Msanii wa kizazi kipya ajulikanae kama Diamond a.k.a The platnum inasemekana amekubwa na msongo wa mawazo kiasi cha kushidwa kufanya mambo yake kama ilivyo ada kutokana na kumwagwa na mrembo Wema sepetu.
Rafiki wa karibu wa msanii huyo waliwahi kumuonya achane mapema na demu huyo kwani yupo kimaslahi zaidi ila yeye alilemaza shingo na kudhani kuwa alikuwa akipendwa kwa dhati na kisio lake la kumuoa Wema litatimia kumbe ndo analisogelea jumba bovu.
MARY JOEL VODACOM MISS ARUSHA CITY CENTER 2011
Mkuu wa IMF azuiliwa korokoroni New York
Mkuu wa Shirika la IMF Dominique Strauss-Kahn
Mkuu wa Shirika la fedha duniani  ( IMF ) ,Dominique Strauss-Kahn, amezuiliwa katika gereza moja la  wafungwa sugu ya Rikers Islands mjini New York, kwa tuhuma za kujaribu  kumbaka mhudumu wa hoteli.
Jaji amesema kulikuwa na tisho la Strauss-Kahn,  mwenye umri wa miaka 62,  kutoroka iwapo angeachiliwa kwa dhamana.   Mkurugenzi huyo alikamatwa jumamosi iliopita punde baada ya kuabiri  ndege. Baadaye alishtakiwa kwa kujaribu kumbaka mhudumu wa hoteli moja  mjini New York.
Strauss-Kahn anakabiliwa na mashtaka saba na huenda akapewa kifungo cha hadi miaka 25 jela ikiwa atapatikana na hatia.
Mkuu huyo wa shirika la IMF amekanusha mashtaka dhidi yake.
Mawakili wake wameelezea kukasirishwa kwao baada ya kunyimwa dhamana , lakini wakasema mteja wao hatimaye ataondolewa lawama.
''Makabiliano ndiyo yameanza'', wakili wa upande wa utetezi Benjamin Brafman aliiambia mahakama.
Kutokana na kuzuiliwa kwake, Strauss-Kahn  alishindwa kuhudhuria mkutano wa mawaziri wa fedha kutoka umoja wa ulaya  mjini Brussels, Ubelgiji ambako mkopo wa kunusuru uchumi wa Ureno, wa  kiwango cha dola milioni mia moja na kumi uliidhinishwa.
Nchi ya Ureno imekuwa ya tatu inayotumia sarafu  ya Euro kupokea msaada kutoka kwa umoja wa ulaya na shirika la IMF,  baada ya Ugiriki na Ireland.
RIHANNA AJIPEREKA KWA CHRIS BROWN?!
 
 RIHANNA 
Rihanna  ameanza kujigonga kwa mpenzi wake wa zamaniChris Brown baada               ya juzi Ijumaa kumfata kwenye mtandao wa Twitter na Chris Brown naye    kumjibu faster....

CHRIS BROWN 
RiRi  alikua hawasiliani na Chris Brown kwa miaka 2 sasa tangu mwaka 2009,            na ni ajabu kwa kumpata coz yeye ana twitter followers kama  milioni 5 hivi                na baadaye Rihanna akajishitukia na  kutupia kwenye twitter kuwa watu wasije wakafikiria vingine coz ni  twitter tu na kwa sasa Chris Brown amemaliza tour  yake ya nchini  Australia na kwa sasa ana-shoot video mpya na Justin bieber iitwayo Next  to You jijini Los Angeles  
 
 

No comments:
Post a Comment