Mkurugenzi
Mtendaji wa Hoteli ya Doubletree by Hilton Zanzibar, Bw. Samuel(kulia)
Bond na Mkewe Jenny Bond wakibadilishana mawazo na mmoja wa majaji wa
tuzo za ZIFF 2014 Mykel Parish (aliyeipa mgongo kamera) kabla ya kuanza
kwa tuzo za ZIFF 2014.
Mkurugenzi
Mkuu wa ZIFF, Profesa Martin Mhando akiwakaribisha wageni waalikwa
waliohudhuria usiku maalum wa tuzo za tamasha la 17 la ZIFF 2014
zilizofanyika mwishoni mwa juma.
Alisema
tamasha hilo halitabadili wajibu wake wa tangu awali wa,mkuchochea
mabadiliko miongoni mwa jamii na serikali hali ambayo inajenga jamii
yenye kuheshimu maendeleo na wajibu wa kila mmojawao.
Alisema
pamoja na kuwa na safari ndefu bado ZIFF ndio jukwaa lenye uhakika kwa
watengeneza sinemakatika bara la Afrika na kadhalika.
Katika utoaji tuzo,ZIFF ilialika zaidi ya watengeneza filamu 30 kutoka nchi mbalimbali.
ZIFF 2014 – AWARDS
SIGNIS AWARDS
SPECIAL MENTION
Shadow Tree
By BIja Viswa
(Tanzania)
EAST AFRICAN TALENT AWARD (1000 dollars)
Sticking Ribbons
by Bill Jones
(Kenya)
SIGNIS PRIZE
Espinho Da Rosa/ The Thorn Of The Rose
by Filipe Henriques
(Guine Bissao)
SEMBENE OUSMANE AWARDS
Umunthu,
by Mwizalero Nyirenda
(Malawi)
Body Games,
by Richard Pakleppa& Matthias Rohrig Assuncao
(Namibia / Brasil / South Africa)
SPECIAL MENTION
Welcome to Loliondo
by Morten West
(Denmark)
ZUKU BONGO MOVIES AWARDS
ZUKU PEOPLE CHOICE
Shikamoo Mzee
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wananchi Group ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha
hilo, Bw. Richard Bell akizungumza na wageni waalikwa wakati utoaji tuzo
za ZIFF 2014 lililomalizika mwishoni mwa juma visiwani Zanzibar. Aidha
mwenyekiti huyo alisema kwamba Zuku itaendelea kuhakikisha inasaidia
kuinua kiwango cha uigizaji na utengenezaji sinema za Kiswahili kwa
kutambua kwamba filamu hizo ni sehemu ya uzalishaji wa fedha katika
taifa kupitia utamaduni na kutoa wito kwa wasanii wa Bongo Movie
kupeleka kazi zao kwa ajili ya kuonyeshwa kwenye chaneli za ving'amuzi
vya ZUKU na kujitangaza kimataifa kupitia ving'amuzi hivyo.
BEST ACTOR
Jackson Kabirigi
for Kisate and Nguvu ya Imani
BEST ACTRESS
Esha Buheti
for Mimi na Mungu wangu
BEST DIRECTOR
Issa Musa Cloud
for Shahada
BEST FEATURE FILM
Shahada
Issa Musa
ZIFF AWARDS
LIFETIME ACHIEVEMENT AWARD
Emerson Skeens
Founder of ZIFF
Awarded Posthumously
BEST DOCUMENTARY
Sobukwe: A Great Soul
Mickey Madoda Dube
(South Africa)
BEST ANIMATION
Khumba
Anthony Silverston
(SouthAfrica)
BEST SHORT FILM
Shadowtree
Mti Wakivuli / Biju Viswanath
(India / Tanzania)
BEST EAST AFRICAN TALENT
The King’s Virgin
Daniel Moss
(Tanzania/UK)
Mmoja
wa majaji wa tuzo za Signs kwenye tamasha la ZIFF 2014, Adinda Pamela
akitangaza washindi wa tuzo hizo. Katikati ni Mratibu wa Majaji wa tuzo
za ZIFF 2014, Fabrizio Colombo na kulia ni mmoja wa "ushers" akiwa
ameshikilia tuzo hiyo.
CHAIRMAN’s AWARD
Sodiq
Adeyemi Michael
(UK)
SPECIAL JURY AWARD
Julio Mesquith
Main Actor
The Thorn of the Rose
BEST FEATURE FILM (SILVER DHOW)
The Thorn of the Rose - Espinho da Rosa
by Filipe Henriques (Guinea Bissau)
BEST FEATURE FILM (GOLDEN DHOW)
Half of a Yellow Sun
Biyi Bandele (USA)
ADY
de Batista akiongea kwa furaha kwenye usiku maalum wa tuzo za Signis
katika kusheherekea tamasha la 17 la ZIFF lililomalizika mwishoni mwa
wiki visiwani Zanzibar.
ADY de Batista akishuka jukwaani baada ya kupokea tuzo na Meneja wake.
Channel Coordinator wa ZUKU Swahili, Bilha Olimba akitangaza jina la mshindi wa tuzo za ZUKU PEOPLE's CHOICE. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wananchi Group ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo kupitia brand ya ZUKU, Bw. Richard Bell
Shamsa Ford akizungumza kwa niaba ya JB kabla ya kupokea tuzo hiyo.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wananchi Group ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha
hilo kupitia brand ya ZUKU, Bw. Richard Bell akikabidhi tuzo ya ZUKU
PEOPLE's CHOICE kupitia filamu ya SHIKAMOO MZEE ya mwigizaji Jacob
Steven almaarufu kama JB iliyopokelewa na msanii mwenzake Shamsa Ford.
Shamsa Ford akishukaa jukwaa kwa furaha isiyona kifani.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wananchi Group ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha
hilo kupitia brand ya ZUKU, Bw. Richard Bell akimkabidhi tuzo mwigizaji
bora Jackson Laurent Kabirigi kupitia filamu ya "Kisate na Nguvu ya Imani" (wa pili kushoto) aliyeambatana na ndugu yake Feysal Arikardy (kushoto).
No comments:
Post a Comment