Ridhiwan alikanusha madai hayo baada ya nyakati tofauti Katibu Mkuu wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa na  Mchungaji Christopher Mtikila kutoa madai kuwa Ridhiwan pamoja na  kumaliza shule miaka michache iliyopita, hivi sasa ni tajiri bilionea.
            Akizungumza jana jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari,  Ridhiwan, alisema habari hizo si za kweli bali za kizushi na kwamba  zimejaa uongo unaolenga kumchafua yeye pamoja na baba yake Rais Jakaya  Kikwete huku wakipandikiza chuki kwa umma.
           Ridhiwan alisema kwa sasa anamiliki shamba la hekari moja na nusu,  gari aina ya Toyota Cami na akaunti tatu tofauti zilizo katika benki ya  NBC, Stanbic na CRDB.
          Alipoulizwa mbona anaonekana akitembelea magari ya kifahari, mtoto  huyo wa Rais alisema: “Hapa mjini unaweza kumuona mtu amevaa suti  ukadhani ya kwake kumbe ameazima. Mimi nina marafiki wengi, huwa  wananiazima magari yao nitembelee, juzijuzi hapa nilikuwa na benzi ya  rafiki yangu….jamani miundombinu ya mjini si mnaijua?”   
            Alisema kutokana na kuwaheshimu wazee hao na umri walionao ni bora  watumie busara na kujitokeza ili watoe ushahidi juu ya hayo waliyoyasema  na hatua zaidi zichukuliwe.   
   Aliongeza kuwa iwapo itadhihirika kuwa habari walizozieleza ni za  uongo basi atakuwa tayari kuwasamehe; lakini alidai leo atawafikishia  barua wazee hao ambapo ndani ya wiki mbili amewataka wathibitishe  taarifa hizo walizozitoa juu yake.
          “Kama haitoshi narudia tena niliwaahidi ushirikiano na endapo watataka  ili kuthibitisha yote hayo waliyosema na hata yale wanayoyasikia,  wakithibitisha habari walizopewa ni za uongo basi wasisite kuueleza  umma,” alisema Ridhiwan.
STL ATIMBA UJERUMANI NI KWAJILI YA NUSU FAINALI 
 
             Yule  Rapper wa kike aliweka maskani yake nchini Norway,Stella Mwangi aka STL toka kenya  amewasili nchini Ujerumani kwenye nusu fainali za Euro Vision  iyakayofanyika mjini Dusseldorf tarehe 10 May2011
 STL  anaiwakilisha Norway na anatarajiwa ku-perform track yake kali ya Haba  Haba na atashindana na artist toka  Albania,Finland,Georgia,Russia,Serbia, Switzerland,Armenia,Poland na  Uturuki na kama akipita ataingia fainali itakayofanyika May 12,2011
 STL  ana track kali kama Take It Back na Biashara na nyimbo hizo zimetumika  kama soundtracks kwenye movie za American Pie,Save the Last Dance naCSI  New York
WATU 300 WAZAMA KWENYE MAJI DRC
            Zaidi ya watu 100 wanahofiwa  kufa baada ya chombo walimokuwa  ndani kuzama katika Ziwa Kivu, kusini  mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
           Mwandishi watu, amesema ajali hiyo ilitokea katika mji wa Tshikapa, Kusini mwa DRC. Ajali hiyo ilitokea jumapili usiku.
          Mashua hiyo ya kusafirisha mizingo inasemekana ilizama ikiwa na zaidi ya watu 300.
          Maafisa wanasema idadi kamali ya watu  waliofariki haijulikana. Hata hivyo watu 30 wanasemekama wamenusurika  baada ya kuogelea hadi kwa ufukwe wa ziwa hilo.
         Ajali ya sasa imetokea wiki moja baada ya watu  50 kufa katika ziwa hilo upande wa Mashariki, pale mtumbwi wao  ulipozama. Shughuli za uokozi zinaendelea.
Wow, this chick has to be in the running for being one of the baddest in the game right now. Just look at those abs! Jordin Sparks is killin em’ right now and we’re not made she’s sharing this picture.
 
 

No comments:
Post a Comment