MISS EARTH 2010 ROSE SHAYO ASHIRIKI KUFANYA USAFI MANISPAA YA KINONDONI.
MISS Earth Tanzania 2010, Rose Shayo kwa mara ya kwanza leo ameshiriki katika moja ya program zake za kijamii kwa kufanya usafi katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Program hiyo iliyoandaliwa na mrembo huyo na kusimamiwa na Kampuni inayoandaa mashindano hayo kwa ngazi ya taifa 'Compass Communiacation' chini ya Mkurugenzi wake Maria Sarungi ilianzia katika Ufukwe wa Coco Beach na maeneo jirani na ufukwe huo uliopo Masaki. Akizungumza na Mwananchi, mrembo huyo alisema kuwa huo ni mwanzo tu katika program zake za kufanya kazi za kijamii na kuahidi kuwa atakuwa bega kwa bega na watanzania kuhakikisha analitumia taji hilo vema katika masuala ya kijamii. "Nijukumu la watanzania wote kuhakikisha tunaiweka nchi yetu katika hali ya usafi, mimi kama miss Earth Tanzania na jukumu kubwa la kuhakikisha nchi yangu inakuwa katika hali ya usafi, nimeanzia katika manispaa hii ya Kinondoni na baada ya kurejea nchini kutoka Vietnam nitaendelea na manispaa nyingine", alisema Shayo. Naye Kaimu Afisa Afya Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Johnson Ndaro, alisema kuwa mrembo huyo ameonyesha uzalendo wa hali ya juu na kuongeza kuwa kitendo hicho kinatakiwa kuigwa na watu wengine ambao anaimani Kinondoni bila uchafu inawezekana. Shayo anatarajia kupanda Jukwaani mwanzoni mwa mwezi Novemba nchini Vietinam kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Earth Duniani huku matarajio yake yakiwa ni kuiwakilisha nchi vema kwa kutwaa taji hilo
No comments:
Post a Comment