Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Sunday, January 6, 2013

PROF JAY NA SAKATA LA KUINGIZWA MKENGE NA WAKENYA

  Kwa mujibu wa gazeti la The Star ka nchini Kenya, rapper Joseph Haule aka r Profesa Jay hivi karibuni aliingia kwenye mgogoro na promoter wa mjini Mombasa Kenya aliyemchukua kufanya show. Prof alikuwa amechukuliwa kufanya show mbili siku ya Christmas kwenye kumbi za Jamboree Resort na Quetu Beach Resort.
 Inavyodaiwa Profesa Jay hakuwa amelipwa fedha zote kwa show ya pili na hivyo alipewa camera aina ya Nikon D3000 kama rehani.Baada ya show, Prof aliondoka nchini Kenya na crew yake na kuibeba kamera hiyo. Sasa waandaaji hao wanadai kuwa walimpatia Prof hela yake iliyokuwa imesalia.

 Issue hiyo imekuwa kubwa kiasi ambacho passport ya mpambe aliyekuwa amesafiri na Jay nchini humo imeshikiliwa ili asiondoke.Waandaaji wanadai kuwa walimlipa Profesa Jay shilingi 252,000 za Kenya ambazo ni zaidi hata ya fedha walizokuwa wamekubaliana na sasa wanataka warudishiwe fedha yao.

Polisi wanashughulikia kesi hiyo na Prof aliyekuwa ameingia makubaliano ya show nyingine katika ukumbi wa Jamboree December 31 aliitosa show hiyo.source na gumzo la jiji

No comments: