WAZIRI MWANDOSYA AREJEA NYUMBANI
Waziri
wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya
Apollo, nchini India, kwa takriban miezi minane, amerejea nchini, baada
ya afya yake kuimarika. Habari
zilizopatikana jijini Dar es Salaam zilizothibitishwa na Naibu Waziri
wa Wizara hiyo, Mhandisi Gerson Lwenge, Profesa Mwandosya alirejea
nchini juzi. Mwingine
aliyethibitisha jana kurejea kwa waziri huyo mwandamizi, ni mkewe, Lucy
Mwandosya. Hata hivyo, Mhandisi Lwenge, ambaye alizungumza na
jana, alipotakiwa kueleza maendeleo ya afya ya Waziri Mwandosya,
alijibu: “Sijamuona, ndio naenda. Ukinitafuta baadaye nitakwambia.” Awali,
Mhandisi Lwenge, alipoulizwa kama Waziri Mwandosya amerejea nchini,
alijibu: “Ndio amerudi” na alipotakiwa kueleza lini alirejea, alijibu:
“Jana (juzi).” Baadaye,
majira ya saa 11.05 jioni jana, ilimtafuta Profesa Mwandosya
kwa simu yake ya mkononi, ambayo ilipokelewa na mkewe, Lucy. Baada
ya mwandishi kujitambulisha na kueleza shida yake ya kutaka kuzungumza
na Profesa Mwandosya, Lucy, alisema muda huo waziri asingeweza
kuzungumza kwa vile alikuwa anapumzika.
MILIONI 55 ZAKUSANYWA RED RIBBON FASHION SHOW
MILIONI 55 ZAKUSANYWA RED RIBBON FASHION SHOW
WAKATI jumla ya sh.
Milioni 55 zimechangishwa katika maonyesho ya mitindo kwa ajili ya
kuadhimisha siku ya ugonjwa hatari wa UKIMWI duniani (Red Ribbon Fashion
Gala), mwanamuziki nyota nchini, Diamond aling’ara vilivyo kwa kuonyesha kipaji kingine cha maonyesho ya mavazi.
Fedha
hizo zilipatikana kwa njia ya mnada wa vitu mbali mbali na nyingine
zikitolewa kwa njia ya udhamini wa shughuli hiyo iliyotumika pia
kuadhimisha siku ya ugonjwa hatari wa Ukimwi Duniani.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Tanzania Mitindo House (TMH), Khadija Mwanamboka
aliwashukuru wadau wa maonyesho ya mavazi kwa kujitolea kufanikisha
kupatikana kwa fedha hizo ambazo zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa kituo
cha mafunzo ya fani mbali mbali kwa watoto yatima wanaoishi na virusi
vya Ukimwi.
Mwanamboka
alisema kuwa kituo hicho kitajengwa jijini na kitatoa mafunzo ya njia
mbali mbali za kupambana na maisha, Ujasiliamali, Ushonaji nguo,
mafunzo ya kompyuta na jinsi ya ubinifu wa mitindo au mavazi. Alisema
kuwa jumla ya watoto yatima 100 watakuwa wanapata mafunzo katika kituo
hicho kila mwaka.
Baadhi
ya wadhamini waliochangia kufanikisha kwa fedha hizo ni kampuni ya
simu ya mkononi, Vodacom Tanzania na wadau wa maonyesho ya mavazi ambao
walichangia kimya kimya katika maonyesho hayo yaliyofanyika kwenye
hotel ya Double Tree.
Katika
maonyesho hayo, mkali wa miondoko ya Bongo Fleva nchini, Diamond naye
alifanya vitu vyake jukwaani kwa kuvaa nguo aina ya Kidoti iliyobuniwa
na mbunifu chipukizi, Jokate Mwegelo.
Wengine
walioonyesha mavazi jukwani ni Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark
Production, Ritha Poulsen ambaye baadaye nguo yake iliunuliwa na mcheza
filamu maarufu nchini, Steven Kanumba.
Wabunifu
mbali mbali akiwemo Doreen Estazia nao walionyesha mavazi yao, Doreeen
alionyesha mitindo yake maarufu ya Eskado Bird. Wabunufu wengine
waliotamba katika maonyesho hayo ni Ali Rhemtullah, Diana Magese, Mollel
na Zamda.
Wadhamini
wengine wa shughuli iyo walikuwa Redds, Clouds Entertainment, Kiondo
Communications, I_View Media team na Hall Neel Production. Wengine
waliosaidia maonyesho hayo ya mavazi ni Amaya Beauty Saloon and SPA,
Bank M Tanzaniia, Stanbic Bank, Mimis collections, Kidoti By Jokate
Mwegelo, Bongo Real Mamaz na Bluecherriemoe.
Wadau wengine ni Flaviana Matata Foundation, Amina
Design, Jenifa Pemba, FM Express events and services ltd, Ernst
&Young, ,LR Creations, Millen Magese Foundation Tiffex, Cool Blue
Iku Lazaro, Miraj Kikwete, Halima Kamus, Mabibo Beer Wines nd Spirits
Ltd, and World Link Travel and Tours ltd.
No comments:
Post a Comment