Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Sunday, October 3, 2010

AMISUU AMKANA DIAMOND!!...KUMBE HAJAONA NDANI
                     Amisuu mmalik

    Mlimbwende wa miss Tanzania 2010 ambae alishika nafasi ya tatu miss kinondoni Amisuu mmalik ameukana uvumi uliotapakaa kila kona ya nchi kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki wa bongo flava Diamond.
     Akiongea kwa njia ya simu na Uniqueentertz blog na kusema hana uhusiano na kijana huyo hajamfikiria kama siku moja atakuwa na Diamond kwani mwanamuziki huyo amekuwa rafiki wa kawaida tu japokuwa amekuwa akiomba ridhaa kwa Amisuu amkubali na hajajibiwa lolote "nashangaa Diamond anawaambia watu kuwa mimi ni mpenzi wake angali anajua mimi nna mtu wangu" alilalamika Amisuu.
     Nilipomuuliza Amisuu kama kijana huyo mbana pua ashawai kujiachiia nae japo kwa chati kama inavodaiwa na magazeti ya udaku..Amisuu alikana na kusema mwanamuziki huyo amekuwa akiongea nae kwa simu na kumtembelea sehemu ambazo amisuu akiwepo ambapo katika usiku wa kumtafuta balozi wa mitindo wa Redds pale malaika,Diamond alonekana akitafuta kila njia mpaka akapata nafasi ya kubonga na mrembo huyo kwani alionekana kuhangaika kupiga simu wakati Amisuu anaposhuka jukwaani na baada kusogea nyuma ya jukwaa.
    "mamii...mamii....aah..umependeza sana ..." hii ni kauli iliyodakwa na blog hii toka kwa Diamond ambapo amisuu akiwa ameshuka stejini ambapo nilikuwa nae karibu nikisikia akiongea na mrembo huyo,kwakuwa namfahamu sana hamisuu na Diamond ni kijana wetu nikamuuliza ..vp untoka na huyo mrembo?..Diamond akacheka kisha akabadili mkao.
     Kinyume na hayo Amisuu alikana kuwa na uhusiani na kijana huyo mpaka akaapa kwa jina menyezi ....nikawa sia swali zaidi  basi tuamini ivyo wadau.

USIKU WA SHEAR CHARITY BALL

Mkurugenzi wa Shear Illutions, Shekha Nasser akisoma hotuba yake mbele ya wageni waalikwa mbalimbali katika harambee ya kuchangia juhudi za CCBRT katika kusaidia watoto wenye matatizo.

Mkurugenzi wa Shear Illutions Shekha Nasser akizindua rasmi jarida la Shear kwa kutimiza mwaka mmoja,hafla hiyo ilikwenda sambamba na tukio la Shear Charity ball usiku huu ndani ya hotel ya Double Tree Hilton,Masaki jijini Dar.

Mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia Juhudi za CCBRT katika kusaidia watoto wenye matatizo,Bw. Januari Makamba akizungumza mbele ya wageni waalikwa katika harambee hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree Hilton,Masaki jijini Dar usiku huu.Bw. Januari Makamba amewataka watanzania kusaidia watoto wenye matatizo ili nao waweze kupata mahitaji muhimu kama watoto wengine na kuwapunguzia matatizo waliyonayo.
Baadhi warembo wakiwa katika picha ya pamoja pindi waliposhiriki katika tukio la Shear Charity Ball usiku huu,ndani ya hotel ya Double Tree Hilton,Masaki jijini Dar.
Raqey akiwa na mkewe pamoja na Mdau mwingine wote kutoka I-View Photography

Mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia Juhudi za CCBRT katika kusaidia watoto wenye matatizo, Januari Makamba wa pili kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano Vodacom Tanzania,Mwamvita Makamba kulia na kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa na katikati ni Lissa Jensen aliyewahi kuwa mshiriki wa Miss Tanzania.
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia tukio la Shear Charity Ball usiku huu.

Ma Mc wa shughuli hii maalumu iliofanyika usiku huu ndani ya moja ya ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Double Tree Hilton,shoto ni Taji Liundi pamoja na Penny.

Wageni waalikwa mbalimbali walioshiriki katika harambee ya Shear Charity Ball iliyokuwa maalum kwa ajili ya kuchangia harakati za CCBRT katika kusaidia watoto wenye matatizo.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Vodacom Tanzania,Mwavita Makamba kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Meya wa Wilaya ya Ilala, Jerry Silaa kulia na katikati ni mrembo Lissa Jensen.

Wageni waalikwa mbalimbali wakiwasili katika kushiriki harambee ya Shear Charity Ball iliyokuwa maalum kwa ajili ya kuchangia harakati za taasisi ya CCBRT katika kusaidia watoto wenye matatizo mbalimbali.Picha na Full Shangwe na Jiachie Blogs.
 

No comments: