JESHI
la polisi mkoa wa Iringa kupitia dhana ya polisi jamii na ulinzi
shirikishi limefanikiwa kukamata mali za wizi zilizokuwa
zikisafirishwa kwenda nchi ya DRC Kongo zikiwa na thamani ya Tsh
milioni 100 pamoja na lori lenye thamani ya Tsh milioni 100 ambalo
liliteketezwa kwa moto kabla ya dereva na utingo wa lori hilo
kulichoma moto kama njia ya kupoteza ushahidi.
Imedaiwa
kuwa watu zaidi ya 6 wanashikiliwa na jeshi hilo la polisi
akiwemo dereva na utingo wake ambao wanadaiwa kuhusika na tukio la
wizi huo.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi alisema kuwa tukio hilo
lilitokea juzi May 31 ambapo askari wa doria wilaya ya Mufindi
wakiwa katika shughuli hiyo ya doria walifanikiwa kuliona lori
hilo likiwa limeegeshwa kando ya barabara ya Iringa –Mbeya eneo la
Kinegembasi wilaya ya Mufindi huku likiwa limeteketea kwa moto katika
kibini yake.
Alisema
kuwa watu hao waliteketeza lori lenye namba za usajili T527 DPQ
likiwa na tela lenye namba T 974 EFE aina ya scania mali ya kampuni
ya Dandu ambalo walilikuta likiungua huku silizi zake zikiwa
zimefunguliwa na baada ya uchungu wa awali walibaini kuwa lori hilo
lilikuwa limebeba mitumba na viatu na baada ya msako ndipo
walipofanikiwa kukuta mitumba hiyo ikiwa imefichwa katika nyumba
moja kuukuu mali ya mama Gray Mpinga mwenyeji wa Maguhani Mufindi.
Alisema
kuwa mali hizo ambazo ni mabelo ya mitumba na viatu yalitoka
Bandarini kwenda DRC chini ya dereva wa lori hilo ni Enedia Christian
(26) mkazi wa Mbeya na utingo wake Deus Gendo (20) mkazi wa Mbeya .
Kamanda
Mungi alisema kuwa utingo na dereva wa lori hilo baada ya kufika
kijiji hicho cha Maguhani walivunja kontena na kushusha mali zote na
kuzihifadhi katika nyumba hiyo kabla ya kutafuta mteja na kisha
lori kulichoma moto.
Alisema
kuwa baada ya kufanya wizi huo walitoweka na simu zao kuzimwa na
kutokana na jitihada za jeshi la polisi kupitia mtandao wa
kimawasiliano wa kuthibiti na wizi wa mitandaoni walifanikiwa
kuwanasa watuhumiwa hao wakiwa kijiji cha Nyololo.
Mbali
ya kuwakamata dereva na tingo pia polisi wamekamata watu mbali
mbali wahusika wa mtandao huo na kuendelea kumsaka Masko Buhewa mkazi
wa Nyololo kwa kuhusika na umilikiwa wa mtandao huo .
|
No comments:
Post a Comment