Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendleo(CHADEMA)
Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)kimesitisha maandamano siku ya kesho kutokana serekali kukubali kuongeza muda wa kujadili muswada wa katiba mpya.
MBUNGE ANASWA AKIPIGACHABO PICHA ZA NGONO BUNGENI
Arifinto akipiga chabo video za ngono ndani ya Bunge | Friday, April 15, 2011 2:40 AM Mbunge wa nchini Indonesia ambaye alijipatia umaarufu kwa kusimama kidete kushinikiza sheria kali zipitishwe kama vile kutupwa jela miaka 15 kwa kushiriki kwenye video za ngono, mbunge huyo amelazimika kujiuzulu baada ya kunaswa akiangalia ngono bungeni. | |
Arifinto, mwanasiasa wa nchini Indonesia ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kupigania sheria za kupinga video na picha za ngono, amenaswa akiangalia video ya ngono ndani ya kikao cha bunge. Arifinto alilazimika kujiuzulu ubunge baada ya picha zake kusambaa kwenye vyombo vya habari zikimwonyesha akiwa bize kwenye laptop yake akiangalia video ya ngono. Arifinto alikuwa miongoni mwa wanasiasa walioshinikiza na hatimaye kupitishwa kwa sheria ya kupinga picha, video na vitendo vya ngono hadharani. Sheria hiyo iliyopitishwa mwaka 2008 inaweka wazi kuwa adhabu ya kutupwa jela hadi miaka 15 au kupigwa faini itamkumba mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kubusiana hadharani au kuangalia picha au video za ngono. Kuzionyesha, kuzimiliki au kuzihifadhi video au picha za ngono ni marufuku kwa mujibu wa sheria hiyo. Arifinto mwenye umri wa miaka 51 ambaye pia ni baba wa watoto watano, alikuwa ndio msemaji mkubwa wa kushinikiza kupitishwa kwa sheria hiyo. Arifinto aliitisha kikao na kutangaza mbele ya waandishi wa habari kuwa anajiuzulu ubunge wake mara moja. "Huu ni uamuzi wangu, hakuna mtu aliyenishinikiza kufanya hivyo", alisema Arifinto ambaye kama raia wengine wa Indonesia anajulikana kwa jina moja tu. Indonesia, ni nchi ya kidemokrasia yenye jumla ya watu milioni 237, ndiyo nchi yenye waislamu wengi kuliko nchi zote duniani. BASI LA NGOLIKA LAPATA AJAlI WATU 10 wamefariki dunia na wengine wanane kujeruhiwa -- wanne kati yao wakiwa katika hali mbaya -- baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana na kupinduka katika eneo la Makumira wilaya ya Arumeru mkoani Arusha majira ya saa 12.20 asubuhi. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Thobias Andengenye, ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T 773 BGT lililokuwa likiendeshwa na Selemani Juma (30) mkazi wa Kijenge, na basi la Ngorika aina ya Scania lenye namba T 633 ANF lililokuwa likiendeshwa na Emmanuel Mchoro (30) mkazi wa Mwanga Kilimanjaro. Andengenye alisema chanzo cha ajali hilo kimetokana na Hiace kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake ambapo alikuweko pia mwendesha baiskeli. Hata hivyo, kabla ya kufikia uamuzi huo aliona basi hilo la Ngorika likija kwa kasi ndipo alipoamua kulikwepa ili asigongane nalo uso kwa uso. Kabla hajamaliza kufanya hivyo basi la Ngorika liliigonga Hiace hiyo ubavuni na kusababisha watu tisa waliokuwa ndani ya gari hilo kufariki dunia papo hapo. Andengenye aliwataja marehemu hao kuwa ni: Kizo Rafael Ndosi (35) mkazi wa Arumeru, Patriki Temba (28) mkazi wa Usa River, Samsoni Emanuel Minja (60), Hamisi Charles(30) mkazi Usa River, John Kess(38) mkazi wa Majichai na Huruma Safiel (28) mkazi wa Usa River. Wengine ni Emmanuel Mchoro (30) mkazi wa Mwanga ambaye yeye ni dereva wa basi la Ngorika na Fatuma Msuya (35) mkazi wa Usa River ambaye ni mwanamke pekee aliyefariki katika ajali hiyo na mpanda baiskeli aliyejulikana kwa jina moja la Elvisa. Alisema mpaka sasa jeshi la polisi linamshikilia dereva wa Hiace mpaka pale upelelezi utakapokamilika. Mganga Mkuu Mkoa wa Arusha, Salashi Toure, alisema wamepokea majeruhi 16 ambapo kati ya hao mmoja amehamishiwa hospitali ya Seliani kutokana na mapafu yake kuvuja damu nyingi. Dereva wa basi la Ngorika, Emmanuel Mchoro(30) akiwa amebebwa kutoka ndani ya basi hilo akiwa amekufa, baada ya kulaliwa na basi hilo kwa muda wa masaa matano. Lil Wayne’s Crew Gets Busted for Impersonating Police OfficersIt seems like Lil Wayne just can’t out of the news. During a show in Indianapolis members of Lil Wayne’s security team have been arrested on charges of impersonating police officers. The arrests stem from the suspects driving an unmarked car wearing police uniforms. They were reported to be leading Wayne’s tour bus to a night club after his performance. No idea why they couldn’t get real police escorts but any press is good press. Let’s just pray that Weezy doesn’t get caught up in this mess and ends up back in the slammer. We need Weezy home! |
No comments:
Post a Comment