Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Monday, May 23, 2011

HUKUMU YA EPA WATANZANIA WABAKI MDOMO WAZI.....!!!

....FARIJALA HUSSEIN NA RAJAB MARANDA....
    Hukumu ya kesi ya wizi wa Sh bilioni 1.8 katika Akaunti ya madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetolewa leo kwa
   Farijala Hussein na ndugu yake Rajabu   Maranda,wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela ambapo pia wametakiwa kurudisha fedha hizo kwa Serikali
     Jopo la majaji watatu likiongozwa na Mh Saul Kinemela,limewatia hatiani kwa mashitaka nane yanayowakabili shitaka la kwanza lilifutwa kwa kuwa upande wa mashitaka ulishindwa kuthibitisha hilo,Kwa kosa la pili mshitakiwa wa kwanza pekee atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela,kosa la tatu na la nne 
    washitakiwa wote watatumikia adhabu ya miaka mitano,kosa la tano mshitakiwa wa pili pekee atatumikia adhabu ya miaka miwili jela huku Kosa la sita washitakiwa wote kwa pamoja watatumikia adhabu ya miaka miwili jela na kosa la saba na la nane wote watatumikia adhabu ya miaka mitatu jela," alifunguka Hakimu Mgeta




MCHUNGAJI ALIETABIRI KIAMA....AINGIA MITINI!
MCHUNGAJI HAROLD CAMPING
    Kiama kilitakiwa kiwe Jumamosi saa 12 jioni lakini hakikutokea kama kilivyotabiriwa na mchungaji Harold Camping wa nchini Marekani ambaye alitumia pesa nyingi sana kuwaonya watu kwa miezi kadhaa kuwa kiama kingetokea jana May 21,2011
    Wafuasi na waumini wa Mchungaji Harold Camping wamebaki hawajui la kufanya baada ya kuhubiriwa kwa miezi mingi kuwa kiama kingetokea jana jumamosi saa 12 jioni,huku familia moja ilisafiri kilomita 4830 toka   Maryland hadi California mbele ya ofisi ya radio ya mchungaji Camping na kusubiri kupaishwa mbinguni kwenda kuonana na Yesu huku
    Mzee mmoja wa miak 60,Robert Fitzpatrick kwa kuamini kuwa mwisho wa dunia umefika na kwa kuamini mafundisho ya mchungaji Camping,alitumia dola $140,000 toka kwenye akiba yake ili kuchapisha mabango na vipeperushi vya kuwaonya watu kuwa mwisho wa dunia ni May 21 Mchungaji Camping mwenyewe hajaonekana tena na amekaa kimya na hadi sasa hajasema chochote kwanini kiama hakikutokea kama alivyotabiri na kuwahabarisha watu kwa miezi kadhaa kabla,hata hivyo bado waumini  
   wengine wa mchungaji Camping wanaendelea kumuamini mchungaji huyo wakisema kuwa kuchelewa kutokea kwa kiama ni mtihani mwingine toka kwa Mungu juu ya imani zao

No comments: