Miss Tanzania Salha Isarel akipokea funguo ya gari aina ya Jeep
Patriot kutoka kwa Meneja Matukio na Udhamini wa kampuni ya Vodacom
Tanzania Rukia Mtingwa kama ishara ya makabidhinao ya zawadi ya ushindi
kwa kutwaa taji la Miss Tanzania 2011 katika shindano
lililofanyika Septemba.Kulia ni Mkurugenzi wa Lino Agency waratibu wa
shindano hilo la Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga na mwengine
anaeshuhudia ni Meneja Masoko wa CFAO wadhamini wenza wa shindano Bw.
Alfred Minja. Gari hiyo ina thamani ya shilingi 72 Milioni.
Miss Tanzania Salha Isarel akionyesha funguo ya gari aina ya Jeep
Patriot lenye thamani ya shilingi milioni 72mara baada ya kukabidhiwa
na Meneja Udhamni na Matukio wa kampuni ya Vodacom Tanzania Rukia
Mtingwa wa pili toka kulia kama ishara ya makabidhinao ya zawadi ya
ushindi kwa kutwaa taji la Vodacom Miss Tanzania 2011 katika shindano
lililofanyika Septemba.Kulia ni Mkurugenzi wa Lino Agency waratibu wa
shindano hilo la Vodacom Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga na mwengine
anaeshuhudia ni Meneja Masoko wa CFAO wadhamini wenza wa shindano Bw.
Alfred Minja.
Vodacom
Miss Tanzania Salha Isarel akifungua mlango wa gari lake aina ya Jeep
Patriot lenye thamani ya shilingi 72 milioni tayari kwa kuondoka nalo
mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Meneja Udhamini na Matukio wa
kampuni ya Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa hayupo pichani,Ikiwa ni zawadi
ya ushindi kwa kutwaa taji la Vodacom Miss Tanzania 2011 katika
shindano lililofanyika Septemba.
Rais
Jakaya Kikwete akimpongenza Balozi Liberata Mulamula kwa kazi nzuri
aliyoifanya katika sekreteriati ya Maziwa Makuu kwa miaka mitano.
Pembeni ni Dr Asha-Rose Migiro Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Rais Kikwete na Dr Migiro na Balozi Mulamula leo leo December 15, 2011
katika hoteli ya Speke Commonwealth Resort kitongoji cha Munyonyo nje
kidogo ya jiji la
Kampala kunakofanyika mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa Makuu (ICGLR)
ambapo Balozi Mulamula ndiyo amemaliza rasmi muda wake wa kufanya
kazi kama Katibu Mtendaji wa (ICGLR) na kumuachia kiti Prof. Lumu
Alphonse Ntumba Luaba (59) wa DRC.
No comments:
Post a Comment