Askari wa Kike pekee aliyemudu Kuhitimu Mafunzo Maalum ya kutuliza
Ghasia Magerezani, Wdrs. Diana Nyaluta akionesha Ukakamavu wake pamoja
na Ujasiri alionao alipoweza kuitumia kikwazo cha kamba kutambaa nayo
huku akiwa amebeba silaha yake mgongoni aina ya Sub Machine gun(SMG)
kama anavyoonekana.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa hotuba
yake katika Ufungaji wa Mafunzo Maalum ya kutuliza Ghasia Magerezani leo
Septemba 05, 2013 yaliyofanyika Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia
Magerezani.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(wa kwanza kulia)
akiangalia baadhi ya Vifaa ambavyo hutumiwa na Askari wa Kikosi Maalum
cha Kutuliza Ghasia Magerezani wanapokuwa katika Operesheni mbalimbali
za Kijeshi ikiwemo kutuliza Ghasia Magerezani zinapotokea (pembeni
kushoto) ni Askari wa Kikosi Maalum akiwa amevalia Vifaa hivyo tayari
kukabiliaa na ghasia yoyote.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akimvisha kibaka
cha rangi ya kijani Askari Wdr. Sostenes Mwacha kwa niaba ya Wahitimu
wenzake kutokana na kufanya vizuri zaidi katika Mafunzo hayo Maalum ya
Kutuliza Ghasia Magerezani leo Septemba 05, 2013 katika Kikosi Maalum
cha Kutuliza Ghasia Magerezani, Ukonga Jijini Dar es Salaam.
Na Inspekta Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza, Dar es Salaam Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja amewaasa Askari wa Jeshi
la Magereza nchini kuzingatia maadili ya kazi pamoja na kufanya kazi kwa
bidii na kujituma wakati wote wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao ya
kila siku.
Kamanda Jenerali Minja ameyasema hayo leo wakati wa Ufungaji wa Mafunzo
Maalum ya Kutuliza Ghasia Magerezani ya Kozi No.09 ya mwaka 2013
yaliyofanyika katika Kikosi Maalum cha kutuliza Ghasia Magerezani,
Kilichopo Ukonga Jijini Dar es Salaam.
"Zingatieni maadili ya kazi pamoja na kufanya kazi kwa bidii na kujituma
kwani ndiyo chachu ya mafanikio yoyote yale ya kazini au mafanikio yenu
binafsi". Alisisitiza Kamanda Minja.
Aidha, akijibu hoja za changamoto mbalimbali zilizowasilishwa katika
risala ya Wahitimu wa Mafunzo hayo Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini,
John Casmir Minja alisema kuwa tayari Ofisi yake imeanza kuchukua hatua
ya kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo za upungufu wa vitendea kazi,
makazi duni na upungufu wa Vyombo vya Usafiri kadri hali ya kifedha
inavyoruhusu.
No comments:
Post a Comment