Baada ya kugundua wananchi wamemshtukia baada ya kumhoji maswali na
kushindwa kujibu aliamua kutimua mbio kukwepa kamera ya Francis Godwin
isimpate picha yake, kama unavyomuona hapo mdau mguu gafla umetokea
kimiujiza pamoja na mkono, yote hiyo alikuwa ameificha kwa kutumia koti
lake na Suruali alizovaa.
Baada ya hali kuwa tete alijikuta anazisahaumpaka kandambili zake, kama unavyoziona.
Huyu ni omba omba anayeigiza kutokuwa na mkono
mmoja na mguu Mmoja akiwa amekaa eneo la M.R Iringa mjini akisubiri kuomba chochote kutoka kwa
wapita njia leo.
Ule usemi wa wahenga kuwa ukistaajabu ya mussa utayaona ya
firauni leo umetimia katika eneo la M.R mjini Iringa baada ya wananchi
waliokuwepo eneo hilo kupigwa na butwaa baada ya mzee janja ambaye amekuwa
akishinda eneo hilo na kujifanya mlemavu asiyekuwa na mkono mmoja na mguu
mmoja kutimua mboni kukwepa kamera ya mtandao huu.
Tukio hilo limetokea
majira ya saa 8 mchana baada ya camera ya mtandao huo kufika eneo hilo la
kushuhudia umati wa wananchi wakiendelea kumpa fedha mzee janja huyo ambae
alijifanya mlemavu wa vuongo na kuongea kwa shida .
Hata hivyo baada
ya mmoja kati ya wananchi kufika eneo hilo alionyesha kufichua mbinu hiyo
chafu ya mzee huyo kujifanya ni mlemavu wakati asubuhi alikutana nae maeneo ya mjini akiwa
mzima wa afya njema na katika kumhoji zaidi ndipo kamera ya mtandao huu
ilipoamua kufanya kazi yake ya kunasa kituko hicho na ndipo mzee huyo
alipoanza kuongea kwa sauti vizuri tofauti na alivyokuwa akijifanya kuwa
hawezi kuongea kabisa (bubu)
Wakati mabishano yakiendelea eneo hilo
ghafla mzee huyo alisimama kwa miguu yake yote miwili pamoja tofauti na awali
alivyokuwa akijifanya ni mlemavu asiye na mguu mmoja ila baada ya watu kutaka apigwe
picha ndipo mzee huyo alipoanza kutimua mbio huku ulemavu aliokuwa nao
akiusahau hapo pamoja na kandambili zake na hakuna mtu aliyeweza kumfukuza na
kufanikiwa kumkuta.
Baadhi ya wananchi wameuomba uongozi wa Manispaa
ya Iringa kuwabana omba omba hao ambao wamekuwa wakidanganya watu kuwa wao
ni walemavu kumbe ni wazima na kutaka kuwepo kw
No comments:
Post a Comment