Music Coordinator wa ZIFF, Edward
Lusala akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari
(hawapo pichani) kuhusiana na wasanii watakaotoa burudani kwenye tamasha
hilo.
Lupita Nyong’o, Genevieve ndani ya nyumba
Tukio kubwa ambalo kwa sasa Tanzania hasa
kwenye viunga vya Zanzibar na nchi nyingine duniani katika tamasha hilo
la 17, ni ujio wa msanii wa Kenya na Mexico, Lupita Nyong’o,
atakayeudhuria utoaji wa tuzo hizo za ZIFF mwaka huu.
Lupita ambaye ametwaa tuzo za Oscar na
nyingine nyingi na kupelekea kutikisa Hollywood kwa sasa ni miongoni mwa
mastaa watakaokuwa kwenye tamasha hilo huku akitarajiwa kuambatana na
wazazi wake wote wawili pamoja na wadogo zake.
Prof. Mhando amesema tayari wazazi wote
wawili wa Lupita akiwemo Dorothy na Peter Anyang’ Nyong’o, watakuwapo
kwa siku zote 10 kwenye tamasha hilo huku Lupita mwenyewe akiahidi
kuangalia uwezekano wa kuhudhuria japo katika utoaji wa tuzo kama ratiba
za shughuli zake hazita mbana.
Prof. Mhando alisema Lupita ni zao la ZIFF
na ndiyo iliyomfungulia mwanya wa kujulikana na baadaye alienda kusoma
zaidi masuala hayo ya filamu, ambapo alishiriki ZIFF 2007 kama
Volunteer.
Mara nyingi staa huyo amekua akihudhuria
matamasha na halfa mbalimbali za utoaji wa tuzo na zawadi zingine huku
akiwa ameambatana na wazazi wake wote wawili.
Lupita mbali na tuzo hiyo ya Oscar, kupitia
filamu ya ‘12 Years a Slave’ pia filamu hiyo imempatia tuzo mbalimbali
zikiwemo: tuzo ya Steve McQueen kama mwigizaji mwenye mvuto, mwigizaji
bora wa kike aliyeshirikishwa, ‘Academy Award’, ‘Screen Actors’ Guild
Award’, ‘NAACP Image Award’, ‘Independent Spirit Award’, ‘Broadcast Film
Critics Association Award’, na nyingine nyingi.
Genevieve Nnaji.
Mbali na Lupita, katika kuongeza utamu wa
tamasha hilo, mastaa wengine nguli wa Afrika kwa mwaka huu wanaotarajiwa
kuwapo katika ushuhudiaji wa utoaji wa tuzo hizo ni pamoja na muigizaji
na mwanamitindo nyota wa Nigeria, Genevieve Nnaji.
Wengine ni Amr Waked (Misri), Faouzi
Bensaidi (Morocco), Nadia Buari, Richard Mote Damijo ‘RMD’, John
Dumelo, Desmond Eliot na Florence Masebe.
No comments:
Post a Comment