Wakiwa katika picha ya pamoja watoto ambao ni mapacha watatu, Rehema, Amani na Neema.
Na Kalisa Kachuchu wa Kajunason Blog, Dar es Salaam.
Mkazi
wa Kimara, jijini Dar es Salaam, Edwin Rweyongeza, amewaomba Watanzania
kumsaidia kuwatunza watoto wake mapacha watatu ili waweze kukua vizuri
kutokana na matatizo ya kipato yanayomkabiri.
Rweyongeza,
aliitaja misaada hiyo kuwa ni pamoja na Chakula cha watoto lishe,
yakiwamo maziwa pamoja na matibabu ya kuishiwa na damu yanayoendelea
kuwa tatizo kwa watoto wake.
Akizungumza
muda mfupi uliopita na Habari na Matukio Blog, Rweyongeza alisema
ukosefu wa kipato unaomsumbua, unamfanya ashindwe kuwamudu watoto hao
waliozaliwa Julai sita mwaka 2011 katika Hospitali ya Mwananyamala.
Alisema
kutokana na ukosefu wake wa kipato, Ustawi wa Jamii wilaya ya
Kinondoni, ilikubali Rweyongeza apate msaada kutoka kwa jamii, kwa barua
yao waliyoandikaa Septemba 14, mwaka 2011 yenye kumbukumbu namba
W/WG/2011 na kusainiwa na A.Mbusa.
“Naomba
msaada kutoka kwa Watanzania wenzangu na Dunia kwa ujumla ili watoto
wangu waweze kupata lishe na kufanikisha maisha yao, maana mimi baba yao
kwa sasa sina kipato chochote kwasababu sina kazi ya kuniingizia
kipato.
“Kama
ningekuwa na uwezo nisingeomba msaada, ukizingatia kwamba watoto watatu
kuwalea ni kazi kubwa, hasa kwa masuala ya lishe na matibabu, kama vile
maziwa na mengineyo yanayochangia kukua vizuri,” alisema Rweyongeza.
Kwa
wenye moyo nahitaji la kumsadia, kijana huyo mwenye miaka 29, alizitaja
namba zake ni 0767 646599, 0719 909085, huku akitanguliza shukrani zake
za dhati kwa Watanzania wote.
Mkazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam, Edwin Rweyongeza akiwa na familia yake kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment