Abubakari
Kikulu (29), alipiga picha na mbunge huyo Desemba 23 mwaka jana, baada
ya Lema kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara eneo la Mererani, ikiwa ni
sehemu ya mikutano aliyoifanya kutokana na Mahakama ya Rufani Tanzania
kumrejeshea ubunge wake.
Mbali
na kupiga picha hiyo na Lema pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki
Joshua Nassari, kijana huyo alionekana katika picha hiyo akionyesha
vidole viwili, ambayo ni alama ya Chadema.
Hata
hivyo, baada ya picha hiyo, JWTZ lilimtilia shaka kijana huyo na
kutangaza rasmi kumsaka, ili lijiridhishe kama ni mmoja wa wanajeshi
wake.
Baada
ya kumsaka kwa takriban siku 12, kijana huyo alikamatwa Januari 3,
katika Mji wa Bomang’ombe wilayani Hai na baada ya kupekuliwa alikutwa
na sare hizo.
Jana,
Kikulu alifikishwa mahakamani mjini Moshi, akiwa chini ya ulinzi wa
polisi na kusomewa mashtaka mawili, ambayo yote alikiri kuyafanya kama
ilivyodaiwa mahakamani.
Baada
ya kukiri kosa hilo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa
Kilimanjaro, alimhukumu kifungo cha miaka minne jela, ili iwe fundisho
wa wakosaji wengine wa aina hiyo.
Kabla
ya hukumu hiyo, Wakili wa Serikali, Ignas Mwinuka alimsomea mshtakiwa
huyo mashitaka yake mawili, likiwamo la kujifanya Ofisa wa Jeshi, wakati
akijua ni uongo.
Wakili
huyo alidai mahakamani kuwa Januari 3, mwaka huu katika eneo la
Bomang’ombe wilayani Hai, mtuhumiwa huyo alijitambulisha kama mtumishi
wa umma.
Katika
shtaka la pili, wakili huyo alidai siku hiyo hiyo katika Mtaa wa
Msikitini, eneo hilo la Bomang’ombe, mtuhumiwa alipatikana na sare za
JWTZ kinyume cha sheria.
Sare
hizo ni pamoja na suruali moja, mashati mawili na kofia mbili, vyote
vikiwa na alama za Jeshi la Wananchi wa Tanzania la Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Baada
ya Hakimu Kobelo kumuuliza mshtakiwa kama ni kweli alitenda makosa
anayoshitakiwa, mshtakiwa huyo alikiri makosa yake katika hali ambayo
haikutarajiwa.
Kutokana
na kukiri kwake makosa hayo, Hakimu Kobelo alimhukumu kifungo cha miaka
miwili kwa kosa la kwanza la kujifanya Ofisa wa JWTZ na miaka mingine
miwili kwa kosa la pili.
Hata
hivyo, Hakimu Kobelo alisema kuwa kwa kuwa adhabu hizo zinakwenda kwa
pamoja (concurrent), mshtakiwa huyo atatumikia kifungo cha miaka miwili
jela.
Kwa
mujibu wa hakimu huyo, kosa alilolifanya mtuhumiwa huyo ni baya na
linastahili adhabu kali, ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaotumia
vibaya sare za majeshi nchini.
No comments:
Post a Comment