Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Tuesday, January 25, 2011

Muandishi: Othman Michuzi | Tarehe: Monday, January 24, 2011
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akizungumza na vyombo vya habari leo katika mkutano wa ufunguzi wa rasmi wa mchakato wa tuzo za Muziki Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa TBL.kushoto ni Mratibu wa tuzo kutoka BASATA,Angelo Luhala na kulia ni Meneja wa Bia ya Balimi,Edith Bebwa.


KILIMANJARO PREMIUM LAGER na BASATA leo wamezindua rasmi mchakato wa kuwatafuta na kuwa tunza wasanii wa Tanzania waliofanya vizuri kupitia kazi zao za Muziki kwa mwaka wa 2010.

Mwaka jana Tunzo hizi za Muziki nchini Tanzania zilifanyiwa mabadiliko makubwa ambayo yataendelezwa na kuboreshwa zaidi mwaka huu. Mchakato wa kuwapata vinara hao utapitia hatua zifuatazo:

1. ACADEMY:
ACADEMY ya Tunzo za Muziki Tanzania ni mkusanyiko wa wadau wa muziki mia moja (100) kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania ambao huwekwa pamoja katika eneo moja kuwawezesha kuchanganua na hatimae kupata wateule (Nominees) wa vinyang’anyiro (categories) mbali mbali. Utaratibu huu haujabadilika na mwaka huu utafanyika tarehe 12 na 13 Februari 2011.

2. Majaji:
Majaji hua na kazi moja kubwa ya kuhakiki uteuzi wa Nominees uliofanyiwa na Academy ikiwa ni pamoja na kura zitakazopigwa na wananchi. Wao hutumia zaidi vigezo halali vinavyopatikana na mkusanyiko wa rekodi za wasanii zilizotoka kwa mwaka 2010, kazi zao za mwaka 2010, Mafanikio n.k n.k. Jopo hili hujumuisha wadau wa muziki 15.

3. KURA:
Kura za wapenzi wa Muziki nazo hujuishwa katika kuchangua washindi. Mwaka huu kura za wapenzi na mashabiki wa wasanii zitabeba asilimia 50 na majaji asilimia 50. Njia za kupiga kura ni pamoja na:
- SMS.
- Email.
- Magazeti.
- Fliers.

Wawezeshaji:
Kilimanjaro Premium inaendelea kufanya kazi na makampuni matatu katika mchakato na uwezeshaji wa Tunzo za Muziki. Makampuni haya ni pamoja na:
1. Digital Arts – Wasimamizi wakuu wa mchakato wa Tunzo.
2. 1Plus Communications – Wasimamizi wa mawasiliano ya wasanii pamoja na umma.
3. Entertainment Masters – Wasimamizi wa burudani na mahitaji yake.
4. Deloitte Management Consulting – Wasimamizi na wahakiki wa mchakato wa upatikanaji wa wateule pamoja na washindi wa Tunzo za Muziki Tanzania.

Maelezo ya ziada:
Mwaka huu Kilimanjaro kama mdhamini imeamua kuwarudishia wadau na wapenzi wa muziki wa Tanzania usiku wa tunzo. Burudani yote ya usiku huo itatolewa na wasanii wa hapa nyumbani tu. Hapatakuwa na msanii kutoka nje ya nchi kwa vile wasanii wetu wa ndani wanaweza na wanatosha ukizingatia ni Tunzo zao.
 

No comments: