It's called "This Ain't Osama bin Laden XXX" -- and the porn studio claims Osama's secret porn stash was a major inspiration ... telling us, "We're pretty sure from what we've heard that bin Laden was a big fan of Hustler. He was looking at porn, now porn is looking at him."
T-PAIN AMZIMIA KESHA INOMA NOMA..!!
Msanii Tallahassee Pain  "T-Pain" na Mkali wa Pop/Female Rapper Ke$ha wameonekana wamepiga picha ya kimahaba  na kwa sasa kuna uvumi kuwa wanatupa mbicji 
 T-Pain  na Ke$ha walionekana jijini Las Vegas,na walikuatana weekend moja  kwenye show ya Wango Tango na T-Pain na kuanza kumfukuzia.
  kutupia kwenye Twitter T-pain alisema “Usiku wa jana nilimzimia  sana Ke$ha,wala siku-share nae mapenzi,ila namzimia coz anajua  kutupia akitaka kufanya showz” na baadaye Ke$ha naye akajibu “hata mimi  nakuzimia T-Pain,usikonde wala nini” na baadaye kwenye tweeter zikatupiwa picha zao zilizoandikwa         K-Pain aka Ke$ha-Pain.
HALI TETE KWA WILLIAM LUKUVI NA CYRIL CHAMI
Mh.William Lukuvi 
Kwa mara nyingine,KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk.  Willibrod Slaa, amewataja vigogo na watendaji wa serikali wakiwamo  mawaziri wawili na wabunge akiwatuhumu kufanya ufisadi wa kujigawia  vitalu vya uvunaji magogo katika msitu wa taifa uliopo Mufindi mkoani  Iringa.
   Miongoni mwa aliowataja ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,  William Lukuvi na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, huku  akisisitiza kuwa wamepata vitalu hivyo ‘kifisadi’.
   Dk. Slaa aliwataja mawaziri hao na watuhumiwa wengine wakati  akihutubia maelfu ya wakazi wa Mafinga katika mfululizo wa mikutano ya  hadhara na maandamano ya chama hicho yaliyoingia mkoani hapa jana.
   Alisema hatua ya mawaziri hao kumiliki vitalu hivyo si haki, kwani  inasababisha kuwapo mgongano wa kimasilahi baina yao na msitu huo ambao  kwa nafasi zao kama viongozi wa kiserikali walipaswa kuusimamia kwa haki  na uwazi ili uwanufaishe wananchi, hususan wakazi wa Mufindi.
   Akifafanua hoja yake hiyo, Dk. Slaa alisema Dk. Chami kwa nafasi yake  kama Waziri wa Viwanda na Biashara, ndiye mwenye jukumu la moja kwa moja  kusimamia haki kwenye msitu huo unaotumiwa pia na Kiwanda cha Karatasi  cha Mufindi Paper Mills, lakini naye amechukua vitalu tena katika  utaratibu aliosema si wa wazi.
   Alisema mwaka jana waziri huyo akiwa Naibu Waziri wa Viwanda na  Biashara ndiye aliyeongoza kamati maalumu ya serikali iliyokwenda  Mufindi kuchunguza mgogoro wa kiwanda hicho pamoja na msitu kinaoutumia,  lakini kinyume cha kanuni za kibunge, kiongozi huyo wa serikali sawa na  wenzake akiwamo William Lukuvi aliowataja, hawakusema wazi kama wana  masilahi katika msitu huo.
   “Naitaka serikali ieleze ugawaji huu wa vitalu vya msitu wa Mufindi  ulitangazwa lini na utaratibu gani wa uwazi ulitumika ili kila Mtanzania  wakiwamo wananchi wenyewe wa Mufindi wawe na haki ya kushindania vitalu  hivyo.
   “Pili, namtaka Chami na viongozi wengine wa kiserikali waliochukua  vitalu vya msitu huo wajieleze kwa nini wasiwajibishwe kwa kumiliki  vitalu vya msitu bila kutangaza wazi masilahi waliyonayo ya kiuongozi  katika msitu huo.
   “Tutawasha moto bungeni mpaka haki ya wananchi na msitu wao ipatikane,  hawa ni mafisadi. Wakituzidi kwa wingi wao bungeni, basi tutafanya  maandamano yasiyokoma nchi nzima hadi mafisadi hawa wawajibishwe na haki  za wananchi zitimizwe,” alisema Dk. Slaa na kushangiliwa na umati wa  watu.
Mkuu wa IMF Ajiuzulu
Mkuu wa IMF Dominique Strauss-Kahn mahakamani
Mkuu wa shirika la fedha duniani, Dominique Strauss Kahn amejiuzulu.
Taarifa hiyo ya kujiuzulu kwa Strauss Kahn imechapishwa katika wavuti wa shirika hilo.
Anasema amejiuzulu  ili atumie muda uliobakia  kujitea katika kesi inayomkabili ya kujaribu kumbaka mwanamke mmoja  mjini New York.
Strauss Kahn ametuma taarifa yake kwa bodi ya  shirika hilo. Amesema kuwa anakanusha mashtaka yote dhidi yake na  amesikitishwa na kisa hicho kilichomkabili.
Shirika hilo limesema kuwa litatangaza hivi  karibuni utaratibu wa kumteua mkurugenzi mpya. Kwa sasa John Lipsky  ataendelea kuwa kaimu Mkurugenzi mkuu wa IMF.
Awali waziri wa fedha wa Marekani amesema kuwa  mkuu wa shirika la fedha duniani (IMF), Dominique Strauss-Kahn, ambaye  anakabiliwa na mashtaka ya kujaribu kumbaka mhudumu wa hoteli, hawezi  tena kuendesha shughuli za shirika hilo.
Timothy Geithner ametoa wito kwa IMF kumteua rasmi kaimu mkuu wa shirika hilo.
Bwana Strauss-Kahn anazuiliwa katika jela moja  mjini New York baada ya kukamatwa hapo jumamosi kwa kosa la kujaribu  kumbaka mhudumu wa hoteli moja.
Strauss-kahn ambaye amezuiliwa katika gereza la  wafungwa sugu la Rikers Islands mjini New York yupo chini ya ulinzi  mkali kuchunga asijiue. Hii ni baada ya kufanyiwa uchunguzi wa  kimatibabu.
Wakili wa mwanamke huyo kutoka Guinea, Afrika  Magharibi,  anayemtuhumu Strauss-Kahn, amesema mteja wake amepata  mshutuko ambao sio wakawaida.
Wakili huyo ameongeza kuwa kwa sasa yupo mafichoni  na kwamba anajihisi ''Yuko pekee duniani''.
Strauss-Kahn, mwenye umri wa miaka 62,  anakabiliwa na mashtaka saba dhidi yake na iwapo atapatikana na hatia,  atahukumiwa kifungo cha hadi miaka 25 jela.
 AMBER ROSE NA MAUZO YA FRONT PAGE
Amber rose amepata shavu la kuuza front page katika jarida la king kwa mara nyingine.
 
 



No comments:
Post a Comment