MAMBO YA KIDOSI NA UFUGAJI WA DHATI
Mama wa kidosi akimnyonyesha ndama wake,ni mapenzi makubwa kwa wanyama au ni balaa
The way anavomuhusidu ndama huyu mpaka anampakata kama kichanga..
TAMKO LANGU KUHUSU MOVIE YA FAMILY DISASTER
Msingi mkuu wa Taifa ni jamii zilizostawi barabara,ambazo nazo hujengwa na familia imara zilizo katika himaya ya mihimili mikuu miwili;yaani baba na mama,walioungana kwa ndoa sahihi kulingana na jamii husika.Msingi huu mkuu; familia ikistawi vema hufanya kila uzao utokao hapo kuwa ni imara na wa kupigiwa mfano,hii ina maana kuwa watoto watakuwa na tabia zilizotukuka na zinazozaa maadili mema yanayowafanya wawe kioo cha Taifa popote walipo.Na kwa upande mwingine, msingi huu mkuu ukishindwa kutekeleza majukumu yake sawa sawa, inakuwa ni sawa na chumvi iliyoharibika huwezi kuitia kitu chochote ikakolea na kuvutia.Kipindi cha tangu kuzaliwa mwana mpaka kufikia umri wa kwenda shule, huwa ni kipindi cha matunzo kwa mwana; anatunzwa kwa ajili ya kufikia utu uzima aweze kujitegemea akiwa katika afya njema tayari kukabiliana na majukumu ya utu uzima.Kwa upande mwingine, kipindi cha malezi huanza pale watoto wanapofikia umri wa miaka kumi na ziada,kwani hapo mtoto anakuwa tayari kwa maandalizi ya kuwa mtu mzima. Kipindi hiki huwa kinamfanya mtoto kuwa mdadisi mno kwa kila kitu anachokiona hususani yale yanayohusiana na mambo ya kimahusiano; kipindi hiki ni kipindi muhimu sana kwa wazazi na watoto kwani inatakiwa kuwa karibu sana kuliko kipindi chochote kwani watoto wana matarajio makubwa sana kutoka kwa wazazi wao kwa kila wanachohitaji kukijua,na kwa kuwa wazazi tayari wameshashuhudia kipindi kama hicho inakuwa rahisi kwao kuwaelekeza,kinyume chake mambo yatakuwa mabaya kuliko inavyofikiriwa.
FAMILY DISASTER ni kisa kinachoonesha jinsi wazazi wanaposhindwa kukubali kuyatwaa majukumu yao na kuharibu kabisa ustawi wa familia zao.Wazazi kwa kuthamini sana nafsi zao kuliko za watoto wao,wanajikuta wakivutana badala ya kuwalea watoto wao,kitu ambacho kinasababisha watoto hao kukosa kupata malezi ya mambo muhimu na kujikuta wakiiga tabia mabya kutoka kwa majirani,marafiki na watu wengine wasio na maadili, kwasababu ustawi wa familia haupo.Sina maana mbaya kutengeneza filamu hii, Maana yangu ni nzuri tu nia ni kuelimisha jamii .Kuhusu kuvaa nguo fupi ni jinsi story inavyotaka maana hawa watoto wameigiza kama watukutu waliokosa maadili.Wadau nisimalize uhondo nataka mtambue kitu kimoja katika maisha kuwa huwezi kujifunza kitu bila kukosea .Nina uhakika tena mkubwa sana filamu hii itakuwa fundisho kubwa kwa wazazi na watoto wote wasiokuwa na maadili. Naomba tusubiri wadau.
No comments:
Post a Comment