Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Wednesday, June 11, 2014

Jennifer Lopez abadili mawazo, atashiriki ufunguzi wa kombe la dunia kesho

Jennifer Lopez abadili mawazo, atashiriki ufunguzi wa kombe la dunia kesho
Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Jennifer Lopez amebadili msimammo wa kutohudhuria sherehe za ufunguzi wa fainali za kombe la dunia, na kutangaza kuwa atakuwa sehemu ya sherehe hizo zitakazofanyika kesho huko Arena de São Paulo, mjini São Paulo.
J-Lo ambae hakutoa sababu za kutohudhuria sherehe hizo siku mbili zilizopita, amesema ameona kuna umuhimu wa kuhudhuria katika sherehe za ufunguzi hivyo hii leo usiku anatarajia kusafiri kuelekea nchini Brazil.
Amesema anaamini mashabiki wake walisikitishwa na taarifa ambazo zilitolewa na shirikisho la soka dunia FIFA za kutokuwa sehemu ya sherehe hizo hapo kesho, hivyo ameona sio jambo jema kufanya hivyo kwa kuhisi huenda akawanyima haki wanaompenda kumuona akiwa jukwaani sambamba na wasanii wengine, ambapo wataimba wimbo maalum wa kombe la dunia wa mwaka huu unaoitwa ‘We Are One’.
Wasanii wengine watakaoshirikiana na Jennifer Lopez kuimba wimbo huo ni Pitbull na mwenyeji Claudia Leitte.
 Mary J. Blige Propose

No comments: