UPO mpasuko wa wazi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kama ambavyo vikao na matamko mbalimbali yanayotoka kwenye chama hicho yanavyoonyesha, hasa kuhusu sakata la serikali kulipa mabilioni ya shilingi kwa kampuni ya Dowans.
Baada ya kauli ya Umoja wa Vijana wa CCM juzi kumtaka mwenyekiti wa chama hicho, Jakaya Kikwete, achukue maamuzi magumu kukinusuru chama, hasa kwa kuwachukulia hatua kali vigogo wawili, Waziri wa Ushrikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, Kamati Kuu ya chama hicho imetoa tamko la onyo kwa vijana hao.
Katibu Mwenezi John Chiligati aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ‘amri’ ya vijana hao kwa Rais Kikwete kwamba awachukulie hatua Sitta na Mwakyembe ni suala la serikali na si la chama.
Alisema kufanya hivyo ni kuingilia mamlaka ya Rais iliyowekwa kwa mujibu wa sheria ambayo hutumika kuongoza nchi na kwamba Kamati Kuu inaiachia serikali kuliangalia hilo.
Huku akisisitiza kwamba tamko la UVCCM ni haki ya kitengo hicho cha chama, alisema Kamati Kuu itawaelimisha zaidi vijana hao na akasisitiza: “Ni lazima maamuzi ya chama yaheshimiwe.”
Alisema maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu iliyokutana Januari 20, mwaka huu, imejadili masuala mbalimbali ikiwemo hali ya siasa nchini na kusema kuwa ni lazima serikali iheshimu maamuzi ya mahakama ya kimataifa ya biashara kuhusu mgogoro wake na TANESCO, unaolazimu serikali kuilipa Dowans fidia ya sh 94 bilioni.
Alisema hukumu hiyo ni funzo tosha kwa serikali, hasa katika kuingia mikataba ya miradi ya maendeleo na hata inapotaka kuivunja ni lazima ifuate sheria zilizopo, ikiwa ni pamoja na kufanya makubaliano yenye tija kwa taifa.
“Tunajua hili lililotokea hasa kutokana hukumu ya TANESCO kwa Dowans, tunajua kila Mtanzania ana haki ya kutoa maoni lakini kubwa ni uamuzi wa kisheria na hatuna budi kuuheshimu; kwanza tusubiri uamuzi wa pingamizi lililowekwa Mahakama Kuu ndipo taratibu nyingine zifuatwe na hata tamko la UVCCM ni maoni yao tutakaa nao sisi kama chama na kuwaelekeza taratibu za chama, “ alisema Chiligati.
Alisema TANESCO ilifanya kosa, na Kamati Kuu inaisisitizia serikali umuhimu wa kuzingatia na kuheshimu sheria, ikiwamo maamuzi yaliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Biashara (ICC).
Hata hivyo, alisema pamoja na hukumu hiyo, ni vema serikali ikasubiri uamuzi wa mahakama kuhusu pingamizi lililofunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu (LHRC) juu ya malipo hayo.
Sakata ya Dowans
Chiligati, alisema Kamati Kuu imeona ni vema kuheshimu maamuzi ya Mahakama na hakuna budi kutekeleza hukumu hiyo ila ni busara kwa serikali kutolipa malipo hayo ya bilioni 94 hadi uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu pingamizi lililowekwa na Kituo cha Haki za Binaadamu liamuliwe ndipo taratibu nyingene zifuate kwa mujibu wa sheria.
Migomo ya Wanafunzi, Wahadhiri wa Vyuo Vikuu nchini
Alisema ni vema serikali ifuatilie kwa makini suala hilo na kulipatia ufumbuzi wa haraka na kama kuna tatizo la malipo ilitakiwa kulipwa kwa wahusika ili kuondokana na hali ya migomo ya kila mara.
Alisema ufuatiliaji wa karibu utasaidia kubaini matatizo na hata kupata suluhu ya kudumu kwa haraka na ikiwezekana kumaliza hali hiyo.
Ila ni muhimu kwa wanafunzi na wahadhiri kuwa na utaratibu wa kutoa matatizo yao kabla na kuacha utaratibu hadi mambo yanapoharibika.
Aidha alisema kukaa meza moja mara kwa mara baina ya serikali na wahadhiri kutasaidia kujadiliana kwa kina na kugundua matatizo na kuyapatia ufumbuzi kwa wakati.
Vurugu za Arusha
Katibu Mwenezi huyo wa CCM, alisema kamwe chama chake hakiko tayari kurudia uchaguzi wa Meya kwani uchaguzi ulifuata taratibu zote za kisheria mbali ya CHADEMA kususia uchaguzi huo.
Alisema katika tatizo hilo ni vizuri CHADEMA wakawa wakweli kwani waliweka pingamizi dhidi ya Mbunge wa Viti Maalum, Mary Chatanda na kusahau kuwa CCM ina wajumbe 16, huku wao wakiwa na wajumbe 14 na TLP mmoja.
Alisema kitendo kilichotokea Kamati Kuu imekijadili kwa kina na kusikitishwa na vurugu hizo zilizopelekea kupoteza maisha ya watu watatu na wengine kujeruhiwa kutokana na kadhia hiyo.
“Ni vizuri CHADEMA wakawa wakweli wamesahau Mbunge wa Viti Maalum hupangiwa eneo la kazi na chama chake, kama wao walivyofanya kwa wabunge wao wawili hali ya kuwa wanaishi Moshi mjini lakini wakapelekwa wilayani Hai na wakashiriki kupiga kura, sasa tatizo liko wapi mbona sisi hatujalalamika ila wao tu ndio wafanye hivyo!?” alisema Chiligati.
Maadhimisho ya miaka 34 ya CCM
Kada na kiongozi huyo wa CCM, alisema Febreuari 5, mwaka huu, CCM itatimiza miaka 34 ya kuzaliwa kwake ambapo sherehe za maadhimisho hayo zitazinduliwa jijini Dar es Salaam Februari Mosi, mwaka huu na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Amani Abeid Karume.
Alisema kuwa katika maadhimisho hayo wameyataka matawi ya CCM nchi nzima kufanya mikutano mikuu na kufanya tathmini ya kina namna ya walivyoshinda uchaguzi na hata maeneo waliyoshidwa kuwa wakweli.
Alisema maadhimisho hayo yatakwenda sambamba na mikutano ya hadhara kwa nchi nzima kwa kuwashukuru wananchi kwa kuichagua CCM katika Uchaguzi Mkuu uliopita na Februari 5, kilele chake kufanyika mkoani Dodoma na kuhitimishwa na Rais Kikwete kwa kupokea maandamano ya mshikamano.
Semina kwa wabunge wa CCM
Alisema CCM itafanya semina kwa wabunge wake 260 leo katika Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam ili kuwapa uelewa wa namna ya Bunge na kanuni zake kwa mujibu wa sheria.
Alisema Uchaguzi uliopita zaidi ya asilimia 60 ya wabunge wake ni wapya na 40 ni wa zamani hivyo ugeni wao CCM imeona ni muhimu kuwafanyia mafunzo hayo ili kwenda sambamba na kasi na viwango vya wabunge wa Chama cha Mapinduzi.
Korea kusini yawaokoa mateka baharini
Makamanda wa jeshi la wanamaji la Korea kusini wamevamia meli ya mizigo iliyokuwa imetekwa na maharamia katika bahari ya Arabia.
Lt Jenerali Lee Sung-ho alisema mabaharia wote 21 wa meli ya Samho-Jewelry inayomilikiwa na Korea kusini wameokoloewa.Jeshi hilo la majini limesema wanane miongoni mwa maharamia waliuawa na watano wamekamatwa.
Korea kusini hufanya doria ikiwa ni sehemu inayohusisha mataifa mengi ya kupinga uharamia eneo hilo- ambapo ilipeleka meli ya kivita baada ya meli hiyo kutekwa siku ya Jumamosi.
Shughuli hiyo ya uokoaji ilifanyika takriban kilomita 1,300 kutoka pwani ya Somalia na imeelezwa na Lt Jenerali Lee kama "shughuli ya kijeshi iliyo bora".
Samho Jewelry yenye tani 11,500 ilikuwa imebeba kemikali kutoka muungano wa Imarati kuelekea Sri Lanka ilipotekwa baina ya maji ya Oman na India.
Mapema wiki hii, Rais Lee Myung-Bak aliliambia jeshi hilo kuchukua "hatua zozote ziwezekanazo" ili kuwaokoa Wakorea kusini wanane, Waindonesia wawili na raia wa Burma 11 waliokuwa kwenye meli hiyo.
Manowari ya Choi Young ilikuwa ikiilinda hiyo meli kwa takriban wiki nzima, na jeshi hilo limesema maharamia hao walionekana kupunguzwa nguvu na muda wote wa kukimbizana.
NI KAMA WANAONGEA ..CHEKI JISTORI lenyewe SASA...yaliyomo yamo??...yamooo
KIJANA: dada mambo vipi mi ni handsome unanionaje..? BINTI: : yaa...unavutia hasa msuko.. balaa....
KIJANA: hata..wewe una mvuto sana.. BINTI: mmmh... siamini kweli ??..
KIJANA: aaah nipatie namba yako kiganjani...siunajua mi sibipu natwangaga kotekote BINTI: ok usijali..
KIJANA: asante kwa namba ntakupigia 29t...!! BINTI: ntashukuru kuskia sauti yako..lakin....lakini.... usimwambi mtu eti....
PAUL LUVINGA ATWAA TUZO YA SHUJAA SAFARI LAGER
Mshindi wa SHUJAA wa SAFARI LAGER bwana paul luvinga
Washiriki watatu waliokuwa wanawania nafasi ya shujaa wa safari lager
Bendi ya MJOMBA ikitumbuiza
Mkurugenzi wa masoko wa TBL DAVID MINJA wakati wa kutangaza mshindi wa SHUJAA wa SAFARI LAGER.
Majaji wa shindano la SHUJAA wamemchagua PAUL LUVINGA kuwa shujaa wa tuzo hiyo ambaye ameshinda baada ya kuanzisha MAKTABA ya bure ya mtaani na kusaidia zaidi ya wanafunzi 200.
PAUL ambaye amejishindia kitita cha shilingi MILIONI SABA amewashinda washiriki wengine wawili ambao ni MERCY SHAYO na LEONARD MTEPA ambao wamepata shilingi MILIONI MOJA kila mmoja.
Naibu waziri wa kazi na ajira DOKTA MAKONGORO MAHANGA amesema wakati akitoa zawadi kwa mshindi huyo kuwa shindano hilo ni moja ya ukuzaji wa ajira hapa nchini.
Mshindi PAUL mbali na kujinyakulia shilingi milioni saba pia kampuni ya bia ya TBL imempa kiasi cha shilingi MILIONI TATU ili aweze kuboresha wazo lake katika kusaidia jamii inayomzunguka.
Barmasai ashinda Dubai Marathon
Mwanariadha wa Kenya, David Barmasai siku ya Ijumaa aliibuka bingwa wa mbio za Dubai Marathon, baada ya kujiandikishia muda wake bora zaidi katika mashindano hayo, saa 2, dakika 7 na sekunde 18.
Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa mwanariadha huyo, mwenye umri wa miaka 22, kupata ushindi.Mwaka jana Barmasai alikuwa ni mshindi wa mbio za marathon za Nairobi.
Akizungumza kwa Kiingereza na mwandishi wa BBC Andy Edwards, Barmasai alielezea kwamba mashindano hayo yalikuwa magumu mno, na hakutazamia kuwa mshindi.
"Kwa kweli ilikuwa vigumu mno kushinda mashindano haya. Sikufikiria ningeliweza kupata ushindi katika mashindano haya. Nimefurahi sana kuwatangulia wanariadha wote. Nilishangazwa sana wakati Eliud Kiptanui aliposhindwa kuendelea baada ya kilomita 30", alielezea Barmasai.
Barmasai amesema sasa anafikiria kujiandaa vyema kwa mashindano ya Tokyo Marathon nchini Japan, na kujaribu kuimarisha muda wake.
Mkenya Evans Cheruiyot alimaliza katika nafasi ya pili, na Eshetu Wendimu wa Ethiopia katika nafasi ya tatu.
Kwa upande wa kina dada, Aselefech Medessa wa Ethiopia alikuwa mshindi, kwa kumaliza katika muda wa saa 2, dakika 22, na sekunde 45, sekunde tatu tu kufikia muda bora zaidi wa mashindano hayo.
Lydia Cheromei wa Kenya alikuwa wa pili, na Isabella Andersson kutoka Sweden akamaliza katika nafasi ya tatu.
Afisa wa Congo akamatwa juu ya ubakaji
Maafisa na Umoja wa Mataifa umesema, serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imemkamata afisa wa jeshi juu ya tuhuma za ubakaji wa raia wengi uliofanyika Januari 1 mashariki mwa nchi hiyo.
Lt Kanali Kibibi Mutware anashutumiwa kwa kuongoza ubakaji wa zaidi ya wanawake 50 huko Fizi, jimbo la Kivu ya kaskazini.Kanali Kibibi ameyatupilia madai hayo na kusema ni uvumi.
Kumekuwa na matukio mengi ya ubakaji wa wanawake wengi mashariki mwa Congo, lakini hili limekuwa tukio kubwa la mara moja kutokea ambalo limehusisha jeshi.
Tahirou Diao, msemaji wa umoja wa mataifa huko Uvira karibu na Fizi, alisema maafisa wa kijeshi wa Congo walimkamata walipotembelea Fizi.
Vyanzo vya kijeshi na mashirika ya kutetea haki za binadamu vimesema matukio hayo ya mwaka mpya yalianza wakati kundi la watu lilipomvamia askari ambaye alimpiga risasi raia- ikidaiwa kuwa walikuwa wakigombania mwanamke.
Baada ya hapo kundi la wanajeshi likaamua kulipiza kisasi kwa watu wa Fizi.
Ofisi ya umoja wa mataifa ilisema wanajeshi waliwapiga kisu watu 26, akiwemo mtoto mwenye umri wa miaka minne, kuharibu zaidi ya nyumba 200 na kubaka idadi kubwa ya wanawake.
Wakaazi wengi wa Fizi na muathirika wa madai hayo ya ubakaji wameshutumu Kanali Kibibi, afisa kamanda wa eneo hilo, kwa kuongoza vurugu hizo.
Lakini katika mahojiano na BBC wiki hii, alikana madai hayo na kusema wanajeshi waliofanya uhalifu huo walikiuka amri yake.
Ghasia za miaka 16 mashariki mwa Congo zimekithiri kwa udhalilishaji wa wanawake na watoto wa kike.
Zaidi ya wanawake 300, wanaume na watoto walibakwa na muungano wa makundi ya waasi katika mji wa Luvungi na vijiji jirani kaskazini mwa Kivu kilomita kadhaa kutoka kituo cha umoja wa mataifa mwezi Agosti.
**************************
JE DULLY SYKES ALIMTENDEA HAKI BOB JUNIOR?
Jina la shalobalo alilopewa msaani chipukizi bob junior na dully sykes kiutani lilikuwa lina maana hiyo mama alikuwa anamkejeli akalipokea bila kujua maana akashindwa kulikataa wakati limeshavumaa.
Maana halisi ya shalobalo kwa kimombo ni sehemu nyeti katika makalio ya nyani...je alijua kama dully alikuwa anamkejeli namna na shalobalo alitaka sana kujua maana yake dully akamwambia ipo siku atamwambia...lakini baadae dully alimwambia maana yake ni mtanashati...kweli?
Djaaka was founded in Beira, Mozambique in 2001 by members from the big traditional music and dance company “Companhia de música e dança traditional da Beira”. Not long after their formation they won the regional young musicians’ festival Music Crossroads in 2002. It was here that they gained substantial regional exposure, winning several prizes, one of which was a visit to Fallun, the folk music festival in Sweden.
Their music reflects various traditions from central Mozambique. Djaaka’s sound can be identified largely by their use of marimba which comes from one area of central Mozambique called “Timbila” is heard on many of their songs. The music is contemporary with a strong traditional touch, both funky and deeply rooted. Djaaka sing in a dialect called Massena, which is not far removed from languages of Zambia, like Bemba and Njanja.
Djaaka is a true live band, skilled musician and good dancers, with outstanding outfits. Their live performance has impressed not only their home audience; it has brought them to festivals in Reunion, Mauritius, South Africa, Zimbabwe, Italy and United Kingdom. They have won the “best Mozambican band” award three times at TOP-Ngoma, held by Radio Mozambique.
MODEL OF A WEEK
Candice swanipoel,This South African model and Victoria Secret Angel was discovered at a flea market when she was 15. I wonder how easy it is for creepy men to “discover” models. Anyway, enjoy the week of pictures
No comments:
Post a Comment