Rais
Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa shindano la
kumsaka Miss Utalii wa Dunia mwaka 2006 mara walipomtembelea IKULU
(Picha na Maktaba ya Miss Utalii ORG.
Rais Kikwete akiwa na Gideon Chipungahelo (Chips)
Tanzania
kwa mara nyingine tena imepewa heshima ya kuwa wenyeji wa fainali za
Dunia za Miss Utalii ,ambapo safari hii , Kamati ya Dunia ya Miss
Tourism United Nation Organisation, imeipa heshima ya kuwa wenyeji wa
shindano la Miss tourism United Nations World 2012.
Kupitia
kampuni ya Miss Tourism Tanzania Organization, waandaaji wa mashindano
ya Miss Utalii Tanzania, Tanzania imezishinda nchi nyingine nne zilizo
kuwa zikiwania fulsa hiyo adimu, nchi hizo ni pamoja na Jamaica,
Korea,China,Kenya na Nigeria.
Sambamba
na uteuzi huo, kamati hiyo ya Dunia imemteua Gideon E.G.chipungahelo
kuwa mkurugenzi wa mashindano hayo barani afrika , na makamu wa rais wa
mashindano hayo Duniani .kuanzia Novemba 1,2011.
Mashindano
hayo yatashirikisha jumla ya nchi 120, duniani, na kurushwa LIVE katika
TV za nchi zaidi 100 duniani kote. Pamoja na washiri hao,waandishi wa
habari kutoka nchi zaidi 70 , vipngozi zaidi 120 na wanafamilia zaidi
200 wanatarajiwa kuja nchini sambamba na washiriki wa mashindano hayo.
Tuna mshukuru mungu kwa kuweza kushinda nafasi na heshima hii kwa nchi
yetu, hasa katika wakati huu ambapo ushindani katika sekta ya utalii na
uwekezaji baina ya nchi na hata baina ya mabara ni mkubwa. Tunajisikia
ufahari kwa nchi yetu na kuwa sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali
katika kutangaza utalii,utamaduni na mianya ya uwekezaji wa Tanzania
kitaifa na kimataifa. Shindano hili litatyoa fulsa ya pekee kwa Tanzania
,kutangaza utalii,utamaduni na mianya ya uwekezaji kimataifa na hata
kitaifa,pia kuuthibitishia ulimwengu kuwa vivutio vikuu vya utalii
Afrika ikiwemo Mlima Kilimanjaro,Ngorongoro Creators na Serengeti vipo
Tanzania. Hii ni fulsa pia kwa viwanda na bidhaa za Tanzania kujitangaza
kimataifa na kuingia katika masoko ya kimataifa.
Taratibu
zote za mikataba za kimataifa zimekamilika,tunatarajia kutangaza rasmi
tarehe ya kufanyika kwa shindano hilo nchi, wakati wa fainali za Miss
Utalii Vyuo Vikuu 2011/12 – Kanda ya kati, litakalo fanyika Ijumaa ,
tarehe 30-12-2011 katika ukumbi wa Club la Azziz Dodoma. Shindano hilo
linashirikisha zaidi ya warembo 15 kutika vyuo vikuu vilivyopo katika
mikoa ya kanda ya kati, ikiwemo mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora.
Tayari
taratibu za kitaifa zimanza kufanywa ,zikiwemo za kushirikisha wadau na
mamlaka mbalimbali wa ndani na nje ya nchi. Hatua zote madhubuti
zimechukuliwa na zinaendelea kuchukuliwa kwa kuzingatie uzoefu na
mapungufu ya liyo jitokeza katika fainali za Dunia zilizofanyika nchini
mwaka 2006,pale Ubungo Plaza 11-3-2006.
Mkataba
wa kufanyika kwa fainali hizo za Dunia ,nchini umesainiwa na Rais wa
Miss Tourism United Nation Organisation, Ngugu Leon Willians na Rais wa
Miss Tourism Tanzania Organisation ,Gideon Chipungahelo tarehe
8-12-2011.
No comments:
Post a Comment