Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Saturday, April 9, 2011

CHADEMA KUANDAMANA NCHI NZIMA WIKI IJAYO

               freeman Mbowe kiongzi wa chadema
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema Jumamosi ijayo kitafanya maandamano nchi nzima kupinga muswada wa sheria wa mabadiliko ya Katiba unaoendelea kujadiliwa.

Akizungumza kwenye Viwanja vya Bunge jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema wabunge wote wa chama hicho watatawanywa nchi nzima kushiriki maandamano hayo.

Mbowe alisema lengo kubwa la maandamano hayo ni kupinga muswada huo kupelekwa haraka haraka na pia kukipa chama hicho fursa ya kupata maoni ya wananchi wengi zaidi.

“Jumamosi wiki ijayo tunaandamana nchi nzima, wabunge wote wa Chadema watatawanyika nchi nzima, lengo ni kupata maoni ya wananchi wengi,” alisema Mbowe.

            Alipinga hoja ya Serikali kwamba muswada huo usipopitishwa hivi sasa, hautakuwa na nafasi kwa sababu Bunge la Juni linahusika na Bajeti. Alisema miswada mingi imeshapitishwa kwa hati ya dharura.

           “Tunataka maoni ya wananchi wengi yakusanywe ili yazingatiwe, muswada uletwe bungeni Juni. Suala la kwamba Bunge la Juni ni la bajeti ni sawa, lakini mwaka jana uliletwa muswada wa Gharama za Uchaguzi kwa hati ya dharura ukapita,” alisema.

              Mbowe alisema Chadema kitaendelea kupinga muswada huo kusukumwa haraka haraka na kuwakosesha wananchi fursa ya kuchangia na kwamba, iwapo makosa yatafanyika na kupitishwa hivi sasa, yatakuwa ni majuto makubwa siku zijazo.

            Kuhusu vijana wanaozomea kuhusishwa na Chadema, Mbowe alisema kuzomea ni kuonyesha hisia na kwamba muda wa ubabe kwa CCM umekwisha.“Waacheni wazomee, waacheni washangilie kama unawakataza kuzomea, wakataze na kushangilia. Mbona CCM wakishangiliwa hawakatai, sisi tunazomewa sana lakini tunaamini wanaonyesha hisia zao,” alisema na kuongeza:

           “Kuna wanaozomea kama wabunge wa CCM humu ndani? (Bungeni), tunapoonyesha hisia zetu, hisia za wananchi kwa kutoka ndani ya ukumbi mnaona na kusikia jinsi wanavyotuzomea.”

          Mbowe alisema kuzomewa kunawafundisha wanasiasa kusoma alama za nyakati na kwamba tuhuma za kila mara kwa chama hicho ni hofu ya watawala.Alisema suala la Katiba halitakiwi kubebwa na kuonekana kama ni mali ya kundi, chama au watu fulani, bali kushirikisha wananchi wote, huku akitahadharisha kuwa iwapo wataacha muswada huo kupita na upungufu huo, yatakuwa majuto makubwa siku zijazo.

          Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alidai muswada wa sheria unaopingwa na wadau takriban asilimia 90, hauwezi kusimamiwa kupita kwa nguvu ya dola.Kuhusu chama hicho kutuhumiwa kuhusika na vurugu, Mbowe alisema hizo ni propaganda kwa chama chochote cha siasa, lakini Chadema itaendelea kuhamasisha wananchi kudai haki zao.



VICHWA VYA AJABU 
Unapoumbwa vilivyo unatakiwa kumshukuru mungu

Somaya Reece Used to Do Porn? Photos from One of Her Movies Leak!

Somaya Reece from Love and Hip Hop used to be a porn star, according to Media Takeout.  The gossip site got their hands on stills from one of her pornographic films.  You can see them by clicking the link below.


Gucci Mane Arrested for Pushing Some Chick Out of a Moving Car!


       Gucci Mane was arrested to today and is being charged with a misdemeanor count of battery for pushing a woman out of a moving car in the middle of a dispute.
The crazy thing was that Gucci was arrested by the DeKalb County Fugitive Squad while visiting his probation officer.  Let’s just hope that these claims are false because if they are true Gucci may have to face more jail time.

No comments: