Siku
ya Jana ambayo ilikuwa siku ya wapendanao duniani ambayo wengi
walitumia kuenzi mapenzi yao, huko kenya imethibitika kwamba baadhi ya
wanaume hawakuisheherekea kwasababu ya maumivu waliyonayo ya kupigwa na
kunyanyaswa na wake zao.
mwenyekiti
wa chama cha kutetea haki za wanaume nchini humo Nderitu Njogu, amesema
idadi ya wanaume wanaopigwa na wake zao imeongezeka sana ambapo utafiti
wa chama chake umeonyesha kuwa harakati za kumpa uwezo mwanamke
zimeathiri maadili na kuwafanya wawadharau wanaume.
Nderitu
amesema sababu nyingine kubwa ya wanawake kuwanyanyasa wanaume ni uwezo
mkubwa wa kifedha walionao wanawake kuliko waume zao ambapo hii ishu
imeripotiwa leo, wakati wiki iliyopita Polisi walimkamata na
kumuweka ndani mwanamke mmoja mjini Nyeri huko mkoa wa kati, baada ya
kumshambulia mume wake na kumjeruhi vibaya kwa panga ambae kwa sasa bado
kalazwa hospitali, yani huyo mwanaume.
Kwa
kumalizia, Bw Nderitu anadai kuwa zaidi ya wanaume laki nne na elfu
sitini, walinyanyaswa na wake zao mwaka jana ambapo utafiti wa shirika
lake unaonyesha kesi nyingi za waume kuteswa na wake zao zinaripotiwa
katika mkoa wa kati.
No comments:
Post a Comment