Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Saturday, May 7, 2011

EXCLUSIVE: IZZO BUSNESS AMCHANA MTOTO WA KIKWETE LIVE..!!

      Izzo busness
Msanii wa kizazi kipya nchini Izzo busness a.k.a bizness beibe amemdiss live Ridhiwani Kikwete katika mashairi ya wimbo wake mpya uliojaa maneno ya harakati nzito zisizo na woga dhidi ya kupata matatizo baadae.
        Izzo ambae alikuwa ajihojiwa na kituo kimoja cha redio leo jioni alisema kuwa haogopi chochote kuhusiana na mistari hiyo ambyo inamchana live Ridhiwani.
       Swagga za mchizi huyu pengine zikazua taflani flani kwani mbichi na kavu kazitenganisha.Ngoma hiyo inaitwa Riz-one ambapo ndani yake kakichana sana chama flani.


 CHELSEA YAANGUKIA PUA 2-1
Chelsea imelala 2-1 kichapo toka kwa man u mchezo uliopigwa leo



MARTIN KANDINDA AJIWEKA KINGONO ZAIDI
   Mbunifu na mdau wa matukio kadhaa hapa mjini Martin kadinda amejiachia kwenye photo na demu mmoja ambae jina lake halikupatikana kwa harakaharaka,picha hiyo inaonyesha martin akila denda a.k.a akidendeka  na mwadad ahuyo ambae inasemekana anatengua torati na demu huyo.


Ghasia za kidini zaibukaka Misri

Waziri Mkuu wa Misri, Essam Sharaf, amevunja safari ya kuzuru nchi za Ghuba baada ya ghasia kati ya Waislamu na Wakristo, zilizouwa watu kama sita.
      Hii ilikuwa ziara muhimu kwa Waziri Mkuu, katika nchi za Ghuba ambazo zingeweza kutoa msaada anaohitaji sana, na nchi ambazo piya zina wasi wasi juu ya mwelekeo wa mapinduzi ya Misri.
      Kwa kuvunja safari hiyo, Bwana Sharaf anaonesha anashughulishwa na ghasia nyengine zilizozuka baina ya makundi ya Waislamu na Wakristo.
        Safari hii ghasia zimetokea kwenye mtaa wa kati-kati ya Cairo, pale kundi la Waislamu wa madhehebu ya Sunni, wanaoitwa Salafi, ambao hawapendi mabadiliko, lilipozingira kanisa ambamo likiamini Wakristo walikuwa wakimzuwia mwanamke, ambaye akitaka kubadilisha dini na kuwa Muislamu.
         Risasi zilifyatuliwa, na kanisa na majengo mengine yalichomwa moto.
Ilichukua saa kadha kwa askari wa usalama kuzima mapigano.
Inafikiriwa kuwa Salafi ni wachache kati ya Waislamu, lakini wamekuwa na ghasia nyingi tangu Rais Hosni Mubarak kuondoka mwezi wa Februari.
        Tangu wakati huo, kumetokea mapambano kadha baina ya Wakristo na Waislamu, na Wakristo wengi, ambao ni asili mia 10 ya watu wa Misri, wanahofia usalama wao, endapo makundi ya Waislamu wasiopenda mabadiliko, ndio yatashinda katika uchaguzi wa mwezi Septemba.



JUMA FUNDI ADUNDWA NA NASIBU..!!
Nasibu Ramadhani (kushoto) akimpa masumbwi Juma Fundi wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa lililopigwa raundi 12 na Nasibu kuibuka kidedea na ushindi kwa point.




SEAN KINGSTONE AIDANGANYA DUNI TENA!!
sean_kingston_performing.jpgHARARE - Jamaican rapper Sean Kingston who already has a frosty relationship with ZimbabweanFacebook page that he threw $3 000 to people who attended his show at the Celebration Centre on Friday and at the Glamis arena on Saturday. journalists lied to the world on his
“I love my fans in Africa.I just threw $3 000 in the crowd - I love to give back man, best feeling ever,”Facebook page.
      However according to fans who attended both the Friday and Saturday shows nothing of that sort happened.
says his
    “I did not see any money. What the hell is the guy talking about. I can just tell you that the show was a boring performance, ” said Davis Takuneni, one of the fans who attended both shows.
Sean Kingstonn was in Zimbabwe last week..and...I like this guy, went to one of his shows once or twice,heck he's okay but well..I guess he was kind of a Disappointment in Zimbabwe...



AJARI YA NDEGE YAUWA WATU 25 INDOESIA

Authorities have announced that a regional transport aircraft from Indonesia crashed into the sea, in Papua province. 25 people have died.
The device, MA-60 type, Chinese manufacturing, “fell into the sea about 500 meters from the runway while it was in the landing stage” on Kaimana airport in a small town in West Papua, said ministerial official, Bambang Ervan.
The aircraft of the Indonesian Merpati Nusantara Company has “exploded” and disintegrated when reached the water, said Gunawan, a Navy officer in Papua.
“All passengers have died” and “15 bodies were recovered from the water.” The others are probably in the wreckage of the aircraft, according to him.




DADA YBHOKE AKIJIACHIA NHUKO BIG BROTHER
Mambo katika jumba la BBA 6 yameanza kuchangamka ambako wana dada wawili wa Kitanzania ambao wote ni watangazaji wa vituo vya televisheni nchini wanawakilisha.



MARIAH CAREY AWAPA MAJINA WATOTO WAKE 
kipindi ana mimba
Mwanamuziki wa majuu mariah carey amewapa majina watoto wake aliozaa na mumewe nick cannon,mtoto wa kwanza kapewa jina laMorocea scott cannon na mwngine anakwenda kwa jina la mariyln monroe cannon.
Watoto hap walizaliwa jumapili ilyopita huko Los Angels,usa,



NYETI KUILIKO NYETI TULIZONAZO

punda mwenye rangi ya pinki hutumika kutangaza moja ya mgahawa mmoja huko mexico.

Hawa je wanatangaza nini?,PINK...




kTUZO ZA TASWA KATIKA PICHA JANA USIKU
Mgeni rasmi,Makmau wa Rais,Dr Gharib Bilal pamoja na Waziri wa Vijana,habari,utamaduni na michezo Mh.Emmanuel Nchimbi wakiwa katika picha ya pamoja na washindi waliojinyakulia zawadi mbalimbali usiku wa huu kwenye hafla ya tuzo za TASWA zilizothaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti.
Mgeni rasmi,Makamu wa Rais Dr Gharib Bilal akimkabidhi tuzo kwa mchezaji wa jumla Bi.Mwanaidi Hassan anayecheza mchezo wa netiboli katika timu ya JKT Mbweni.Mwanaidi ndiye alijijinyakulia gari aina ya Toyota GX 100,iliyotolewa na kampuni ya bia ya Serengeti ambao ndiyo waliokuwa wadhamini wakuu wa tuzo hizo za kumsaka mwanamichezo bora wa Mwaka zilizoratibiwa na TASWA,kusho ni Waziri wa Vijana,habari,utamaduni na michezo Mh.Emmanuel Nchimbi akishuhudia tukio hilo.


Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa,akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali mara baada ya kuipokea tuzo yake ya heshima kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal,Mh Mkapa amesisitiza kuwa uwanja huo unapaswa uendelee kutunzwa vyema ili nchi yetu iendelee kuwa na kumbukumbu na urithi kwa vizazi vijavyo.


Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa, akipokea tuzo yake ya heshima kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, chama cha waandishi wa habari za michezo (TASWA) kimempa mzee Kkapa tuzo hiyo maalum ya heshima, kutokana na mchango wake katika michezo hasa ujenzi wa uwanja mpya wa Taifa,Mh Mkapa amesisitiza uwanja huo uendelee kutunzwa vyema ili nchi yetu iendelee kuwa na kumbukumbu na urithi kwa vizazi vijavyo,pichani kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda. Katika utoajiwa tuzo hizo mchezaji wa jumla ni Mwanaidi Hassan anayecheza mchezo wa Netball katika timu ya JKT
Mbweni.
Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa akipeana mkono wa pongezi na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Serengeti Breweries Ltd,Teddy Mapunda kwa kudhamini tuzo hizo za kuwapa heshima na kuwathamini wanamichezo wetu hapa nchini.Anaeshuhudia kwa nyuma ni Mgeni Rasmi,Makamu wa rais Dr Gharib Bilal.
Mwenyekiti wa bodi ya Serengeti (SBL),Mzee Marck Boman akimkabidhi tuzo mchezaji bora wa kiume wa timu ya Yanga Shadrack Nsajigwa.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Serengeti Breweries Ltd,Teddy Mapunda akimkaboidhi tuzo yake ya mwanariadha bora wa kiume Marco Joseph,mbele ya wageni waalikwa waliofika usiku huu,ndani ya Movernpic jijini Dar.
Meza Kuu ikiwa imechangamka,hapa ilikuwa ikifurahia jambo kutoka jukwaani.
Wasanii wa kikundi cha THT wakiwatumbuiza wageni waalikwa usiku huu.
Wanakamati wakijitambulisha moja baada ya mwingine.
Mwenyekiti wa chama cha Michezo (TASWA),Juma Pinto akizunguma mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kushuhudia utoaji tuzo kwa wanamichezo mbalimbali akiwemo na mwanamichezo bora kwa ujumla usiku huu ndani ya hotel ya Movernpick,jijini Dar.

Friday, May 6, 2011

LEO NDIO LEO..MBEYA YAWAKA MOTO..!!

wanachama wa chadema na mapango yao
Wanachama wengine wachadema wakiwa na mabango mbali mbali katika maandamano hayo ya Amani
Baadhi ya Magari yaliyo kuwepo katika msafara huo. 
Siku ya jumamosi inategemewa kuwa ya aina yake baada ya wabunge na viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) kuwasili kwaajili ya maadamano na mkutano mkubwa siku ya jumamosi hii mkoani mbeya pia harakati hizi zitaendelea mikoa mingine iliyotajwa punde.



MTIKILA AMJIA JUU RIDHIWANI
            MWENYEKITI wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, amemtaka mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwan Kikwete, kwenda mahakamani ndani ya siku saba alizosema vinginevyo atakwenda yeye kushtaki kutokana na utajiri alionao kwani ni kosa la jinai.
          , Mchungaji Mtikila alisema kwa taratibu za kisheria Ridhiwan anapaswa kuwapa kwanza ‘Demand Note Letter’( barua ya kuwataka wamwombe radhi au kufuta kauli zao) yeye na Dk. Willibrod Slaa.
“Ikiwa Ridhiwan hatafanya hivyo nitajipanga kwenda mahakamani kuwaeleza Watanzania namna mtoto huyo alivyo ni bilionea kupindukia kwa kumiliki mali nyingi zikiwemo fedha za Watanzania ambazo ni mabilioni katika akaunti zake, kampuni ya malori 150 na ya ujenzi pamoja na ghorofa za kupangisha,” alisema Mtikila.
       Kwa mujibu wa Mtikila, hawezi kuthibitisha kwa vielelezo aliyoyasema wakati alipokutana na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita kuhusu utajiri wa mtoto huyo wa Rais kama hatapelekewa barua hiyo.
         “Yawezekana Ridhiwan anazungumza maneno asiyoyafahamu kisheria na yeye tunasikia ni mwanasheria, kama unamtaka mtu akuombe radhi na kama akishindwa utampeleka mahakamani…maneno hayo kisheria huenda na demand note letter, sasa yeye hajatufikishia je tujipeleke? Alihoji Mchungaji Mtikila.
        Alieleza kuwa kama kweli Ridhiwan ni mwanasheria na anazifahamu sheria, siku ile aliyozungumza na waandishi wa habari angekuwa na barua hizo mkononi tayari kwa kuwapelekea na kusubiri matokeo yake.
        “Sasa naamini kwamba ni kweli Ridhiwan hajui sheria na kama angezifahamu, ningeshapata barua yangu mapema kwa kuwa anayafahamu makao makuu ya DP pale Ilala Msikitini na kama hazifahamu ofisi hizo angeniletea nyumbani kwangu Mikocheni B tuko jirani.”
    Juzi Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, naye alimtaka Ridhiwan kwenda mahakamani haraka kwa kuwa yaliyozungumzwa na kinywa chake yana ukweli. 



Lil' Kim Refuses to Name Her Dog After Nicki Minaj

nicki_minaj_lil_kim_dog.jpgThings have been relatively quiet between Nicki Minaj and Lil' Kim for the past few weeks, but the latest flare-up took place on Twitter, Monday night (May 2).
       Kim fired off a series of angry messages at Minaj in reply to a tweet from the Young Money rapper that reportedly read, "Lil Kim U Next." A look at Nicki's Twitter timeline will show no evidence of the tweet now, but it angered Kim enough to send her into a rage.
       After asking fans to help with choosing a name for her new dog, she took aim at Minaj after followers suggested she name the pup after her rival.
      "I would never name her "S---ty Garbaj"!!! My dog is way prettier than that b----!!!," she wrote. "What type of coward lame a-b---- tweets some s--- and then deletes it. REAL b-----s stand by what they say BOZO..."




KIM KADARSHIAN AKIRUSHA UFUKWENI NA MCHEZA BASKET(NBA)KRIS HUMPHRIES
 Mambo yakanoga hivi, utamu wa denda ukaenelea
 Malavidavi kwa sana huko mexico 




JIM JONES KAKATA NYWELE ZAKE 
  Jim Jones has had long hair since like 1996 or something and seemed as if the long perm turned cornrows were a staple of his look.  Well, now he has decided to go for the big chop.


Floyd Mayweather Jr. Facing More Charges


       Boxer Floyd Mayweather Jr. is facing new misdemeanor harassment charges accusing him of threatening two homeowner association security guards outside his Las Vegas home.
The charges filed Thursday in Las Vegas stem from an October dispute over parking with guards in the gated community where the undefeated prizefighter lives.
      Mayweather’s lawyer, Karen Winckler, didn’t immediately respond to messages from The Associated Press seeking comment.
Mayweather already faces a September trial on a misdemeanor battery charge stemming from allegations that he poked a 21-year-old guard in the face during a separate argument over parking tickets in November. He also faces unrelated felony charges in a domestic argument with his ex-girlfriend and two of their children last year.
          The new charges allege Mayweather threatened the guards after they cited several of his vehicles parked on the street in violation of association rules.
According to a police report, guard Miguel Burgos told police that Mayweather approached him and co-worker Aaron Ryan after they cited the cars and told them not to touch his vehicles.
The guards tried to explain the association’s parking rules, but Mayweather said he had 29 vehicles and they didn’t need to touch them, Burgos told police.
        “I already have a pending gun charge and I don’t want any problems, but my homeboys have guns and I’ll call them to come over and take care of you guys,” Mayweather said, according to Burgos’ account. “What do you guys want to do?”
Mayweather does not have gun charges pending against him.
        The guards said Mayweather then took the citations and put them on the windshield of the officers’ vehicle while laughing, repeating the threat several times and telling them to leave.
        Police said the guards left and called police, but told officers they didn’t want to press charges. Ryan called police two weeks later saying he wanted to move forward with the case.
Winckler told police in March that Mayweather would not be available for an interview.
       Mayweather, 34, is 41-0 in his professional career with 25 knockouts. His last fight was against Shane Mosley a year ago.

BREAKING NEWS; MSAFALA WA CHADEMA WAPATA AJARI...!!!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhsTZDQrOc7N9Tm8O-j1aM4XhyVmwpMSDQGoLAnkAg2yLU1CeRrlK5g8TZMudaQ_zj_FNKB03RqqtK15Pot9K8kXGo4y7NaKfE3w6THIP-JvGfUaaokvikIEKWbx_Y6q3E9cr2CyEUfdb4/s1600/halima.jpg
Mh.halima mdee
Ajari ya gari la mbunge wa kawe halima mdee kugongwa kwa nyuma na gari iliyokua ikimfuatia  nyuma kasi baada ya roli moja kumchomekea mbele ya gari la mbunge huyo ilibidi lifunge bleki gafla na kupelekea gari la nyuma kumgonga kwa nyuma ,safari iliendelea kama kawaida baada ya kizazaa iko kumalizika mkoani iringa ambapo wabungewa chadema wanaelekea mbeya kwajili ya mkutano wa maandamano baada ya kumalizika siku 21  kupitazilizotolewa na chadema. 

CIARA APATA BOYFRIEND MPYA ...!!!

Ciara na Amar'e Stoudemire walionekana pande za New York City wakiwa zero distance na kufunguka kuwa kwa sasa yuko  kwenye maisha Amare

RAIS MKAPA AJIKABIDHI KORTINI..!!

Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa

RAIS mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ameridhia kupanda kizimbani kumtetea aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na mwenzake aliyekuwa Ofisa Utawala wa ubalozi huo, Grace Martin wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

        Mahalu na mwenzake wanakabiliwa na mashtaka hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, wakidaiwa kuhujumu uchumi kwa kuisababishia Serikali hasara ya Euro 2,065,827.60.
        Wanadaiwa kusababisha hasara hiyo kupitia mchakato wa ununuzi wa jengo la ubalozi huo, wakati wa utumishi wao.
       Tayari Rais Mkapa amewasilisha mahakamani hapo hati yake ya kiapo akimtetea Profesa Mahalu na mwenzake kuhusiana na tuhuma hizo zinazowakabili.

      Kwa mujibu wa wakili wa kina Mahalu, Mabere Marando, ikiwa hati hiyo ya kiapo itakubaliwa na upande wa mashtaka na kisha kupokelewa mahakamani basi itatumika kama kielelezo cha ushahidi kwa upande wa utetezi bila Mkapa mwenyewe kulazimika kufika mahakamani.

        Lakini kama hati hiyo ya kiapo itakataliwa na upande wa mashtaka, basi Mkapa ameridhia kuwa yuko tayari kufika mahakamani mwenyewe na kutoa ushahidi wake mbele ya mahakama hiyo.
Katika hati hiyo ya kiapo, Mkapa amemtetea Profesa Mahalu kuwa amefanya naye kazi kwa muda mrefu na anamjua kuwa ni mtu mwaminifu, mtiifu na mchakapakazi.

       Mkapa alieleza katika hati yake hiyo kuwa mchakato wa ununuzi wa jengo hilo ulifanyika wakati wa uongozi wake na kwamba alikuwa akijua kila kilichokuwa kikiendelea kuhusiana na ununuzi huo na kwamba ulifanyika kwa mujibu wa sheria.

       Alifafanua kuwa mpango wa ununuzi wa jengo hilo ulikuwa ni utekelezaji wa Sera ya Serikali wa kuwa na majengo yake ya kudumu katika kila ubalozi kwa kununua au kujenga ikiwa ni njia ya kupunguza gharama za upangaji.
Aliongeza kuwa Serikali yake ilimpa Profesa Mahalu mamlaka yote ya kusimamia na kutekeleza mchakato wa ununuzi wa jengo hilo kupitia nguvu ya kisheria aliyopewa na Serikali yake.

        Mkapa alisisitiza kuwa kupitia utaratibu wa Serikali alikuwa akijua kuwa  taarifa ya uthamini wa jengo hilo iliyofanywa na Wizara ya Ujenzi ilikuwa ni Dola za Marekani 3.0 milioni wakati Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ilikadiriwa Euro 5.5 milioni

      “Kupitia utaratibu wa Serikali nilifahamu kuwa jengo hilo lilinunuliwa kwa gharama ya Dola za Marekani 3.0milioni  sawa na Euro 3,098,741.40,” alisema Mkapa na  kuongeza:
“Kupitia utaratibu wa Serikali nilikuwa nafahamu na hivyo kuidhinisha mchakato wote na taratibu za ununuzi wa jengo hilo lililoko Vialle Cortina d’Ampezzo 185 jijini Rome.”

      Mkapa pia alisema kuwa alitambua kuwapo kwa mikataba miwili katika ununuzi wa jengo hilo na kwamba yeye mwenyewe ndiye aliruhusu kufanyika kwa kuwa ilikuwa ni muhimu katika kutimiza maslahi ya taifa.
Pia Mkapa alisisitiza kuwa alikuwa na bado anatambua taarifa ya serikali bungeni ya Agosti 3, 2004  iliyoeleza na kuthibitisha kuwa taratibu zote za ununuzi wa jengo hilo zilifuatwa kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali na kwamba dalali alilipwa kikamilifu.



SPIKA MAKINDA AFIWA NA MAMA YAKE 

Mbunge wa Njombe-Kusini na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Anne Makinda amefiwa na Mama yake mzazi,Bi Tulikela Samnyuha (86) kilichotokea mkoani Dodoma
Mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumapili ya tarehe 8 May,2011 Njombe



 BEN KINYAIA NA AUNT EZEKIEL MAHABA MANENE

waigizaji wetu akiponda raha ndani ya bwawa la kuogelea huvu vinywaji laini viburudisha ndimi zao


Kikongwe abakwa akatwa sehemu za siri

        MKAZI wa Kijiji cha Njoro wilayani Kiteto mkoani Manyara, Bi. Mwajuma Selemani (70) amebakwa na watu wasiojilikana na kuchanwa chanwa sehemu za
siri na kitu chenye ncha kali.

     Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Njoro, Bw. Selemani Farandi amesema tukio hilo lilitokea Mei 3, mwaka huu, wakati bibi huyo akitoka shambani kwake kwenda nyumbani hivyo kukutana na vijana wawili ambao waliamtaka bibi huyo kuwauzia alizeti.


      “Hawa vijana walifika shambani na kumkuta mama akivuna alizeti walimtaka awauzie lakini mama lisema hauzi wakaondoka baada ya muda alirudi mmoja na kumtaka tena auze ndipo mama akapata wasiwasi na kulazimika kuanza safari kurudi njiani,” alisema Asha Iddi mtoto wa mama huyo.


      Alisema akiwa njiani mama huyo alijitokeza kijana ambaye hakufahamika na kumpiga 'ngwara' akaanguka hatimaye kumchania nguo za ndani na kutimiza kumbaka na kumchana chana sehemu za siri na kiti kinachodaiwa kuwa cha ncha kali.


“Pamoja na mama kubakwa kwa mujibu wa Daktari aliyempima ametueleza kuwa aliingiziwa kitu kigumu sehemu za siri kilichomfanya apate maumivu makali amayo kwa sasa yanampa shida hata kujisaidia haja kubwa na ndogo inamwia vigumu,” alisema  Bi. Asha. 
GARI LA TUZO YA TASWA HADHARANI 
      Baadhi ya viongozi wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na waandishi wa habari wakitazama gari ambalo mwanamichezo bora atapewa kesho katika sherehe za utoaji tuzo walio mahiri katika fani  hiyo. Meneja Mawasiliano na Habari wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) inayodhamini tuzo hizo, Teddy Mapunda (wa nne kushoto) alikabidhi gari hilo leo kwa uongozi wa TASWA katika hafla iliyofanyika Hotel ya Movenpick, Dar es Salaam. Kwa Mujibu wa TASWA thamani ya gari hilo ni sh. milioni 13. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya tuzo hiyo, Masoud Sanani.


Besigye apofuka macho apelekwaulaya kupata matibabu!!

Dr. Kizza Besigye
                 Kiongozi wa Upinzani nchini Uganda Dkt Kizza Besigye atapelekwa ng'ambo kwa matibabu zaidi.
Mkewe kiongozi huyo Bi Winnie Byanyima aliambia kuwa madaktari wanaomshughulikia mwanasiasa huo katika hospitali moja Mjini Nairobi wanahofia kuwa Besigye alipata madhara makubwa ya sumu kwenye ngozi na macho yake.
                 Kiongozi huyo wa upinzani alisafirishwa hadi Nairobi kwa matibabu zaidi baada ya kupigwa na polisi wa Uganda wakati wa kuzima maandamano aliyokuwa akiongoza ya kutembea kwa miguu hadi kazini kupinga kuongezeka kwa gharama ya maisha nchini Uganda.
                 Bi Byanyima amemuomba Rais Yoweri Museveni kufanya mashauriano na upinzani pamoja na viongozi wa Kidini ili kutafuta suluhu juu ya matatizo yanayoikumba Uganda badala ya kuwa timua nguvu kupita kiasi kutawanya maandamano.



 WAANDISHI BORA WAPEWA TUZO

Usiku wa kuamkia leo, katika ukumbi wa Mlimani City, wanahabari bora wa Magazeti, Runinga, Radio, Wapiga Picha na Wachora Katuni walitunukiwa kwa kupewa tunzo na zawadi mbalimbali kwa kuthamini kazi zao nzuri walizofanya mwaka jana. Tunzo hizo za kila mwaka zimeandaliwa na Bararaza la Habari Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na zimepewa jina la Excellence Journalism Awards Tanzania (EJAT). Pichani ni Mweneyekiti Mtendaji wa IPP Media, Bw. Reginald Mengi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi walioshinda sehemu ya tunzo hizo mara baada ya kukabidhi cheti na zawadi.
Mwandishi wa ITV, Festus Sigamonamo (kulia) akipokea tunzo yake kutoka kwa Bi. Fauziat Aboud
Majaji wasataafu wakiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Bi. Blandina Nyoni (kulia)
Bw. Mengi akiwa na Jaji Mstaafu, Mark Bomani
Mtangazaji wa TBC1, Masoud Masoud (kulia) akipokea tunzo yake
Mtangazaji wa Radio Mlimani (Tuma Dandi) kulia, akipokea tunzo yake baada ya kuibuka kidedea
Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One, Bi Joyce Mhaville (kulia) akimkabidhi tunzo mtangazaji Dorcas Raymond wa Channel Ten

Thursday, May 5, 2011

breaking news..!! CHADEMA WAZUA KIMBEMBE TENA!

Chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA)kimeazimia kufanya maandamano makubwa kutoa elimu kwa Umma kuhusiana mambo kadhaa ambayo chama hicho kinapinga mwenendo wake.
  Wachambuzi wa mambo ya KIsiasa wanasema kuwa moja ya ajenda ambazo wanategemea kusikia nyeti zilizojificha kuhusiana na utajiri wa ridhiwani kikwete ambao haundani na kipato chake toka apate ajira.
   Mikoa ambayo itapitiwa na mikutano hiyo ni Mbeya ,singida,rukwa,morogoro na mji wa sumbawanga kuanzia kesho.




MWILI WA OSAMA KUONYESHWA HADHARANI
Osama laying dead on hospital death bed
Osama Bin Laden Death Photo
   Wasiwasi mkubwa kuhusu ukweli wa mauaji ya mwanzilishi na Kiongozi wa Al-Qaeda Osama Bin Laden, serikali ya nchini hapa inatarajia kutoa picha za mwili wake zilizopigwa kabla ya kuzikwa.
    Tangu Rais Obama atangaze kuuawa na kuzikwa kwa Osama bin Laden, maoni mbalimbali yametolewa yakitaka kuwekwa wazi kwa mwili wake ili ukweli wa tukio zima la mauaji ueleweke duniani.
    Mkurugenzi wa Shirika la Kijasusi la CIA, Leon Panetta, alikiambia kituo cha televisheni cha NBC cha nchini hapa kuwa picha ya mwili wake itatolewa ili kumaliza utata huo.
    Kutolewa kwa picha hizo kunatokana na makubaliano yaliyofikiwa baada ya mvutano mkubwa uliotokea kati ya CIA na maofisa wa serikali juu ya wazo hilo.
    CIA hawakuwa na wazo la kutoa picha kutokana na mwili wake kuwa katika hali ya kutisha, kufuatia kuwa na majeraha makubwa aliyoyapata maeneo ya kifuani na usoni.
Taarifa zilizopatikana awali zilionyesha kuwepo kwa mkanganyiko kuhusu tukio zima la kuuawa kwa Osama huku Ikulu ya Marekani ikishindwa kueleza ni watoto gani wa Osama waliuawa.
     Taarifa nyingine za utata ni maelezo kuwa mke wa Bin Laden aliuawa kwa kupigwa risasi, huku ikiwa haijalezwa wazi kuhusu ulikopelekwa mwili huo.
     Dunia bado imebaki katika kiza kinene kinachohitaji mwanga wa ukweli kutokana na jana maofisa wa nchini hapa kufafanua kwamba mke wa Bin Laden hakuuawa na kusema mwanamke mwingine ndiye aliuawa katika shambulio hilo.
       Maofisa hao walisema mwanamke huyo huenda alikuwa mke wa Sheikh Abu Ahmed, ambaye alikuwa mfanyakazi wa mkewe Osama.
      Ingawa msemaji wa Ikulu, Jay Carney, aliweka wazi kuwa wakati wa shambulio hilo Bin Laden hakuwa na silaha, lakini maofisa walidai Bin Laden alijibu mapigo (alijihami) dhidi ya makomandoo.


WEMA SEPETU ATIWA MBARONI KWA UTOVU WA NIDHAMU






Aliyekuwa Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu (27) , mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo, Kinondoni kwa kosa la kutukana hadharani.


Ilidaiwa Mahakamani hapo kuwa mshitakiwa huyo alimtukana matusi ya nguoni msanii wa kizazi kipya, Raheem Rummy 'Rais wa masharobaro' ambapo mshitakikosa lake.


Hata hivyo mshitakiwa huyo alidai mahakamani hapo kuwa aliamua kumtukana mshitakiwa kwa sababu ya dharau zake alizokuwa anamfanyia.


''Mheshimiwa Hakimu si kawaida yangu kutukana ovyo ovyo, lakini hasira zimenifanya nifanye hivyo na ndiyo maana nimekubali kosa langu.


Mbele ya Hakimu Mariamu Masamalo, ilidaiwa na Karani Sharifa Dunia kuwa, Aprili 11 mwaka huu Kinondoni, mshitakiwa alimtukana mlalamikaji huyo na kesi imehairishwa mpaka Aprili 18 mwaka huu.
Wema Sepetu katika pozi.


CHRISS BEEZ AKANUSHA KUTAMANI NDOA NA KARRAUCHE TRAN

Chris Brown kuptia mtandao Twitter alizima uvumi uliokua umezagaa kuwa alimuomba mpenzi wake waoane wakati wa sikuu za Easter...
CHRIS BROWN AKIWA NA 'DEM WAKE' KARRAUCHE TRAN
Chis Brown inasemekana kuwa alimuambia dem wake Karrauche Tran kupitia kwenye simu kuwa anamuomba waowane lakini hakuwa na pete kwa wakati huo na mdada huyo kukubali,lakini Chris Brown akafunguka kuwa yeye ni mdogo sana kujihusisha na hizo issue za kuoa kwa sasa coz ndio kwanza ana miaka 21 tu!

Wednesday, May 4, 2011

BREAKING NEWZ...!! LUNDENGA NA CHIPUNGAELO KUTOANA MACHO..!!

   Rais wqa miss utalii tanzania Bw,Gideon chipungaelo ametupa lawama za wazi kwa mkurugenzi wa Lino Agency kuwa Bw Hashim Lundenga anamuhujumu katika michakato yake kwa kuwarubuni warembo wa miss utalii wafanye kazi na miss Tanzaia bila makuballiano yoyote.
     Lundenga alimjibu Chips kuwa anatakiwa kupeleka malalamiko yake BASATA na sio kulalamika kupitia vyombo vya habari ama kumshitaki kwa waandaji wa mashindano ya dunia.
     kwa jinsi navyowafahamu watu hawa wwili wanahekima na busara za kutatua tofaut zao,Anko na chips nyie ndio dira yetu sisi waandaji chipukizi tunajifunza mengi toka kwenu haina haja kuwapa watu faida malizeni kiutu uzima au vipi broo. 

 
SILYVIA SHALLY AKANUSHA KUMWAGWA NA NKANUMBA!!
Mrembo silyvia shally amekanusha habari zilizoandikwa kwenye blogu hii kuwa hana msongo wowote kimawazo  dhidi ya kumwagana na mume wake mtarajiwa steven kanumba,hiii ni kutokana na ukweli kwamba walizimiana sana enzi za uhai wa penzi lao.
    Silyvia alibainisha kuwa chanzo cha kumwagana si tamaa bali ni tatizo lililopo ndani ya penzi hilo lililobaki kuwa historia dhidi ya wawili hao ambapo kanumba anaonekana kama mwenye furaha zaidi baada ya kuachana na silyvia wakatri dada yetu anasonekana kuumia zaidi licha kudai hana time tena na muigizaji huyo maarufu barani Afrika.
    "sijaachwa na kanumba yeye ndiye alikuja home kuniomba msamaha sikumjibu lolote" alilalama kimwana huyo.
    Hata hivyo kanumba alitoa kauli moja tu "kaka mpenzi wangu ni pesa na nipo kwaajili ya pesa nizichange kwanza,sina time na kidosho huyo tena,anatapatapa tu mwili na roho yake vimeachanana nadhani".The great alipigilia msumali wa mwisho.



 BASTOLA YAMPONZA RAY NUSURA APATE KICHAPO TOKA RAIA

 Msanii wa Bongo Movies Vicent Kigosi "The Greatest" alizusha taflani mid-night flani pande za Club Billicanas akiwa na waigizaji wakike wa Bongo Movies Wema Sepetu na Jack Pentezel
Issue ilikua ni kuhusu parking pande hizo na kutokea kutoelewana kati yake na washikaji wengine na kuamua kutoa bastola na kupiga juu ili kuwatisha wasimzuru baada ya mzozo mkali kutokea maeneo hayo
Baada ya ray kufyatua risasi hewani Kila aliyekua karibu alitafuta uchochoro na baada ya hali shwari punde raia walimzingira na kumpa kipondo baridi kabla kuja askari na kumnusuru na kichapo hiko toka kwa raia. 

REAL MADRID YASHIDWA KUITAMBIA BARCERONA YATOKA SURUHU
Barcelona imejikatika tiketi ya kucheza fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya baada ya kutoka sare ya 1-1 na Real Madrid kwenye mchezo wa pili wa nusu fainali.
Pedro
Pedro
Katika mchezo wa kwanza uliojaa na misukosuko Barcelona ilipata ushindi wa mabao 2-0.
Pedro aliipatia Barcelona goli hilo, huku Marcelo akisawazisha bao hilo.
Barcelona sasa watapambana na mshindi kati ya Manchester United au Schalke 04.
Fainali itachezwa Mei 28 kwenye uwanja wa Wembley, jijini London.

Tuesday, May 3, 2011

KIBUTI CHA KANUMBA CHAMTESA SLYVIA SHALLY..!!

       mzimu wa penzi la kanumba kwa slyvia shally bado unamsumbua kiasi chakumpa msongo wa mawazo zaidi baada ya kupewa kibuti cha moja kwa moja.
    Wachunguzi wa mambo ya kimahaba wanasema kuwa slyvia alimwagwa kutokana na tabia yake ya kuendekeza tamaa zisizo na msingi angali anahudumiwa kila atakacho toka kwa kanumba.
        Dada yetu kapewa usafiri wa kuendea chuo na misele ya hapa na pale,anakaa mazingira mazuri nyumbani kwa staa huyo wa movie,matibabu ya hali ya juu sehemu wanapotibiwa mawaziri,goodtime zakufa mtu na fedha za kutosha lakini inadaiwa hakuridhika na bata zoote hizo.
     Aidha dada yetu nae aliwai kusema ananyanyasika kwa kumpenda superstar huyo kwani yuko bize muda mwingi lakini ni sababu za  wivu na si kweli kanumba hajatulia,swahiba katulia mimi namjua.
     Kwa sasa penzi lao liko chali na kanumba hana time tena na mademu wa kibongo kwani ameona ni wasaliti tu hata humfanyie kitu gani lakini atatoka tu,kilichobaki ni kuzichanga tu.
Kwa mara ya kwanza kanumba na slvia walikutana Club much more katika mchujo wa mamodo mwaka 2009 ndipo kila mmojawao akaonyesha dalili za kumrushia jcho la kumtamani mwenzake



Uswizi yapiga tanji mali za Gaddafi


Bw Hosni Mubarak
                  Uswizi imesema imepiga tanji takriban mali zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni moja za Kanali Muammar Gaddafi wa Libya na viongozi walioondolewa madarakani kutoka Misri na Tunisia.
Waziri wa mambo ya nje wa Uswizi Micheline Calmy-Rey alisema takriban dola za kimarekani milioni 960 zimepatikana.
        Waziri huyo alisema, kati ya hizo, kiwango kikubwa cha faranga za kifaransa milioni 410 zimehusishwa na aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak na washirika wake.
        Faranga nyingine zenye thamani ya milioni 360 zinaaminiwa kuwa za uongozi wa Kanali Gaddafi.
Na faranga milioni 60 zinamhusu aliyekuwa kiongozi wa Tunisa Zine al-Abidine Ben Ali na washirika wake.




MGANGA ATOKA MWANZA ATOA TIBA KWA BUKU MBILI JIJINI

Dawa ikiwa jikoni.
MGANGA wa kienyeji, Marwa Ndege Gonzaga, mkazi wa Mwanza, amejitokeza hadharani na kutangaza kuwa anatoa dawa ya kikombe yenye uwezo wa kutibu magonjwa sugu zaidi ya sita kwa gharama ya shilingi 2,000.
Gonzaga ameyataja magonjwa ambayo dawa yake inatibu kuwa ni vidonda vya tumbo, presha, kupooza, kutopata mtoto, kisukari na Ukimwi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Gonzaga ambaye jijini Dar es Salaam anapatikana Ilala, Karakata-Airport katika ofisi za Ediperry, alisema alianza kutibu tangu mwaka 1986.


Mganga huyo akichota dawa na kuwapa baadhi ya waandishi waliohudhuria mkutano huo katika Ukumbi wa Idara ya Habari. 




RIHANNA NA VIDEO MPYA HUKO JAMAICA

Rihanna teased her fans with a behind-the-scenes look at her island video shoot for her new single 'Man Down,' the latest from her fifth studio album 'Loud.'
rihanna_jamaica_man_down_photos.jpg

The Bajan babe chose to film the new video in Jamaica and tweeted all the way. "WELCOME TA JAMROCK!!! #projectmandown," she posted upon her island arrival. Rihanna teamed up with long-time partner in crime, director Anthony Mandler for the 'Man Down' video. Mandler began working with Rihanna in 2006 on her 'Unfaithful' video and most recently worked with the superstar on the set of 'Only Girl (In the World).' He has also worked with stars like Drake, Usher, Jay-Z, T.I. and John Legend.
"Eatin a roti, on my way to #JAMRock Rah Rah!!!!," she posted to her Twitter page on her way to the shoot (left). She tweeted another ... behind ... the scenes photo of her self in colorful, barely-there-bottoms and signature red hair with a pal "chillin on set" (right).
The singer made sure to stay relevant and on top of current events despite her mini island vacation away from the States -- she wrapped that video shoot and her series of tweets with a mash up of her 'Man Down' lyrics and a nod to the news of the Osama Bin Laden's death. "Obama Bama Bama...sry I meant, oh Mama Mama Mama, I just shot a man down #brrrap," she wrote earlier today (May 2).




MLA URODA AFUMANIWA KWENYE DANGURO
Mwanaume huyu wa nchini China amekuwa maarufu duniani kufuatia kusambazwa kwa picha zake online wakati akihatarisha maisha yake kwa kujaribu kushuka toka ghorofani akiwa uchi wa mnyama akiwakimbia polisi waliovamia danguro alilokuwa akijisevia uroda.

WAYNE ROONEY HATOCHEZA NUSU FAINALI UEFA

Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson atampumzisha Wayne Rooney katika mchezo wa nusu fainali ya Ubingwa wa Ulaya mzunguko wa pili dhidi ya Schalke 04 siku ya Jumatano.
Wayne Rooney
Wayne Rooney
Wakiwa wanaongoza kwa mabao 2-0 waliyopata katika mchezo wa mzunguko wa kwanza na huku wakikabiliwa na mchezo muhimu wa kuamua hatma ya ubingwa wa England dhidi ya Chelsea siku ya Jumapili, Ferguson anajipanga kupumzisha baadhi ya wachezaji wa kikosi chake cha kwanza.
Dimitar Berbatov huenda akaanza pamoja na Michael Owen katika safu ya washambuliaji wawili.
Fabio da Silva hata hivyo hatacheza, kutokana na kuumia mguu.
Mbrazili huyo aliumia siku ya Jumapili, Manchester United ilipolazwa bao 1-0 na Arsenal, matokeo yanayoufanya mpambano baina ya Man United na Chelsea katika uwanja wa Old Trafford kuwa muhimu zaidi kwa kuweka wazi nani hasa atakuwa katika nafasi nzuri ya kutwaa taji la ubingwa msimu huu.

BREAKING NEWS..!! OSAMA BIN LADEN KAZIKWA BAHARINI..!!

         The dilemma of what to do with Osama bin Laden's body appears to have been quickly resolved if reports that he has been buried at seaprove correct.
            Burying him on land could have led to his grave becoming a centre of contention as well as raising questions about where he should be buried.
        "Finding a country willing to accept the remains of the world's most wanted terrorist would have been difficult," a US official said, adding: "So the US decided to bury him at sea."
        Fears about Bin Laden's burial place turning into a shrine for Islamists were probably unfounded, since the Wahhabi/Salafi tradition rejects such things. Even Saudi kings are buried in unmarked graves.
         Senior US officials initially told news agencies that his body would be disposed of in accordance with Islamic tradition, which involves ritual washing, shrouding and burial within 24 hours.
          Although the swift burial complies with Islamic custom and should therefore avoid causing any offence in Muslim countries, the apparent haste could lead to claims that the person killed was not really Bin Laden – though the US authorities have taken DNA samples and appear to have no doubts.   The 24-hour rule has not always been applied by the US in the past. For example, the bodies of Uday and   Qusay Hussein – sons of the Iraqi dictator – were held for 11 days before being released for burial.
             Burial at sea is rare in Islam, though several Muslim websites say it is permitted in certain circumstances.
              One is on a long voyage where the body may decay before the ship reaches land. The other is if there is a risk of enemies digging up a land grave and exhuming or mutilating the body – a rule that could plausibly be applied in Bin Laden's case.
              For sea burial, according to alislam.org, the body should be lowered into the water "in a vessel of clay or with a weight tied to its feet". The website adds: "As far as possible it should not be lowered at a point where it is eaten up immediately by the sea predators


RIDHIWANI AUKANA UBILIONEA...DR SLAA KUJIBU MAPIGO?

            MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM), Ridhiwan Kikwete, amekanusha tuhuma zilizoelekezwa kwake juu ya kumiliki mali na mabilioni ya fedha.
Ridhiwan alikanusha madai hayo baada ya nyakati tofauti Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa na Mchungaji Christopher Mtikila kutoa madai kuwa Ridhiwan pamoja na kumaliza shule miaka michache iliyopita, hivi sasa ni tajiri bilionea.
          Akizungumza jana jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari, Ridhiwan, alisema habari hizo si za kweli bali za kizushi na kwamba zimejaa uongo unaolenga kumchafua yeye pamoja na baba yake Rais Jakaya Kikwete huku wakipandikiza chuki kwa umma.
         Ridhiwan alisema kwa sasa anamiliki shamba la hekari moja na nusu, gari aina ya Toyota Cami na akaunti tatu tofauti zilizo katika benki ya NBC, Stanbic na CRDB.
        Alipoulizwa mbona anaonekana akitembelea magari ya kifahari, mtoto huyo wa Rais alisema: “Hapa mjini unaweza kumuona mtu amevaa suti ukadhani ya kwake kumbe ameazima. Mimi nina marafiki wengi, huwa wananiazima magari yao nitembelee, juzijuzi hapa nilikuwa na benzi ya rafiki yangu….jamani miundombinu ya mjini si mnaijua?”
        Alisema kutokana na kuwaheshimu wazee hao na umri walionao ni bora watumie busara na kujitokeza ili watoe ushahidi juu ya hayo waliyoyasema na hatua zaidi zichukuliwe.
Aliongeza kuwa iwapo itadhihirika kuwa habari walizozieleza ni za uongo basi atakuwa tayari kuwasamehe; lakini alidai leo atawafikishia barua wazee hao ambapo ndani ya wiki mbili amewataka wathibitishe taarifa hizo walizozitoa juu yake.
        “Kama haitoshi narudia tena niliwaahidi ushirikiano na endapo watataka ili kuthibitisha yote hayo waliyosema na hata yale wanayoyasikia, wakithibitisha habari walizopewa ni za uongo basi wasisite kuueleza umma,” alisema Ridhiwan.


STL ATIMBA UJERUMANI NI KWAJILI YA NUSU FAINALI

            Yule  Rapper wa kike aliweka maskani yake nchini Norway,Stella Mwangi aka STL toka kenya amewasili nchini Ujerumani kwenye nusu fainali za Euro Vision iyakayofanyika mjini Dusseldorf tarehe 10 May2011
STL anaiwakilisha Norway na anatarajiwa ku-perform track yake kali ya Haba Haba na atashindana na artist toka Albania,Finland,Georgia,Russia,Serbia, Switzerland,Armenia,Poland na Uturuki na kama akipita ataingia fainali itakayofanyika May 12,2011
STL ana track kali kama Take It Back na Biashara na nyimbo hizo zimetumika kama soundtracks kwenye movie za American Pie,Save the Last Dance naCSI New York

WATU 300 WAZAMA KWENYE MAJI DRC

Mitumbwi nchini DRC
            Zaidi ya watu 100 wanahofiwa kufa baada ya chombo walimokuwa ndani kuzama katika Ziwa Kivu, kusini mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
           Mwandishi watu, amesema ajali hiyo ilitokea katika mji wa Tshikapa, Kusini mwa DRC. Ajali hiyo ilitokea jumapili usiku.
          Mashua hiyo ya kusafirisha mizingo inasemekana ilizama ikiwa na zaidi ya watu 300.
          Maafisa wanasema idadi kamali ya watu waliofariki haijulikana. Hata hivyo watu 30 wanasemekama wamenusurika baada ya kuogelea hadi kwa ufukwe wa ziwa hilo.
         Ajali ya sasa imetokea wiki moja baada ya watu 50 kufa katika ziwa hilo upande wa Mashariki, pale mtumbwi wao ulipozama. Shughuli za uokozi zinaendelea.



Wow, this chick has to be in the running for being one of the baddest in the game right now.  Just look at those abs!  Jordin Sparks is killin em’ right now and we’re not made she’s sharing this picture.

Monday, May 2, 2011

MARIAH CAREY AJIFUNGUA MAPACHA..!!


 Furaha imeongezeka zaidi katika familia ya Nick canoon,Jumamosi ya tarehe 30 April 2011 mnamo saa 12:07 za mchana kwa saa za Marekani jijini Los Angeles baada ya Mariah Carey kujifungua watoto mapacha baby ambapo kulwa ni wa kike na doto ni wa kiume.
Carey amejifungua salama na hii ili kukamilisha furaha ya ndoa yao Mariah Carey alikua anasikiliza wimbo wake wa We Belong Together! huku mumewe akisikilizia kwa chati,lakini watoto hawa bado hawajapewea majina.