Wema na Diamond
Habari zisizo rasmi zilizoenea mjini ni kwamba Wema sepetu amjia juu Jokate baada ya kusemekana alivunja amri ya sita wakati wakifanya video ya "mawazo" na Mchumba wa Wema namzungumzia Diamond.
Nyeti zinaendelea kusema Wema alifumania Jokate akibadilisha radha ya ndimi na Diamond,hata hivyo wema alilalama sana kutokana na kumwamini JOKATE ni rafiki wa karibu asingeweza kumpa mambo Diamond.
nyeti zaidi...
KISHINDO
cha Jokate Mwegelo ni kizito, kimeingia ndani ya uhusiano wa brazameni,
Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Wema Sepetu kisha kuwafanya wawili hao kila
mmoja kushika hamsini zake.
Wema,
amefunga virago, ameondoka nyumbani kwa Diamond, Sinza Madukani, Dar es
Salaam kwa mtindo wa “wanakwenu kwa heri, nimechoka masimango, narudi
nyumbani kwetu leo.”
Madai
‘yanahiti pointi’ kuwa Diamond na Jokate wapo kwenye penzi jipya lenye
nguvu, Wema ameligundua hilo, ameona ni maji marefu, kwa hiyo amejiweka
pembeni kuepuka msongamano.
Inazidi kudaiwa kwamba Wema alijaribu kumfanya Diamond atulie lakini ikashindikana, ilipodhihirika Jokate ameshika mpini, alianza kupata mateso ya moyo na hisia kwa jinsi alivyofanywa ‘spea tairi’.
Madai ‘yanahiti’ pia kwamba Wema alithibitisha kuwa Diamond na Jokate
wanamchezea ‘ukuti ukuti’ baada ya kuwafumania wakiwa ‘vere klozi’
kimahaba kwenye Hoteli ya Picolo, Masaki, Dar es Salaam.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa Wema alipowakuta Diamond na Jokate,
hakuangusha varangati kama mmiliki, badala yake alinywea utadhani yeye
ndiye mwizi kisha akawaambia: “Samahanini sana kwa kuwaingilia kwenye
starehe zenu.”
WAZIRI NCHIMBI AUNDA KAMATI YA KUPATA VAZI LA TAIFA
WIZARA
ya Habari, vijana, utamaduni na michezo, imesema mchakato wa kupata
vazi la taifa unaendelea vizuri kwani wabunifu wazalendo wa mitindo ya
mavazi nchini wameshirikishwa na kutoa mapendekezo yao.
Taarifa ya waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo, DOKTA Emmanuel Nchimbi amesema ili kuhitimisha mchakato huo.
Kamati maalum ya kukamilisha mchakato huo imeundwa ambapo kamati hiyo
inaongozwa na Mwenyekiti wake JOSEPH KUSAGA, katibu wake ni ANGELA NGOWI.
Wengine
ni wajumbe ambao ni HABIBU GUNZE, JOYCE MHAVILLE, MUSTAFA HASSANALI,
ABSALOOM KIBANDA, MAKWAIYA KUHENGA na NDESAMBUKA MERINYO.
Itakumbukwa
kuwa Serikali, kupitia Idara ya Maendeleo ya Utamaduni ya Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ilianzisha mchakato wa kupata Vazi
la Taifa mwaka 2004.
No comments:
Post a Comment