Februari
ya kila mwaka huenda ikawa ni kumbukumbu mbaya kwa
mwanamitindo na Miss Tanzania 2001, Hapiness Millen Magese ambaye
mwezi huo ndipo alipogundulika kuwa hataweza kupata mtoto
katika maisha yake yote.....
Hali
hiyo ndio imemlazimu mwanamitindo huyo kuanzisha taasisi ya
kuwasaidia wanawake wengine hapa nchini ili waepuke kile ambacho
kimemkuta yeye baada ya kuondolewa uzazi kwa ugonjwa ambao
hapendi kusikia unamtokea mwanamke mwingine.....
"Nikiwa
sekondari nilikuwa napatwa na ugonjwa ambao kwa wakati huo
niliona ni wa kawaida.Nilikuwa napata maumivu makali wakati wa
hedhi yaliyonisababishia kutapika na wakati mwingine kupoteza
fahamu," anasema.
"Kila
nilipoingia kwenye hedhi nililazimika kulazwa kwa siku sita
hadi kumi hospitalini,kutokana na maumivu hayo kuna wakati
wanafunzi wenzangu waliwahi kunihoji ni kwa nini mimi kila
mwezi lazima niugue," anasimulia
Anasema
ilifika wakati wakawa wanamhesabia tarehe kutoka siku anayotoka
hospitali hadi mwezi mwingine atakapolazwa tena
"Niliteseka sana, nakumbuka kuna siku nilizidiwa wakati mama yangu hayupo.Baba akachukua jukumu la kunibeba na kunipeleka hospitali," anasema.
"Nilipokuwa
kwenye maumivu makali aliniambia nijikaze kama mwanamke, hivyo
nikawa namficha baba maradhi yangu, ingawa ilikuwa kila mwezi
kama siyo kunipeleka hospitali yeye basi lazima aje kunitazama
hospitali."
Anasema
hata baada ya kujiingiza kwenye masuala ya urembo, bado hali
ya maumivu wakati wa hedhi iliendelea na siku alipoamua
kujiingiza kwenye uanamitindo kuna watu walimuuliza atamudu
kweli kufanya mitindo na hali aliyonayo?
"Nikiwa
hapa nyumbani sikujua nasumbuliwa na nini. Siku moja nikaamua
kwenda kupima wakati huo nikiwa Afrika Kusini, nikagundulika
kuwa na ugonjwa wa Endometriosis na tiba pekee ikawa
kufanyiwa upasuaji," anasema Magese.
Anasema
alifanyiwa upasuaji mara ya kwanza na kuonyesha yai lake moja
ni bovu hivyo kutakiwa litolewe ingawa alikuwa na uwezo wa
kubeba mimba.
"Nilifanyiwa
upasuaji mara ya pili,kila siku nikalazimika kuwa nafanyiwa
uchunguzi ili kubaini maendeleo ya hali yangu, lakini cha
kushangaza hali ilizidi kuwa mbaya.Kuna wakati nilijiuliza kwa
nini mimi?" anasema Magese.
Anasema
katika kipindi hicho alikuwa anachoma sindano kila asubuhi kwa
siku 63 ili kunusuru kizazi chake bila mafanikio, aliendelea
kufanyiwa upasuaji mara 12 zaidi.
Endometriosis ni nini? Dalili zake ni zipi?
Daktari
bingwa wa magonjwa ya akina mama na uzazi wa Hospitali ya
Taifa Muhimbili, Dr. Fadhlun Almy anasema bado hajapata jina la
Kiswahili la ugonjwa wa Endometriosis, lakini unasababishwa na
seli za tumbo la uzazi kuwa nje ya kizazi.
"Dalili
za ugonjwa huu ni maumivu makali wakati wa hedhi na maumivu
hayo yanasababisha makovu ndani ya ukuta wa tumbo.Makovu hayo
yakizidi yanasababisha mirija ya uzazi kuungana na Ovari," anasema
No comments:
Post a Comment