Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Wednesday, April 6, 2011

MISS DAR CITY CENTER YAANZA KUUNGURUMA

Pichani ni wanyange 18 ambao wamejitokeza kushiriki kwenye shindano la kumsaka Miss Dar City Centre 2011.Bongoweekend ilipata fursa ya kuwatembelea na kuwaona mashaallah wamo miongoni mwao ambao huenda wakafika mbali.
Shindano hilo linaratibiwa na Fetty Intertainment chini ya Mkurugenzi Fetty Mgovano ambaye nayeye alikuwa mshiriki wa Miss Tanzania 2005.
Shindano la Miss Dar City Centre litafanyika katika viwanja wa Lamada Ilala Dar es salaam Mei 13 mwaka huu.
Warembo hao wanafundwa na Rehema Uzuia ambaye alikuwa Miss Ruvuma pia alishiriki katika shindano la Miss Tanzania 1999 akisaidiana na Miss Morogoro 2003 Angel Michael.
Mbai ya waalimu hao pia mnenguaji wa bndi ya TOT kwa sasa Bokilo ambaye aliahi kung'ara katika bendi ya Twanga ndiye anafundisha kucheza shoo.
Mlezi wa warembo hao nikaambiwa ni Fatma Issa.

MOZE NA WEAZEL WAMDISS ZUENA HUJUI KUIMBA,ETI AKALIME VIAZI TU!


Mahasimu wa Bebe Cool,Weasel na Moze toka Goodlyfe Crew wameukejeli na kuucheka wimbo wa mke wa Bebe Cool,The Gagamel Crew First Lady Zuena uitwao Owa Boda

Weasel na Moze walianza kumcheka Zuena tangu alipoanza kuimba kwa kusema hawampi 5 wala nini,na kwa kumshauri tu angeenda kulima viazi aachane na kuimba kabisa


MILANGO YA KISASA YAWATOA USHAMBA WABUNGE
milango ya kisasa iliyopo katika jengo la bunge imewatoa ushamba wabunge wengi jamhuri ya muungano baada ya kuganda kwa dakika kadhaa kushindwa kuingia kutokana na teknolojia ya kutumia kadi kuwashinda wabunge hao.


Spurs yatota 4-0, Inter waadhiriwa 5-2

Meneja wa Tottenham Harry Redknapp amesema timu yake iliachwa ikipigana "vita isiyoweza kushinda" baada ya kucheza wakiwa 10 na kusulubiwa kwa kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Real Madrid.
Wachezaji wa Real Madrid wakishangilia bao la Adebayor
Wachezaji wa Real Madrid wakishangilia bao la Adebayor
Mshambuliji wa Spurs Peter Crouch alitolewa nje baada ya dakika ya 14 za mchezo hatua ya robo fainali ya Ubingwa wa vilabu vya Ulaya, mkondo wa kwanza, kutokana na kuoneshwa kadi mbili za njano kwa rafu mbaya alizocheza.
"Ilikuwa kibarua kigumu tukicheza 10," alisema Redknapp. "Mnatakiwa kuwa 11 na pia uwe katika kiwango kizuri kuweza kupata matokeo hapa.
"Bado kazi haijamalizika hadi itakapomalizika, lakini tuna mlima mrefu kuukwea."
Spurs kwa muda wa dakika 75 walicheza wakiwa 10 na tayari walikuwa nyuma kwa bao moja baada ya Emmanuel Adebayor kupachika bao mapema kwa kichwa kabla ya Crouch kutolewa nje.
Adebayor mshambuliaji wa zamani wa Adebayor aliendelea kupachika mabao mara tu baada ya kuanza kipindi cha pili, kabla Angel di Maria na Cristiano Ronaldo kukamilisha kazi kwa kupata ushindi mnono. Real Madridi katika La Liga wanashikilia nafasi ya pili nyuma ya Barcelona.
Tottenham ilikumbwa na taharuki kabla ya mchezo kuanza, baada ya kulazimika kufanya mabadiliko ya kikosi chake cha kwanza baada ya Aaron Lennon kutojisikia vizuri na nafasi yake ikachukuliwa na Jermaine Jenas.
Redknapp ameongeza kusema: "Tulimpoteza Aaron Lennon dakika chache kabla ya mchezo kuanza, hakuwa anajisikia vizuri, alisema tu hana nguvu. Ilitulazimu kufanya mabadiliko wakati tukitoka katika chumba cha kubadilishia nguo.
"Baadae tukafungwa bao moja na isitoshe Crouchy akatolewa nje."
Crouch alioneshwa kadi ya kwanza ya njano katika dakika ya nane baada ya kumchezea rafu mbaya Sergio Ramos na baada ya dakika sita akaoneshwa kadi ya pili ya manjano iliyofuatiwa na nyekundu na akatolewa nje kwa kumchezea rafu Marcelo karibu na kisanduku cha lango la Madrid.
Crouch alikataa kuzungumza baada ya mchezo katika uwanja wa Bernabeu, lakini nahodha wa Tottenham Michael Dawson, amebainisha Crouch aliwaomba radhi wachezaji wenzake.
Kwa Spurs kupoteza mchezo huo ina maana, sasa itawabidi wafanye kazi ngumu kupita kiasi kuweza kusonga mbele watakapokumbana na Real Madrid wiki ijayo katika uwanja wao wa White Hart Lane, lakini Redknapp anafahamu fika kazi waliyonayo ni kubwa kupita kiasi na hawapewi nafasi ya kusonga mbele, na amekataa kukiri kwamba wametolewa.
Na katika mchezo mwengine Schalke ilifanikiwa kufunga mabao matatu katika kipindi cha pili na kuvuruga mipango ya Inter Milan ya kutetea ubingwa wao wa vilabu vya Ulaya na kuwalaza mabingwa hao watetezi mabao 5-2.
Wachezaji wa Schalke wakishangilia bao
Wachezaji wa Schalke wakishangilia bao


Inter Milan ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya kwanza ya mchezo lililofungwa na Dejan Stankovic, kabla Joel Matip kusawazisha.
Diego Milito akaipatia Inter bao la pili kabla ya Goncalves Edu kujibu mapigo na kuisawazishia Schalke na matokeo yakawa 2-2.
Baada ya hapo katika kipindi cha pili Schalke walicharuka na alikuwa Raul Gonzalez aliyefunga bao la tatu na Andrea Ranocchia akajifunga mwenyewe na kuipatia Schalke bao la nne. Inter walipata pigo baada ya mlinzi wao wa kutegemewa Cristian Chivu kuoneshwa kadi nyekundu na kutolewa nje, kabla Edu kumalizia kazi kwa kufunga bao zuri la tano.
Kwa Schalke, iliyo katikati mwa msimamo wa ligi ya Ujerumani maarufu Bundesliga, kufika hatua ya nusu fainali ya Ubingwa wa Ulaya kwa mara ya kwanza, ambapo huenda wakakabiliana na ama Chelsea au Machester United, inaonekana ni jambo wanalotazamia sasa.


Angelina Jolie: Rolling with a Rough Crowd in Tunisia


Angelina Jolie was surrounded by a pushy crowd of onlookers in Tunisia yesterday -- while visiting a refugee camp for those who've fled the violence in Libya.

040511_angelina_jolie_video

Jolie was playing the part of goodwill ambassador for the U.N. High Commissioner for Refugees when some people in the crowd got physical with each other.

Angelina was eventually escorted into a waiting vehicle and driven away from the scene without incident.


Vilabu Kenya vyapewa haki ya kupiga kura

Mfumo mpya wa kupiga kura utatumika kumchagua mkuu wa Shirikisho la Soka nchini Kenya, katika jitahada za kuondoa ufisadi.


Kwa mara ya kwanza vilabu vyote vya soka vilivyosajiliwa nchini Kenya, vinavyofikia 3000, vitakuwa na uwezo wa kupiga kura.
Kabla ya hapo ilikuwa ni idadi ndogo tu ya wajumbe waliokuwa wakipata nafasi ya kupiga kura.
"Mfumo huo wa zamani, ulikuwa ukitumiwa kuchagua viongozi wasiofaa, waliokuwa wakihonga majumbe wawachague," Peter Ogonji, Mkuu wa Bodi Huru ya Uchaguzi nchini Kenya(IEB) ameiambia BBC.
Kampuni inayosimamia soka nchini Kenya, Football Kenya Limited (FKL), inayotambuliwa na Fifa kuwa ndiyo rasmi inayosimamia mchezo wa kandanda nchini humo, inatazamiwa kufanya uchaguzi wa mwenyekiti wake mwezi huu.
Maafisa wa Shirikisho la Soka la Kenya, Kenya Football Federation (KFF), wapinzani wa FKL, pia wanaruhusiwa kugombea.
Kuna matumaini makubwa uchaguzi huo utamaliza miaka kadha ya ubishi na migogoro, iliyosababisha kuporomoka maendeleo ya mchezo wa soka nchini humo.
Uchaguzi huo utasimamiwa na Tume ya uchaguzi ya Kenya, inayosimamia pia uchaguzi wa kisiasa nchini humo, ingawa tarehe maalum haijapangwa.
Wagombea katika nafasi ya mwenyekiti kwa FKL, watatakiwa kuonesha " hati maalum juu ya mwenendo mwema " kutoka Idara ya Upelelezi wa makosa ya jinai ya Kenya, alisema, Ogonji.
"Tunataka kumpatia kila mmoja nafasi ya kugombea nafasi illiyopo, lakini wakati huo huo watakaogombea nafasi hizo ni lazima wawe viongozi wanaoaminika."
Ogonji amekiri kwamba maafisa wa IEB bado wanajadiliana na maafisa wa Fifa juu ya idadi ya kura kwa kila klabu.
Fifa inaaminika inapendelea kila klabu kuwa na kura moja tu, wakati IEB wao wanavutiwa na kura tatu kwa kila klabu.

Rwegasira wa TRAWU kuzikwa leo Kinondoni

               MAZISHI ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli nchini (TRAWU) Bw. Silvester Rwegasira aliyefariki dunia ghafla kwa ugonjwa wa moyo juzi, anatarajiwa
kuzikwa leo kwenye makaburi ya Kinondoni.
          Mwenyekiti wa TRAWU, Bw. Bakari Kiswala alisema jana Dar es Salaam, kuwa taratibu za mazishi ya marehemu Rwegasira zinafanyika nyumbani kwake ghorofa za TAZARA na mwili ya marehemu utaagwa kuanzia saa 5 asubuhi.
          Bw. Kiswala alisema wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) na wale wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) na waombolezaji wengine wataanza kutoa heshima zao za mwisho saa 5 asubuhi mpaka saa 7 mchana.
        Alisema shughuli za kuaga mwili wa marehemu zitafanyika katika stesheni ya Tazara na baadaye safari ya kwenda makaburini itaanza.
        Alisema ibada ya kumuombea marehemu itafanyika Tazara ikiendeshwa na Paroko wa Kanisa Katoliki Chang'ombe, ambayo itakwenda sambamba na kuaga mwili wa marehemu.
        Bw. Kiswala alisema marehemu Rwegasira alikuwa mfanyakazi wa TAZARA kabla ya kuazimwa na TRAWU miaka minane iliyopita kufanya kazi ya Katibu Mkuu wa chama hicho wadhifa aliokuwa nao hadi anafariki.
        Bw. Rwegasira alifariki dunia Hospitali ya Dar Group baada ya kulazwa kwa muda mfupi akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo na mwili wake kuhamishiwa Hospitali ya Aman

No comments: