Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Friday, June 3, 2011

MBOWE MASHAKAN TENA MAHAKAMANI...??

  
     MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha imeagiza tena Jeshi la Polisi kumkamata Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Bw. Freeman Mbowe baada ya kushindwa kujisalimisha mahakamani katika kesi inayomkabili.
    Akitoa hukumu dhidi ya washtakiwa wengine waliojisalimisha mahakamani baada ya kushindwa kuhudhuria katika mahakamani hapo Mei 27 mwaka huu, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Bw. Charles Magesa alisema kitendo cha mshitakiwa wa kwanza katika shauri hilo kushindwa kujisalimisha labda anataka kukamatwa na polisi.
    Mahakama hiyo awali, iliamuru Mwenyekiti huyo pamoja na viongozi wengine akiwemo Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dkt. Willibrod Slaa, wabunge wawili wa chama hicho, Bw. Phillemon Ndesamburo (Moshi Mjini) na Bw. Godbless Lema (Arusha Mjini) wakamatwe na kufikishwa mahakamani hapo baada ya kushindwa kuhudhuria katika kesi inayowakabili ya kufanya kusanyiko lisilo halali Januari 5 mwaka huu.
    Washtakiwa wengine ambao mahakama ilitoa hati ya kukamatwa ambao hata hivyo walijisalimisha mahakamani siku mbili baadaye ni pamoja na mchumba wa Dkt. Slaa, Bi. Josephine
Mushumbusi, Bw. Richard Mtui, Bi. Aquiline Chuwa na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Bw. Samson Mwigamba.
    Pamoja na washtakiwa na wadhamini wao kutofika mahakamani, hata Mawakili wao, Bw. Method Kimomogolo na Bw. Albert Msando pia hawakuwepo mahakamani wakati hati hiyo inatolewa, lakini
washtakiwa Bw. Joseph Selasini (Mbunge wa Rombo) na Bw. Dadi Igogo pia hawakuwepo mahakamani siku hiyo, na mahakama haikutoa hati ya kuwakamatwe kwa sababu wadhamini wao walikuwapo.
    Washtakiwa waliohudhuria mahakamani hapo siku hiyo ni pamoja na Bw. Nai Steven, Bw. Mathias Valerian, Bw. John Materu, Bw. Daniel Titus, Bw. Juma Samuel, Bw. Walter Mushi, Bw. Peter Marua na Bw. Erick Makona.
     Hakumu Magesa alisema mshitakiwa wa kwanza (Mbowe) baada ya kutolewa hati ya kumkamata au kujisalimisha mahakamani hakufanya hivyo hadi jana wala mdhamini wake, hivyo Ofisa Inchaji wa Polisi anatakiwa kumkamata kwani ni wajibu wake kutekeleza amri halali ya mahakama ni si vinginevyo.
    “Wote walipewa masharti ya kufika mahakamani kama ulivyo utaratibu na iwapo wanapatikana na udhuru wa kibinadamu basi ni wajibu wa wadhamini wao kuhakikisha wanafika mahakamani kueleza kilichowasibu. Kimsingi si sahihi kutofika mahakamani bila taarifa, hivyo Ofisa Inchaji amkamate na kufikishwa mahakamani,” alisema.
     Bw. Ndesamburu alinusurika kwenye hukumu hiyo baada ya Mdhamini wake, Bw. Reuben Ngowi kuibuka mahakamani hapo na kutoa udhuru uliomkuta mshtakiwa huyo pamoja na yeye mwenyewe, ambapo Hakimu Magesa alikubaliana naye na kufuta amri hiyo, hivyo kuachiwa huru.
Katika hukumu dhidi ya washitakiwa wengine waliojisalimisha pamoja na wadhamini wao, walipewa onyo kali na kutakiwa kutorudia kosa hilo kwani kufanya hivyo ni kukiuka maagizo halali ya mahakama.
Alisema amepitia hoja za wakili wa upande wa utetezi, na kwa kuzingatia sababu zilizotolewa mahakamani, aliamua kufuta amri hiyo na kuahirisha kesi hiyo hadi Juni 24, mwaka huu.




SEPP BLATTER....ASHINDA URAIS WA FIFA...!

Joseph Sepp Blatter toka Switzerland alirudia kiti chake cha Urais wa FIFA kwa kipindi kingine cha Miaka minne baada ya kushinda kwa kura 186 kati ya 203 zilizopigwa kwenye mkutano wa 61 wa FIFA huko Zurich-Uswisi
Kabla ya kura za Urais kupigwa,Vyama vya Soka vya England na Scotland vilieta shinikizo ili Uchaguzi wa Urais wa FIFA usimamishwe ili kuchunguzwa kwa tuhuma za rushwa, lakini hoja yao ilikosa nguvu na kuungwa mkono na Wanachama 17 tu wa FIFA kati ya Wanachama 206 waliopiga kura kuamua kuhusu hoja yao
Sepp Blatter alianza kuiongoza FIFA kama rais tarehe 8 June 1998



Uganda yatishia kuondoa majeshi yake Somalia

Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Uganda Yoweri Museveni
   Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesema kuwa serikali ya mpito ya Somalia inahitaji mwaka mmoja zaidi ili kukabiliana vyema na wapiganaji wa Kiislamu.
    Alionya kuwa kama hilo halitazingatiwa, basi Uganda itaondoa vikosi vyake vinavyosaidia serikali ya mpito dhidi ya wapiganaji wa al-Shabab, alisema.
    Muda wa sasa wa serikali hio inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa unamalizika tarehe 20 mwezi Agosti mwaka huu na Umoja wa Mataifa unataka uchaguzi ufanyike haraka.
    Bwana Museveni amesema uchaguzi ukifanyika mwaka huu utatoa fursa kwa makundi ya wapiganaji kujipanga upya.
Uganda ina wanajeshi 5,000 katika kikosi cha muungano wa Afrika wanaolinda amani, nchini Somalia.
    Burundi nayo inachangia idadi ilobakia.
" Inaonekana kwetu itakuwa bora kwa pande zote kama serikali ya mpito itaongezewa muda usiozidi mwaka mmoja," Bwana Museveni aliwaambia wajumbe wa mkutano wa kimataifa kuhusu Somalia mjini Kampala, Uganda.
Rais wa Somalia
Rais wa Somalia
      Uchaguzi ukifanywa mapema,alionya, " Itakuwa ni nafasi kwa watu wenye misimamo mikali kujipanga upya na kuleta matatizo na kutia dosari mafanikio yote yaliyopatikana kufikia sasa".
    Aliongeza: "kama utawala wa sasa utaondoka, au kama utadhoofishwa, basi itakuwa hatuna sababu ya kuendelea kukaa katika mazingira hayo - tutaondoka Somalia."
    Rais wa Somalia Sharif Sheikh Ahmad aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa hali kwa sasa nchini humo si shwari kwa kufanya uchaguzi. Hata yeye alitaka muda wa serikali ya mpito uongezwe.

No comments: