JIJI la Mwanza jana lilikumbwa na machafuko baada ya machinga kufanya vurugu na kuandamana wakipinga kuondolewa kufanya biashara katika maeneo ya mjini kati. Vurugu hizo zilisababisha kufungwa kwa maduka katika maeneo mbalimbali mjini hapa, kuvunjwa vioo vya magari, maduka na baadhi ya barabara kutopitika kwa muda huku kituo kidogo cha Polisi Pamba, kikinusurika kuvamiwa na kuchomwa moto.
Pamoja na vurugu hizo, serikali mkoani Mwanza imewataka wafanyabiashara hao kuheshimu sheria na kanuni za mipango miji zilizowekwa pia maafikiano yaliyofikiwa baina ya viongozi wao, uongozi wa mkoa na halmashauri ya jiji hilo .
Nje ya jengo hilo , waliweka vizuizi vya mawe katika barabara zote zinazoingia jiji na kulazimisha pikipiki na magari yaliyokuwa yakipita kurudi yalikotoka huku wakiwa na chupa za maji ya kunawa kwa ajili ya kujikinga na moshi wa mabomu iwapo polisi wangewafyatulia mabomu ya machozi.
Baada ya mazungumzo hayo, Kandoro aliwaambia machinga kuwa hapingani na sheria na kanuni za mipango miji kwa kuruhusu machinga wafanye biashara katika maeneo waliyoruhusiwa, isipokuwa wafuate masharti waliyopewa katika maeneo ya Makoroboi, Mirongo, Vitunguu Soko Kuu na Mlango Mmoja.
Baada ya kuondoka katika ofisi za halmashauri hiyo, machinga waliingia mitaani tena na kuanza vurugu wakivamia maduka na kuvunja vioo kwa madai kwa wafanyabishara wengine, hawatafanya biashara.
No comments:
Post a Comment