JAHAZI MOLDEN TAARAB YATIMIZA MIAKA 5 NA KUZINDUA ALBAM YAKE YA MPENZI CHOCOLATE
Hassan
Yahya Mwinyi Katibu Mkuu wa kundi la Taarab la Safari Malindi kulia
akimpongeza Khamis Koha Mkurugenzi Msaidizi wa kundi la Muziki wa
Taarab la Jahazi, baada ya kuzindua rasmi albam yao mpya ijulikanayo
kama Mpenzi Chocolate na sherehe za miaka 5 ya kundi hilo zilizofanyika
mkesha wa Krismasi usiku wa kuamkia leo, kwenye ukumbi wa Diamond
Jubilee ikishuhudiwa na mashabiki lukuki wa muziki wa Taarab huku
mtandao wako wa FULLSHANGWE ukiwa ni mmoja wa mashuhuda. Uzinduzi
huo ulioambatana na Jahazi Molden Taarab kutimiza miaka 5 ilidhaminiwa
na kinywaji cha Serengeti Lager kinachozaliswa na kampuni ya bia ya
Serengeti (SBL)
Mwanamuziki
Mzee Yusuf ambaye pia ni kiongozi wa kundi hilo akiingia ukumbini kwa
staili ya aina yake huku akilakiwa na mashabiki wa muziki wa Taarab.
Mmoja wa kundi hilo Aisha Mahamoud akipagawisha mashabiki mbvele ya Camera na mashabiki wake.
Keki Maalum ya miaka 5 ya Jahazi Molden Taarab ikisubiri kuliwa na wapenzi wa bendi hiyo.
No comments:
Post a Comment