Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Friday, July 8, 2011

VIONGOZI CHANZO CHA VURUGU JIJINI MWANZA

Vurugu za wamachinga na mgambo zilizotokea juzi jijini hapa, zimedaiwa kusababishwa na mvutano baina ya ofisi ya Meya na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza.Zima moto shughulini.
Madai hayo yalitolewa jana na Meya wa Jiji, Josephat Manyerere (Chadema), wakati akizungumza wa waandishi wa habari ambapo alidai kwamba ofisi yake haikupewa taarifa ya operesheni ya kuondoa wamachinga katika maeneo yasiyoruhusiwa kufanya biashara katika mtaa wa Makoroboi.

Alipofuatilia, alibaini kuwa hata ofisi ya Mbunge wa Nyamagana, haikuwa na taarifa ya operesheni hiyo, ambayo imesababisha watu saba kujeruhiwa na kwamba habari zilizoenezwa kuwa Chadema walihusika na vurugu hizo kwa sababu halmashauri
inayoongozwa na chama hicho ni ya uchochezi.


Amesema kwa kuwa operesheni hiyo ni batili, amewataka wamachinga waendelee kufanya biashara katika maeneo ya Makoroboi, hadi suala lao litakapopelekwa kwenye Baraza la Madiwani, ili kutafutiwa utaratibu na maeneo yasiyo na bughudha. Mvutano huo wa kiuhusiano, umesababisha ofisi ya Mkurugenzi kutotoa ushirikiano kwa ofisi ya Meya na kutolea mfano wa uuzwaji wa viwanja katika eneo la Kiseke bila ofisi yake kujulishwa.

Aidha, ametoa wito kwa wamachinga kujitahidi kupanga bidhaa zao vizuri, ili watu wapate njia ya kupita na pia wasitumie vipaza sauti kutangaza bidhaa zao na kuhakikisha maeneo ya biashara yanabaki safi na wafanye biashara hizo kuanzia saa 10 jioni.

Amewaomba wenye misikiti na shule katika mtaa wa Makoroboi waendelee kuwavumilia hadi ufumbuzi wa kudumu utakapopatikana kutokana na kwamba kulegalega kwa uhusiano wa kikazi kumesababisha vurugu zilizotokea juzi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Simon Sirro, alisema watu 49 kati ya 131 waliokamatwa juzi kwenye vurugu watafikishwa mahakamani leo baada ya uchunguzi kukamilika.

Jamani vita haina macho, binti huyu alishambuliwa akiwa anakwenda Sokoni alikotumwa na Mama yake.
Sirro amesema hali jijini hapa ni shwari na majeruhi watatu wameonekana kuwa na majeraha ya risasi za Shot gun na uchunguzi unafanywa kubaini walipigwa na nani kama ni mgambo au kwenye maduka waliyovamia.

Magari yaliyochomwa moto.Wenje amesema kuwa yuko tayari kufikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa 

Kivita (ICC) The Hague, Uholanzi katika suala la kutetea haki za wamachinga kufanya biashara katikati ya Jiji.

Hata hivyo, Mbunge huyo amemwomba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuunda Tume ya kuchunguza chanzo cha mgambo kupiga watu risasi kutokana na majeruhi we
ngi wa vurugu hizo kuwa na majeraha ya risasi za bunduki ambazo hazimilikiwi na Polisi.

Magari mawili ya mfanyabiashara maarufu mkoani hapa Mukeshi vunja bei yamechomwa moto na kuteketea, vibanda kadhaa vimevunjwa, Baadhi ya bidhaa zilizopangwa nje zimeibiwa nayo matairi yamechomwa katikati ya njia panda kuingia mtaa wa Makoroboi kuelekea Soko kuu na kiunganishi cha barabara ya Lumumba Mwanza huku baadhi ya wamachinga hao wakirusha maboksi yaliyoshika moto kwenye majengo yaliyo karibu na eneo hilo kwa nia ya kuyachoma moto.

Vibaka wamepora bidhaa na mali zilizokuwa nje ya Nono Super market nakisha kuchoma friji ilokuwa na vinywaji ambavyo walivinywa kabla ya kuiteketeza.



JAMAA AOA WAKE WANNE SIKU MOJA
Ni Jamaa mmoja toka Afrika Kusini aitwae Milton Mbele mwenye miaka 45 ameweka rekodi ya aina yake baada ya kuoa wanawake wanne kwa mpigo
Milton ni meneja wa manispaa ya Indaka Zulu-Natal alifunga ndoa ya kikristo na wake zake hao na baadaye ikafuata sherehe ya kimila.


No comments: