Party ya uzinduzi rasmi ya Jukwaa la Tatu la Swahili Fashion week, itafnyika kesho jumamosi katika ukumbi wa Mach More Bilicanas Group, kuanzia saa 4:00 usiku.
Katika shughuli hiyo itawaleta pamoja wabunifu wa mvazi mbalimbali waliopo hapa nchini na wale ambao watashiriki Swahili Fashion Week ya mwaka huu, Sambamba na hao pia watakuwepo walibwende wa aina mbalimbali ambao watapamba jukwaa la Swahili Fashion Week.
“Tunaamini kwamba kufanyika kwa party ya uzinduzi ni mwanzo mzuri na tunategemea kuwa jukwaa la tatu la Swahili Fashion Week litakuwa bora, kutokana na maandalizi yake kuwa mazuri zaidi, watanzania wategemee kuona vitu tofauti na mwaka jana” Alisema Mustafa Hassanali, muandaaji wa Swahili Fashion Week.
“Kiingilio ni shillingi 20,000/= tu, itapendeza tukijumuika pamoja katika kusheherekea na kuunga mkono Sanaa ya ubunifu wa mavazi hapa nchini”. Alieleza Roy Mbowe wa East Africa Radio.
“Katika Sherehe hiyo ya uzinduzi kutakuwepo na burudani mbalimbali za kuvutia pamoja na bahati na sibu za aina mbalimbli, sambamba na muziki kabambe kutoka kwa DJ wa East Africa Radio”. Aliongeze Roy Mbowe Meneja Masoko kutoka East Africa Radio.
Swahili Fashion Week ni jukwaa linalowakutanisha wabunifu wa mavazi kutoka nchi zinazozungumza lugha ya Kiswahili, mbalo litakalofanyika kuanzia November 4 , 5 na 6 katika Bustani ya Karimjee, Dar es Salaam.
Swahili fashion week 2010 imedhaminiwa na Home of Swahili Fashion week Southern Sun, Origin Africa, USAID Compete, EATV, East Africa Radio, Malaria Haikubaliki, BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania) Ultimate Security, Monier 2000, Colour Print ltd, Global Outdoor Ltd, Amarula, Vayle Springs Ltd, ZG Films, Darling Hair, Danish make up designs, Nipashe, Bilicanas, Perfect Machinery LTD, 1 & 1 internet solutions, Sengi Tours, Ifashion na 361 Degrees.
No comments:
Post a Comment