Bw" Ghannouchi" atakiwa kujiuzulu-Tunisia
Maandamano ya kuipinga serikali ya mpito nchini Tunisia yanaendelea kumshinkiza Waziri Mkuu Mohammed Ghannouchi kuachia madaraka.
Watu hao walianza kuandamana katika eneo la asili la Mohamed Bouazizi, kijana ambaye kifo chake ndicho kilichoanzisha ghasia zilizosababisha Rais Ben Ali kukimbia siku kumi baadae.
Waratibu wa maandamano hayo wamesema wataendelea kukaa nje ya makao makuu ya serikali mjini Tunis, mpaka mawaziri wote wenye uhusiano na Bwana Ben Ali watakapotolewa madarakani.
Bw Ghannouchi ameahidi kung'atuka madarakani baada ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika baada ya miezi sita.
Chama cha wafanyakazi maarufu nchini Tunisisa, UGTT, kimeunga mkono maandamano hayo yaliyoanza Jumamosi mjini Menzekl Bouzaiane - mji ulioshuhudia kifo cha kijana huyo mwezi wa Disemba.
'Lengo la maandamano haya ni kuiangusha serikali,' alisema Rabia Slimane, ambaye ni mwalimu na anashiriki katika maandamano hayo.
Kuna hisia kuwa maandamano ya aina hii yataanza katika nchi zingine.
Nchini Algeria, polisi waliwatawanya takriban waandamanaji 300 waliokuwa wakitetea haki ya kuwa na uhuru zaidi, siku ya Jumamosi.
Pia, kumekuwa na maadamano nchini Yemen dhidi ya utawala wa Rais Ali Abdullah Saleh.
MAMBO YA MAPACHA WATAU -MZALENDO PUB
Hizi ni bata za weekend hii na bendi ya mapacha watatu
No comments:
Post a Comment