Wananchi wakiwa katika harakati za kumuokoa dereva wa gari hili 
ambalo limeagukiwa na mti katika eneo la Skuli ya Jangombe wakati akipita
 katika barabara hiyo. Wakati mvua ikinyesha na kusababisha ajali hiyo.
 Kutokana na juhudi za wananchi na Kikosi cha Askari wa Uokozi cha Faya 
walifanikiwa kumuokoa dereva huyu aliyejulikana kwa jina la Ali 
Abdulrahaman Juma (Chatne)alikuwa akiendesha gari yenye usajili wa namba
  Z 249 AK.   
Wananchi wakimtoa dereva katika gari hiyo kwa kumkimbiza hospitali ya 
mnazi mmoja kwa matibabu zaidi, amepata majeraha kwa kuangukiwa na mti 
huo. 
 Hii ni sehemu ya dereva ilivyoharibika katika ajali hiyo, katika gari 
hiyo alikuwa dereva peke yake na kupata majaraha na kukimbizwa hospitali
 ya Mnazi Mmoja kwa matibabu zaidi. 
 
 
No comments:
Post a Comment