KADA mwandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Fred Mpendazoe, ameendelea kuanika siri za vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), zinazowahusisha na mipango ya kuwahi kukigeuka chama chao na kuanzisha Chama cha Jamii (CCJ).
Mpendazoe aliyekuwa Mbunge jimbo la Kishapu kwa tiketi ya CCM, alijitoa mapema mwaka jana na kujiunga na CCJ kabla ya kuhamia CHADEMA.
Baada ya kumtaja Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kuwa mmoja wa waanzilishi wa CCJ, jana aliwataja Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrisson Mwakyembe, akisitiza kuwa ndio waliokuwa waasisi wakuu wa CCJ.
Mpendazoe aliwataja mawaziri hao wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Njombe, waliofurika katika viwanja vya National Housing, katika mfululizo wa maandamano na mikutano ya hadhara ya chama hicho inayoendelea kwenye mikoa ya nyanda za juu kusini.
Mbali na hao, aliwataja makada wengine wa CCM walioshiriki kuanzisha CCJ kuwa ni Victor Mwambalaswa, Daniel Ole Porokwa na Paul Makonda.
Alisema uwepo wa Sitta na Mwakyembe katika baraza la mawaziri unaifanya serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuwa ya bandia, kwani viongozi hao wanamdharau na walishawahi kuasi CCM kwa lengo la kujiunga na CCJ.
“Sitta na Mwakyembve ndio waanzilishi wakuu wa CCJ, nilishirikiana nao kuanzisha kile chama, lengo lilikuwa tuungane na CHADEMA ili kuongeza nguvu ya kupambana na ufisadi na uongozi mbovu wa CCM, lakini wenzangu walikuja kunisaliti dakika za mwisho.
“Sitta aliahidiwa kupewa uspika na Mwakyembe uwaziri, lakini baadaye wote wamepewa uwaziri baada ya Sitta kunyimwa uspika waliokuwa wamemuahidi kumpa tena.
Wenzangu hawakuwa na dhamira ya dhati, waliongozwa na uchu wao wa kupenda zaidi madaraka. Wako na Kikwete kwa sababu tu ya vyeo vyao. Wasijifanye kupambana na ufisadi...wala wasidanganye CCM imejivua gamba. Wote ni mafisadi...hakuna wa kuiamini CCM,” alisema Mpendazoe na kushangiliwa.
Alisisitiza kuwa wana-CCM hao wamebaki ndani ya chama hicho na serikali yake si kwa sababu ya utiifu na uzalendo wao kwa chama chao bali wamesukumwa na vyeo vya uwaziri na ukuu wa wilaya walivyopewa na Kikwete mwenyewe bila kujua.
Alisema ameamua kuliambia taifa ukweli wote kuhusu wana CCM hao ili umma wa Watanzania uepuke kudanganywa na propaganda zao za kujifanya wanapambana na ufisadi.
Wakati akimtaja Nape siku mbili zilizopita mbele ya wakazi wa Mbamba Bay mkoani Ruvuma, Mpendazoe alisema kijana huyo alishiriki kuandika katiba ya chama hicho.
Alisema ndiye aliyepewa jukumu la kutafuta nakala za katiba za vyama vingine tawala nchini Afrika, ili kupata katiba nzuri ya kuigwa katika kuandika katiba ya CCJ.
Aliwaambia wakazi hao kuwa Nape alilitekeleza vizuri jukumu hilo kwani alifanikiwa kuipata katiba ya chama cha ANC kinachotawala Afrika Kusini, ambayo alisema ndiyo iliyotumika kwa kiasi kikubwa katika kuandika katiba ya CCJ.
RIHANNA AOMBA RADHI KISA CHRIS BROWN!
RIHANNA
Rihanna ameomba radhi kwa kuwakwaza fans wake kwenye mtandao wa Twitter,baada ya kumsemea mbovu kwa kumfata ex-boyfriend,Chris Brown kwenye mtandao wa Twitter
RiRi alimfuata Chris Brown kwenye Twitter,tangu alipopewa kibano kwenye party ya Grammy Awards 2009
CHRIS BROWN
Fans wa Rihanna walimsemea mbovu kwa kumfuata Breezy na kumuacha Riri akijitetea na sasa amaeamua kuomba radhi tena na kuahidi kutorudia tena
CHIDI BENZ NA CHEGE WAGONGANISHWA NA DEMU WA KIKENYA
Demu mmoja artist wa kenya ajulikanae kama Lady B amekuwa akiwachanganya kimapenzi Chid benz na Chege ambapo kwa awamu tofauti demu huyo ameonekana akiwa kimahaba na wasanii hawa wa kitanzania.
Wachunguzi wa mambo wanadai chidi benz amekuwa na safari za mara kwa mara nchini kenya kumfuata kidosho huyo
KWA TAARIFA YAKO UNYUMBA WA MFIKISHA MAHAKAMANI
Mwanamke kakasirika
Mwanamama mmoja huko Dubai anamshitaki mume wake wa zamani, kwa kushindwa kumtaarifu mapema kuwa hawezi kutoa unyumba, kabla hawajafunga ndoa.
Gazeti la Hundustan Times limesema mwanamama huyo amewasilisha kesi ya madai ya dola milioni kumi na moja.
Amesema amepata athari ya kiakili kutokana na tukio hilo. Mwanamama huyo amedai kuwa, alipoolewa, mume wake alimlazimisha kucha kazi aliyokuwa akifanya, na kuuza vito vyake vyote vya thamani. Licha ya hivyo Mwanaume huyo hakumpa haki yake ya ndoa.
Taarifa zinasema baada ya miezi minne, mwanamama huyo aligundua kuwa mume wake huyo jongoo halipandi mtungi na kulazimika kudai talaka. "Kwa kuzingatia misingi ya Kiarabu, na nafasi ya mwanamke katika jamii, nilibaki kimya na kujaribu kumuomba Mungu labda mambo yatakaa sawa" amesema mwanamama huyo akizungumza na gazeti la Hundustan.
CASIDY AUA TENA MTU
Msaii Barry Adrian Reese ajulikanae kama Cassidy a.k.a The ploblem amekamatwa huko Hackensack,New Jersey kwa kile kilichosemekana kuwa Cassidy anahusishwa na mauaji na matukio mengine mawili ya uhalifu yaliyotokea maeneo ya Philadelphia.
Polisi wa Philadelphia walimfuatilia Cassidy tangu alipotoka anapoishi yaani nyubani kwake mchana na kulisimamisha gari lake kitendo kilichomshangaza sasa Cassidy na anatarajiwa kupelekwa mjini Philadelphia kujibu mashitaka hayo
Cassid The ploblem ambae ni husler waukweli si mara yake ya kwanza kukumbwa na skendo za mauaji na uuzaji wa dawa za kulevya.
ALEXIA WILLIAMS AWA MISS DAR CITY CENER
VODACOM Miss Dar City Centre 2011/12 Alexia William (katikati), akipunga mkono muda mfupi baada ya kuvishwa taji hilo, (kushoto), ni mshindi namba mbili Salah Israel na mshindi namba tatu, Jennifer Kakolaki
No comments:
Post a Comment