MTU mmoja mwenye asil ya Kiasia anayehusishwa kumiliki hoteli moja maarufu iliyopo Kigamboni anadaiwa kumjeruhi kwa kumchoma moto mkazi wa Mjimwema, Lila Hussein (25), baada kuingia hotelini hapo bila kulipa kiingilio.
Akizungumza na Dar jana, ndugu wa majeruhi huyo, Abdullah Saiwaad,alisema tukio hilo lilitokea Jumamosi majira kati ya saa 5:00 na 6:00 usiku.
Alisema kabla ya kuchomwa moto, Lila ambaye amelazwa wodi namba 7 katika Hospitali ya Temeke akiwa hajitambui, alivuliwa nguo kisha kumwagiwa mafuta ya petroli na kwamba amejeruhiwa vibaya kuanzia sehemu za magotini hadi shingoni.
Alisema chanzo cha tukio hilo ni Lila kuingia kwenye muziki hotelini hapo bila kulipa kiingilio.
“Hali ni tete, Lila yupo hospitali ya Temeke akipigania maisha yake baada ya kuchomwa moto na mhindi ambaye ni mmiliki wa hoteli ya South Beach, ameungua vibaya tunamwomba Mungu anusuru maisha yake,” alisema Saiwaad.
Alisema baadaye aliokolewa na wafanyakazi wawili baada ya kuamua kupeleka taarifa kijijini Mjimwema.
Kutokana na tukio hilo wanakijiji wametishia kuchoma moto hoteli hiyo na kwamba hali hiyo imesababisha mkuu wa kituo cha Kigamboni kupeleka askari wa doria kusimamia usalama hotelini hapo.
Hapa ndipo tunapokumbuka sera za mchungaji mtikira....
JUSTIN BIEBER AFANYA MAZOEZI NA FC BARCELONA!
Dogo Star wa Pop,Justin Bieber toka Canada alichukua muda wake wa kupiga Tour yake iitwayo My World Tour nchini Spain kwa kufanya mazoezi ya soka na kikosi cha FC Barcelona toka Catalan pande za Joan Gamper Sports Complex,Barcelona
Justin Bieber anayetumia mguu wa kushoto,alialikwa kufanya mazoezi baada ya kuoneka amevaa jezi ya FC Barcelona alipokua anacheza soka na crew yake na baadaye kufunguka kuwa yeye ni mpenzi mkubwa wa FC Barcelona,baadaye kuendelea na tour yake jijini Madrid!
Justin Bieber anayetumia mguu wa kushoto,alialikwa kufanya mazoezi baada ya kuoneka amevaa jezi ya FC Barcelona alipokua anacheza soka na crew yake na baadaye kufunguka kuwa yeye ni mpenzi mkubwa wa FC Barcelona,baadaye kuendelea na tour yake jijini Madrid! JUSTIN BIEBER AKIWA NA BOJAN KRKIC


No comments:
Post a Comment