Mkurugenzi
wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega akiongea na waandishi wa
habari leo kwenye Hoteli ya JB Belmonte jijini Dar es salaam wakati
alipotangaza udhamini wa Miss Tanzania 2012 ambapo Redds imedhamini
mashindano hayo mwaka huu kwa milioni 700, katika picha kutoka kulia ni
Miss Tanzania Salha Israel, Vick Kimaro Meneja wa Redds na Meneja Masoko
wa TBL Fimbo Butala.
Mkurugenzi
wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega na Meneja Masoko wa TBL Fimbo
Butala. wakijiandaa kukabidhiana hati mara baada ya kusaini mkataba wa
udhamini wa mashindano ya Redds Miss Tanzania, wanaoshuhudia ni
Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania Prashant Patel kushoto nyuma na
Vick Kimaro Meneja wa kinywaji c
ha Redds.
Mkurugenzi
wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega na Meneja Masoko wa TBL
Fimbo Butala. wakikabidhiana hati mara baada ya kusaini mkataba wa
udhamini wa mashindano ya Redds Miss Tanzania, wanaoshuhudia ni
Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania Prashant Patel kushoto nyuma na
Vick Kimaro Meneja wa kinywaji cha Redds.
Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original leo
imetangaza rasmi kuchukua nafasi ya “Mdhamini Mkuu” wa shindano kubwa
kabisa la urembo hapa nchini lijulikanalo kama “Miss Tanzania”.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, meneja masoko wa TBL Bw.
Fimbo Butallah alisema; Redds Original, leo inatangaza kuwa ndio
wadhamini wakuu wa mashindano ya urembo Tanzania, yanayojulikana kama
“Miss Tanzania”. Kwa udhamini huu, mashindano haya sasa yatajulikana
kama “REDDS MISS TANZANIA 2012”. Kwa miaka kadhaa sasa Redds
Original imekuwa ikishiriki katika mashindano haya kama mdhamini
mwenza, yaani “Kinywaji rasmi cha Miss Tanzania”. Hivyo leo tunapiga
hatua nyingine kubwa katika historia ya tasnia hii ya urembo hapa
nchini kwa kuwa mdhamini mkuu wa mashindano ya Miss Tanzania.
Katika
kuonesha kuwa Redds Original, imedhamiria kwa dhati kuendeleza tasnia
hii, leo tumesaini mkataba wa udhamini wa mashindano haya kwa kipindi
cha miaka mitatu, yaani 2012 hadi 2014. Hii inawahakikishia wapenzi na
mashabiki wa mashindano haya kuwa wataendelea kushuhudia mashindano
haya na kuburudika na kinywaji cha Redds Original kwa kipindi chote
hiki. Alisema Butallah.
Nae
Meneja wa Kinywaji cha Redds Original Bi. Victoria Kimaro alisisitiza
juu ya udhamini wa mashindano haya kuanzia ngazi za chini hadi ngazi ya
Taifa. Udhamini huu mkubwa wa mashindano ya Miss Tanzania unajumuisha
udhamini tutakaotoa katika maeneo mbali mbali kwa ngazi za vitongoji
hadi Taifa. Tunawaahidi mashabiki wote wa mashindano haya na wadau wa
tasnia ya urembo kujiandaa kwa burudani ya hali ya juu.
Akizungumzia
udhamini huo, Mkurugenzi wa LINO Agency waandaaji wa shindano la Miss
Tanzania, Bw. Hasim Lundenga alisema; Kwa niaba ya kamati ya Miss
Tanzania napenda kutoa shukurani za dhati kwa TBL kupitia kinywaji
chake cha Redds Original kwa udhamini huu, na tunatangaza rasmi kuwa
mashindano haya sasa yataitwa “Redds Miss Tanzania’. Kitu kikubwa
tunachowashukuru wadhamini wetu ni mkataba ambao tumesaini hii leo,
ukituhakikishia udhamini wa mashindano haya kwa miaka mitatu.
Kwa
mara nyingine tunawapongeza zaidi Redds original kwa kuwa mstari wa
mbele katika kuendeleza tasnia hii ya urembo hapa nchini. Tumekuwa nao
bega kwa bega kwa miaka kadhaa sasa, na haiwezekani ukazungumzia tasnia
ya urembo hapa nchini bila kuitaja Redds Original. Alisema Lundenga.
No comments:
Post a Comment