Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Monday, October 18, 2010

breaking news..!!

UDHAMINI WA GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL WAFIKIA 35ML


  Udhamini wa hoteli ya giraffe katika shindano la Girafee unique model 2010 umefikia milioni 35 za kitanzania ambapo baadhi ya mambo mengine na wadhamini kadhaa wakijitokeza kudhamini shindano hilo la mitindo ambalo linategemewa kua la aina yake kwa kufungia mwaka kimitindo
   Girrafe unique model ni shindano la kumtafuta mwanamitindo wa kike mwenye sifa za tofauti ikiwa na lengo kuu la kuleta mapinduzi ya mitindo nchini tanzania
   Pia mbunifu wa mavazi nchini Tanzania ali lemtulah amejitokeza kama mdhamini wa mavazi na mtu atayemchukua model mmoja kama balozi wa nembo ya nguo zake zinazotegemewa kuzinduliwa mwanzoni mwa mwaka ambae atafanya kazi na mwanamitindo huyo kwa mwaka mzima ....ni kitu kikubwa sana watanzania.


WASANII WA RAGGA NA REGGAE KUTUMBUIZA PAMOJA
                                              Msanii kutoka JAMAICA ZANZI- B
Msanii wa miondoko ya Ragga kutoka nchini JAMAICA ZANZI- B anatarajia kushiriki katika tamasha la ‘EXPLOSIVE ZION” lenye lengo la kukumbuka kifo cha nguli wa miondoko ya REGGAE hayati LUCKY DUBE wa AFRIKA KUSINI. 

Meneja wa kampuni ya I-NOCH ambao ndiyo waratibu wa tamasha hilo MUKALAY MTANGAZA na mwanamuziki JHIKOMAN wamesema mbali na kumuenzi LUCK DUBE tamasha hilo litasaidia kuwainua wasanii chipukizi wa fani ya reggae, ragga na dance hall.

Katika tamasha hilo litakalofanyika OCTOBA 29 katika ukumbi wa makumbusho KIJITONYAMA jijini DSM, burudani kutoka kwa wasani wa hapa nchini JHIKO MAN, AFRIKABISA BAND, HARD MAN, SAGANDA na ZEMKALA BAND pia itawaka moto na hapa wanatupa radha ya kile kitakachotokea
 

DHL WATOA VYANDARUA 1500 KITUO CHA KULELEA WATOTO SOS

Wafanyabiashara wanaojishughulisha na usafirishaji wa vifurushi na bidhaa mbalimbali DHL wametoa msaada wa vyandarua 1,500 leo kwa nyumba ya kulelea watoto yatima wanaoishi katika kituo cha (SOS Childrens Villages) kilichopo barabara ya Sam Nujoma Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa vyandarua hivyo Mkurugenzi Taifa wa Kijiji hicho cha SOS, Rita Kahurananga alisema kwa niaba ya kituo,watoto na uongozi wote wa SOS wanatoa shukrani za dhati kwa DHL.

Alisema msaada huo umekuwa ukiwa ni katika mpango mkakati wa kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria pia wakukuwa wakihitaji vyandarua hivyo msaada huo umekuja kwa wakati muafaka .

Kahuranaga aliendelea kwa kusema kuwa vyandarua hivyo watavigawa katika vituo vyao vungine vya kulelea watoto vilivyoko Mwanza, Arusha, Zanzibar, Bagamoyo, Shinyanga na Iringa.

Wakati huohuo aliongeza kwa kusema kuwa wanampango wa kuanzisha vituo vingine vya kulelea watoto katika kisiwa cha Pemba, Mtwara, Iringa na Mbeya ambapo pia wanahitaji wadhamini wajitokeza ili kufanikisha mpango huo endelevu.

Kituo cha SOS kiliasisiwa na Herman Gmeiner ambapo kituo cha kwanza alikilianzisha mwaka 1949 nchini Australia.
SOS ni shirika lisilo la kiserikali na wenye mipango ya muda mrefu ya kuweka malezi bora kwa watoto ambao huanza kulelewa kuanzia umri wa kuzaliwa hadi wanapopata umri mkubwa huku wengine wakimudu kujitengemea ambapo inalea watoto 419 katika vituo.
Mwisho.

Mtoto Kulwa akizunguma na mimi mara baada ya kukabidhiwa vyandarua hapa akirudi darasani.

No comments: