Waasi
nchini Syria wamewaachia huru raia 50 wa Iran waliowakamata mwaka
uliopita, kwa masharti la kubadilisha na zaidi ya raia 2000
wanaoshikiliwa na serikali ya Rais Bashar al Assad.
Raia
48 wa Iran wanaotuhumiwa kuwa wafuasi wa kundi la Islamic Revolutionary
Guard Corps waliotumwa kupigana upande wa serikali wameonekana katika
hotel mjini Damascus wakiwa katika hali nzuri kiafya.
Iran,
mshirika wa karibu wa serikali ya Assad, alisema kuwa watu hao ni
mahujaji wa madhehebu ya Shia waliokuja nchini Syria kufanya ibada
katika maeneo tukufu.
Wakati
huohuo, Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za
Kiarabu kwenye mzozo wa Syria Lakhdar Brahimi yuko mbioni kukutana na maafisa wa ngazi za juu wa Marekani na Urusi mjini Geneva kesho Ijumaa.
Mkutano
huu unafanyika ikiwa ni siku kadhaa baada ya Rais Assad kutoa hotuba
yake ambayo ilitaka kuwepo kwa majadiliano ya amani yatakayomaliza
machafuko nchini humo. Hata hivyo Jumatano iliyopita bwana Brahimi
aliita hotuba hiyo ya Assad kuwa ni ya kidini na yenye kupendelea upande
mmoja.
No comments:
Post a Comment