Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Monday, May 9, 2011

Dr.MWAKYEMBE ATAKIWA KUJIUZULU-CHADEMA

     http://www.newhabari.com/wp-content/uploads/2011/03/Dr-Harrison-Mwakyembe-300x244.jpg
    MZIMU wa sakata la kampuni tata ya Richomond, umezidi kuwaandama wanasiasa nchini, sasa
ikiwa ni zamu ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye ametakwa kujiuzulu kutoka serikalini ili kutunza uadilifu wake baada ya serikali kupuuzia maagizo ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza sakata la kashfa hiyo.
     Ameambiwa kuwa iwapo ataendelea kung'ang'ania kubaki katika serikali ya namna hiyo, atakuwa anafanya hivyo kwa sababu ama ya 'uroho na ulafi' wa madaraka au kutokuwa na uwezo wa kusimamia misimamo ya uongozi adilifu, tofauti na Watanzania wengi wanavyomwelewa.

          Hayo yalisemwa jana na mmoja wa makada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Fred Mpendazoe, ambaye katika bunge lililopita kabla hajajiuzulu ubunge wake wa Kishapu alikuwa ni mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

     Akizungumza katika mikutano ya Operesheni Sangara ya chama hicho katika Nyanda za Juu Kusin, mkoani Mbeya, amesema kuwa Dkt. Mwakyembe ndiye alikuwa mwenyekiti wa kamati hiyo teule ya bunge, ambayo katika moja ya mapendekezo kwenye ripoti yake, ilitaja watendaji wa serikali waliohusika katika kashfa hiyo, mmoja wao akiwa ni Bw. Bashir Mrindoko, ambaye wakati wa sakata la Richmond, alikuwa ni Kamishna wa Nishati, katika Wizara ya Nishati na Madini

         Bw. Mrindoko ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Maji, alikuwa kwenye orodha ya kamati ya Dkt. Mwakyembe ikipendekezwa achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu mpya wa Wizara kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC.

         Bw. Mrindoko ndiye aliyeiandikia barua kampuni hiyo kusitisha mkataba wake na serikali mwezi mmoja tu kabla ya mchakato wa zabuni ya umeme wa dharura haujaanza.



TIMBWILI LA TRAFFIKI NUSURA KUAWA NA DEREVA DALADALA

 Baadhi ya Abiria na wananchi ambao walifika eneo hilo la tukio kushuhudia kimbembe hicho maeneo ya  mwenge ambapo Dereva aligoma kuwapeleka abiria Mbezi Kimara
Traffic akiwa amefika eneo la tukio baada ya kupewa malalamiko na moja ya abilia katika eneo hilo
Break down likiwa tayali eneo la tukio baada ya dereva wa gari hilo kugoma kuwasafikisha abiria na kutaka kuchukua Gari hilo kulipeleka eneo husika

Traffic aliye nusulika kifo akishirikiana na mwenzake kumkamata dereva wa gari hilo
 

1 comment:

Mlanzi George said...

Safi sana uniq kwa kazi nzuri