kuwa inazidi kuwa tete huku Polisi wa Kibiti wakiendelea na
jitihada za kudhibiti hali hiyo kwa kufyatua mabomu hewani kujaribu
kutawanya umati huo wa watu. Vurugu zinaendelea, Habari kwa hisani ya
Father Kidevu.
Wednesday, January 23, 2013
Tuesday, January 22, 2013
MSANII JUX AJITUPA KWA PENZI LA MKE WA MTU JACKLINE CLIFF
Unamkumbuka Jux? Yule chorus Killa wa kundi la Wakacha wazee wa Coders? Yeah, jamaa yuko kimya kiaina lakini kwa mujibu wa picha zake za Instagram the boy is living large! Pamba kali (kama kawaida yake), trip za pipa za hapa na pale kwenda ughaibuni na mambo kibao.
Kikubwa zaidi the songbird is apparently dating one of the hottest models in Tanzania, Jackie Cliff.
Kama humfahamu vizuri Jackie anaonekana kwenye video za nyimbo kadhaa za Bongo Flava zikiwemo Nataka Kulewa wa Diamond na She got a gwan wa Ngwair!
Kupitia akaunti ya Instagram Jackie amepost picha akiwa na Jux na kuandika, “Dinner date with @juma_jux in Garden hotel.”
Na pia Jux kwenye akaunti yake amepost picha ya Jackie akijaribisha kuvaa viatu vyake (Jux) na kuandika, “baby tryn them #me Jordans…#dope though.”
TUHUMA ZA VIGOGO WA BANDARI HIZI HAPA
WIZARA ya Uchukuzi imewatimua kazi Wakurugenzi
wa 3 na Mameneja 2 wa Waliokuwa Watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)
Makao Makuu Dar es Salaam.
Akitangaza Uamuzi huo kwa Wana Habari Ofisini
kwake, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema kuwa katika taarifa
yake aliyo isoma kuwa Wakurugenzi hao walitimuliwa kazi kwa nyakati
tofauti baada uchunguzi wa Tuhuma
zilizokuwa zikiwakabili kukamilika ikiwa ni pamoja na watuhumiwa kuhojiwa.
Kubwa zaidi lililowapelekea wakubwa hao wa TPA
kuachwa nje ya Meli yaDk. Mwakyembe ni Matumizi mabaya ya Madaraka na
Ubadhirifu wa Mali ya Umma na kuitia Hasara serikali na huenda Bodi ya
Wakurugenzi ikijiridhisha ikawafungulia Mashitaka Mahakamani.
Dk. Mwakyembe ambaye yupo mstari wa mbele katika
vita dhidi ya ubadhirifu wa Mali za Umma kwa kuwashughulikia ipasavyo watendaji
wa Sekta zake zote hasa TPA na ATC, aliwataja walio timuliwa kazi kuwa ni aliyekuwa
Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Ephraim Mgawe,
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Huduma, Hamadi Koshuma, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
Miundombinu, Julius Mfuko, Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Cassian Ngamilo,
Meneja Kituo cha Kupakuluia Mafuta, Tumaini Massaro.
Tuhuma zilizokuwa zikiwakabili ni kama ifuatavyo
kwa kila mmoja:-
MKURUGENZI MKUU TPA: EPRAIM MGAWE
Akiainisha
tuhuma zilizomfukuzisha kazi Mgawe kuanzia Ijumaa iliyopita Januari 18 mwaka
huu, Dk Mwakyembe alisema ni pamoja na uzembe uliokithiri.
Dk
Mwakyembe alidai kuwa Mgawe alizembea na kuruhusu kuwepo kwa muda mrefu
utaratibu usiofaa wa upokeaji na uondoshwaji bandarini wa mafuta machafu.
Katika
tuhuma hiyo, Mgawe anadaiwa kuachia kiasi kikubwa cha mafuta safi kuibiwa; na
kushindwa kudhibiti kiwango cha utoaji bandarini wa mafuta machafu kinyume na
mikataba iliyowekwa.
Tuhuma
ya pili iliyomuondoa kazini Mgawe, ni ufanisi duni ambao Dk Mwakyembe
alifafanua kuwa alishindwa kudhibiti wizi uliokithiri bandarini wa mizigo na
mali ya Mamlaka.
Pia
anadaiwa ameshindwa kusimamia utekelezaji wa mkataba kati ya Kitengo cha
Kuhudumia Kontena Bandarini (TICTS) na TPA ambapo TICTS kwa muda mrefu inadaiwa
wamekuwa wakikiuka mkataba huo.
Pia
Mgawe anadaiwa kuipotosha Bodi mpaka ikaridhia uanzishwaji wa chombo cha pili
cha ununuzi ndani ya Mamlaka kinyume ya Sheria.
Kosa la tatu la Mgawe ni kukosa uaminifu kulikopindukia, ambapo anadaiwa kutumia chombo cha pili cha ununuzi kilichoanzishwa kinyume cha sheria na kuingia zabuni mbalimbali bila kufuata utaratibu na kanuni za zabuni kama zilivyoainishwa na Sheria ya Manunuzi.
Pia
inadaiwa miradi mingi iliyongiwa kwa njia hiyo ya chombo cha pili cha ununuzi,
haikuwa na tija kwa Mamlaka zaidi ya matumizi mabaya ya fedha za umma.
Kasa la mwisho lililomuondoa Mgawe kwa mujibu wa Dk Mwakyembe, ni kukiuka sheria na utaratibu ambapo anadaiwa kuingia mkataba na Kampuni ya China Communications Construction Company Ltd (CCCC) bila kuishirikisha Bodi ya Zabuni ya Mamlaka.
Pia
anadaiwa kuongeza mishahara kwa asilimia 15 tarehe mosi Julai, mwaka jana bila
idhini ya Waziri wa Uchukuzi, hivyo kukiuka utaratibu uliowekwa na sheria.
NAIBU
MKURUGENZI MKUU WA HUDUMA, HAMADI KOSHUMA
Tuhuma
zilizomng’oa Koshuma kwa mujibu wa Dk Mwakyembe ni nne, ikiwemo ya matumizi
mabaya ya madaraka. Katika hilo, Naibu Mkurugenzi Mkuu huyo wa Huduma, anadaiwa
kuruhusu michakato mbalimbali ya zabuni bila kufuata utaratibu kwa kisingizio
cha kwamba ni miradi mikubwa.
Koshuma pia anadaiwa kuwa na ufanisi duni, ambapo akiwa Mjumbe wa Bodi ya Zabuni, alishindwa kuijulisha Bodi ya Mamlaka ya Ununuzi ya Umma (PPRA), kuhusu ukiukwaji wa Sheria ya Manunuzi.
Ukiukwaji
huo umefafanuliwa kuwa unahusu kuruhusu Mamlaka kuingia mkataba wa kibiashara
na CCCC bila kuishirikisha Bodi ya Zabuni na kushindwa kutoa ushauri wa kitaalamu
kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka katika udhibiti na uendeshaji.
Kosa la tatu analodaiwa kufanya ni kukosa uaminifu kulikopindukia, ambapo Koshuma anadaiwa kushiriki kuipotosha Bodi mpaka kuanzishwa cha chombo cha pili cha manunuzi kinyume ya sheria.
Baadaye,
anadaiwa kutumia chombo hicho batili bila kufuata utaratibu kwa kisingizio kuwa
ni miradi mikubwa ambapo miradi mingi iliyongiwa kwa njia hiyo, haikuwa na tija
kwa Mamlaka zaidi ya matumizi mabaya ya fedha za umma.
Mwisho Koshuma amedaiwa kukiuka sheria na taratibu kwa kushiriki kuingia mkataba na CCCC bila kuishirikisha Bodi ya Zabuni ya Mamlaka.
Pia
anadaiwa kushiriki kwenye uamuzi wa kuongeza mishahara kwa asilimia 15
kuanzia Julai mosi, mwaka jana bila idhini ya Waziri wa Uchukuzi.
NAIBU MKURUGENZI MKUU WA MIUNDOMBINU, JULIUS MFUKO
Kwa
upande wa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Miundombinu, Mfuko Dk Mwakyembe alisema bosi
huyo wa zamani anadaiwa kushindwa kusimamia maandalizi ya miradi mbalimbali ya
miundombinu ya mamlaka.
Kwa
mfano inadaiwa miradi ya ex-AMi yard, Port Community System na CCTV kwa
muda mrefu iko kwenye utekelezaji bila kukamilika kutokana na misingi mibovu ya
maandalizi. Imeelezwa kuwa fedha nyingi ya Mamlaka imetumika kwenye miradi hiyo
bila matokeo tarajiwa.
Pia anadaiwa kushindwa kusimamia utekelezaji wa mikataba mbalimbali, na kusababisha kutokamilika kwa wakati na kuisababishia Mamlaka hasara kubwa.
Kasa la tatu ni kushindwa kuisimamia kwa ufanisi divisheni ya maendeleo ya miundombinu na kuathiri maendeleo ya Mamlaka kwa ujumla.
Mfuko pia anadaiwa kushindwa kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka katika udhibiti na uendeshaji wa Mamlaka.
Mameneja
Panga la Mwakyembe limewaangukia pia
Mameneja wawili ambao ni MENEJA WA BANDARI YA DAR ES SALAAM, CASSIAN
NGAMILO na MENEJA KITUO CHA KUPAKULUIA MAFUTA (KOJ), TUMAINI
MASSARO.
NGAMILO: Yeye amedaiwa kutumia
madaraka yake vibaya, uzembe uliokithiri na kushindwa kusimamia mkataba
wa mafuta machafu.
Pia anadaiwa kushindwa kusimamia ulinzi wa mali
za wateja, kutoa nyongeza ya mkataba kinyume cha sharia.
MASSARO: Ameachishwa kazi
kutokana na madai ya uzembe uliokithiri, kushindwa kusimamia udhibiti wa mafuta
machafu na kuisababishia Serikali hasara kubwa pamoja na ufanisi duni.
Thursday, January 17, 2013
INASIKITISHA ...KICHANGA CHATUPWA KANDO YA CHUO CHA TUMAINI
Tunaomba radhi kwa picha hii ila hatuna budi kuwapa picha kamili ya mama huyu aliefanya kitendo cha kinyama.
Mtoto
wa jinsia ya kike anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja amekutwa
ametelekezwa pembeni ya mto karibu na chuo kikuu cha Tumaini Iringa.
Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa kitendo hicho ni cha kinyama zaidi katika eneo hilo na hii inaonesha jinsi gani watu wasivyo na utu mioyoni mwao.
"Inavyoonekana mtu huyu alijifungua halafu akamtupa mtoto huyu, hii ni ajabu sana kwa mtu kubeba mimba miezi tisa halafu kuamua kutupa kiumbe kisicho na hatia" alisema kijana huyo aliyefahamika kwa jina moja Rajabu
Kwa mujibu wa kijana aliyeona mwili huo alisema alikuwa anaelekea shambani na ndipo alipoamua kupitia sehemu ambayo huwa anaficha jembe na kuona kiumbe huyo akiwa ametelekezwa huku akiwa amekwisha kufa.
"Inawezekana mtu huyu alimtupa mtoto huyu usiku kwani jana wakati naficha jembe hapakuwa na kitu chochote "alisema kijana huyo.
Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa kitendo hicho ni cha kinyama zaidi katika eneo hilo na hii inaonesha jinsi gani watu wasivyo na utu mioyoni mwao.
"Inavyoonekana mtu huyu alijifungua halafu akamtupa mtoto huyu, hii ni ajabu sana kwa mtu kubeba mimba miezi tisa halafu kuamua kutupa kiumbe kisicho na hatia" alisema kijana huyo aliyefahamika kwa jina moja Rajabu
Kwa mujibu wa kijana aliyeona mwili huo alisema alikuwa anaelekea shambani na ndipo alipoamua kupitia sehemu ambayo huwa anaficha jembe na kuona kiumbe huyo akiwa ametelekezwa huku akiwa amekwisha kufa.
"Inawezekana mtu huyu alimtupa mtoto huyu usiku kwani jana wakati naficha jembe hapakuwa na kitu chochote "alisema kijana huyo.
Wednesday, January 16, 2013
VYANGUDOA WALIVYOPOTUPWA SERO
Machangudoa wakiwa wameziba nyuso zao zilisipigwe picha na mwandishi wetu.
Mke wa mtu akiwa ameziba uso wake kwa mikono ili kukwepa kamara
Mke wa mtu akiwa amejifunika uso kwa Khanga ili asipigwe picha.
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida,mke wa kigogo mmoja ambae anacheo kikubwa
hivi karibuni alibambwa kwenye danguro moja lilipo maeneo ya Sinza
jijini Dar akijiuza.
Habari
zaidi toka kwa watu wa karibu wanaomjua mwanamke huyo maarufu kwa jina
la Mama Amina zinadai kuwa yeye ni mke wa pili wa kigogo mmoja anaefanya
kazi kwenye Wizara moja nyeti ya Serikali ya Jamhuri ya Tanzania.
Aidha watu hao mwandishi wa habari hizi
Jijini Dar kuwa mwanamke huyo alifikwa na balaa hilo katika msako mkali
unaoendelea wa Polisi Kanda ya Kinondoni wa kuwakamata machangudoa wote
wanaojiuza.
Habari zaidi ziliendelea kusema kuwa kigogo huyo ana familia nyingine ambayo inaishi maeneo ya Mbezi Beach .
Huyu Mama Amina amempangishia nyumba maeneo ya Sinza Mori na amekuwa akimpa huduma zote muhimu...
Cha kushangaza ni kwamba kila mumewe akiondoka nyuma huenda kujiuza.
Mwandishi
wetu jana alifika kituo cha Polisi Oysterbay na kushuhudia kundi la
machangudoa hao wakipelekwa Mahakamanikwa gari ya Manispaa pamoja na
gari ya polisi akiwemo mwanamke huyo wa kigogoCha kushangaza ni kwamba kila mumewe akiondoka nyuma huenda kujiuza.
DINI YA MWABUDIAO SHETANI MAKAO MAKUU AFRIKA YALIPOTIWA KUWA NIGERIA
Taarifa iliyoripotiwa january 15 2013 imeeleza kwamba kwa sasa Nigeria imeteuliwa kuwa makao makuu ya dini inayomuabudu shetani.
Nigeria, Ghana na South Africa ndio nchi zinazotajwa kuongoza kwa kuwa na waumini wengi wa dini inayomuabudu shetani Afrika.
Imeelezwa kwamba kuteuliwa kwa Nigeria kuwa makao makuu ndio sababu nyingine pia ya mauaji na umwagaji damu unaoendelea kwa sasa.
Inaaminika damu na kafara za kuuwa ndugu wakiwemo wazazi na jamaa wa karibu ndio sadaka muhimu ya dini hiyo, umeripoti mtandao wa IRL.
Ujumbe maalum: Ila
kumbukeni siku ile ya kutisha ya kuja mwana wa adamu yesu kristo
kuuhukumu ulimwengu imekaribia ,kila goti litapigwa na wale wote
wasiiyoiamini injili ya bwana yesu watatupwa katika ziwa la moto
liwakalo na kibiriti milele hata milele, I love u jesus.
Tuesday, January 15, 2013
ASHUSHIWA KICHAPO BAADA KUDAIWA NDIYE MBAKAJI WA WATOTO
Mwananchi huyu mwenye hasira kali akimnyanyua juu kibaka huyo na kumtupa chini kama akina 'John Cena'.
..Kichapo kikiendelea kwa kibaka huyo.
Kibaka huyo akizidi kuhukumiwa mtaani.
Ustadhi akijaribu kumnusuru kibaka huyo.
Ustadhi huyo aliamua kuondoka na kibaka ili kumwokoa.
Akimpeleka kituo kikuu cha polisi kilichopo jirani na eneo hilo la Shani.
KIJANA mmoja anayesadikiwa kuwa ni kibaka mchana huu amenusurika kifo
baada ya kupokea kichapo kikali kutoka kwa wananachi wenye hasira
wakimshutumu kuiba watoto wadogo na kwenda nao eneo la mto Morogoro
chini ya daraja la Shani na kuwafanyia vitendo vya kihuni.
Akizungumza na Mtandao huu mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa
jina la Juma Athuman alidai kwamba kijana huyo ana kawaida ya kuwateka
watoto wadogo hasa wa shule na kuwapeleka chini ya daraja hilo na
kuwafanyia vitendo vya kihuni.
" Kwa kipindi kirefu tulikuwa tukimsaka kibaka huyu ambaye ana tabia ya
kuwateka watoto wadogo na kuwapeleka mto wa Morogoro chini ya daraja la
Shani.
"Muda huu tumemfuma akiwa chini ya daraja hilo na mtoto mdogo ndipo
tulipomfukuza na kufanikiwa kumkamata eneo hili la kituo cha mafuta
jirani na daraja hili la Shani," alisema Juma Athuman.
WANAFUNZI WA IFM NA MNMA WALIVYOCHEZEA KICHAPO KUTOKA KWA POLISI
BAADA ya wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha (IFM) kwenda kigamboni ambako Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova kuwataka wakawasilishe hoja zao hukohuko ambako wanadai walipeleka majina ya wahalifu na hayajashughulikiwa, waligoma kufanya mkutano kwenye viwanja vya mpira eneo la Machava nakutaka mkutano huo ufanyike kwenye kituo cha polisi Cha Kigamboni ambako wanafunzi wengi wao walielekea huko. |
Mara
baada ya kufika kwenye kituo hicho waliamriwa maratatu waondoke waende
kwenye mkutano na Kamanda Kova wakakataa baada ya hapo ndipo mabomu
yakaanza kupigwa. Kwenye mabomu hayo wanafunzi kadhaa walijeruhiwa na
kuumia wengine walipoteza fahamu.
Hata
hivyo walioshikiliwa wote waliachiwa na kutakiwa kwenda kwenye mkutano
huo ambao uliazimia mambo kadhaa ya utekelezaji ili kutatua tatizo hilo
la wizi kwenye eneo hilo. Kamanda Kova aliwaahidi wanafunzi hao kuwa
watapata mrejesho wa hatua walizochukuwa siku ya tarehe 30 mwezi huu.
|
WABABA WA BSS AZUSHIWA KUMTIA MWANAFUNZI MIMBA
Mapenzi
yao yalianza tangu binti akiwa kidaato cha tatu lakini halikuwa penzi
lenye mashamu shamu kwa kuwa wabababa alikuwa bado hajamiliki pesa na
heshima katika jamii inayomzunguka kama sasa mara tuu baada ya kuchukua
kifuta jasho cha bss na vijihela alivyopewa na mapapaa waliokubali kazi
aliioifanya bss hivyo kuwa na kiburi kilichomfanya amtie mimba mwananfunz ambae aligundulika kuwa ametoa mimba mara taarifa za mahusiano ya wababa na mwanafunzi huyo kufikishwa kwa mama mzazi wa binti huyo.
aliioifanya bss hivyo kuwa na kiburi kilichomfanya amtie mimba mwananfunz ambae aligundulika kuwa ametoa mimba mara taarifa za mahusiano ya wababa na mwanafunzi huyo kufikishwa kwa mama mzazi wa binti huyo.
Wababa
aliwekwa ndani kwa muda wa siku mbili na kesi bado ipo mahakamani na
wazazi wa binti wameapa kumweka ndani wababa na kumfanya kama Babu Sea
huku binti akiwa hajaonekana siku ya 4 sasa na kutokujulikana alipo kwa
madai anampenda wababa na wakimfunga tu nae anakunywa sumu.
SOURCE MPEKUZI!
UNIQUE MODEL CATHERINE ATEMBELEA WATOTO WAGONGWA CCBRT
Unique model 2012 Catherine Masumbigana akiwa na watoto wagongwa katika hospitali ya CCBRT iliyopo msasani jijini Dar es salaam,Catherini alipata fulsa ya kuongea na watoto hao kwa kuwafariji,kuwaonesha upendo na kuwapa zawadi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kazi za kijamii katika taji lake.
Mtoto huyu akiwa na majeraha ya kuungua kwa moto.
Unique mode Catherine akishow love kwa kabebii.
Akiwa anarudi nyumbani,last pic ..pwachaa!
Mtoto huyu akiwa na majeraha ya kuungua kwa moto.
Unique mode Catherine akishow love kwa kabebii.
Akiwa anarudi nyumbani,last pic ..pwachaa!
Monday, January 14, 2013
WANACHUO WAVAMIA WIZARA YA ULINZI KUOMBA ULINZI BAADA YA WENZAO KUBAKWA
Wanafunzi
wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) na wa Chuo
cha Mwalimu Nyerere Kigamboni, wakiwa mbele ya geti la Wizara ya Mambo
ya ndani walipovamia leo majira ya saa nne na nusu asubuhi kufikisha
malalamiko yao ya kutaka kupatiwa ulinzi katika Hosteli zao, zilizopo
Kigamboni.
Wanafunzi hao wamefikia hatua hiyo, baada ya wenzao wawili wa kiume kubakwa na majambazi hadi kulazwa hospitalini, huku wakieleza kuwa kumekuwa na matukio kadhaa ya mara kwa mara ya kuvamiwa na majambazi na kulitaka jeshi la Polisi kutoa huduma ya ulinzi katika Hosteli zao.
Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili waweze kupatiwa ulinzi lakini hadi sasa ombi lao halijaweza kufanyiwa kazi na cha kushangaza zaidi ni kwamba, siku hiyo hiyo waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndiyo siku wenzao wawili wa kiume walipovamiwa na kubakwa hali iliyosababisha wanafunzi kuzidi kuingia hofu ya kuishi katika Hosteli hizo.
Aidha wanafunzi hao wameeleza kuwa kila Majambazi hao wanapowavamia, wamekuwa wakiwataka wanafunzi hao vitu vya thamani kama Laptop, Simu za mkononi na fedha, ambapo kila mwanafunzi anayekaidi amri ya majambazi hao, humfanyia vitendo vya udhalilishaji kama kulawiti na mengineyo.
Wanafunzi
hao wakiwa wamejazana katika kivuko cha Magogni, wakitelemka kivukoni
kwa ajili ya kuelekea Wizara ya Mambo ya ndani. Pamoja na kutakiwa kupungua, wengine walizidi kuendelea kuingia na kukijaza kivuko hicho.
Wanafunzi hao wakiwa nje ya Jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani.
Askari wakilinda usalama.....
Kamanda Kova, akizungumza na wanafunzi hao pamoja na wanahabari wakati wa tukio hilo.
Na sufian mafoto
Subscribe to:
Posts (Atom)