Miss
Universe Tanzania chini ya kampuni ya Compass Communications
inakamilisha jumamosi hii usaili wa warembo jijini Dar es Salaam.
Timu
ya Miss Universe Tanzania ilifanya mchakato wa usaili na picha
(scouting) katika mikoa 8 ambayo ni pamoja na Mwanza, Arusha,
Kilimanjaro, Mbeya, Dodoma, Manyara, Mtwara na Dar es Salaam.
Miss
Universe Tanzania msimu huu utafanya fainali zake mwezi Septemba taehe
27 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa (NATIONAL MUSEUM), Shaban Robert
street jijini Dar es Salaam.
Mashindano
ya mwaka huu umepata wafadhili mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mohamed
Enterprises na Fastjet. Wadhamini wengine watajulikana ndani ya siku
chache. Wadhaimini wote watatambullishwa wiki ijayo.
Kuhusu Miss Universe Tanzania:
Miss
Universe Tanzania ilianza mashindano yake mwaka 2007 na mshindi wake
alikuwa Mwanamitindo Flaviana Matata na aliweza kuitoa kimasomaso nchi
yetu ya Tanzania kwa kushika nafasi ya Sita kidunia.Mwaka uliofuata,
2008 mrembo Amanda Ole Sululu alimrithi Flaviana Matata na kuvaa taji la
Miss Universe Tanzania 2008 akifuatiwa na mrembo Illuminata James mwaka
2009, kisha Hellen Dausen mwaka 2010. Baadae taji lilichukuliwa na
Nelly Kamwelu 2011 na mwaka jana 2012 taji lilinyakuliwa na mrembo
Winfrida Dominic.
Kwa
maelezo zaidi wasiliana na MWANAKOMBO SALIM 0655 441165, SEIF
KABELELE-0713302075 USAHILI WA DAR ES SALAAM UTAFANYIKA KESHO TAREHE
7-9-2013 PALE NYUMBANI LOUNGE KUANZIA SA NNE ASUBUHI
No comments:
Post a Comment