Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Joyce Mapunjo akielezea
jinsi alivyodhalilishwa na gazeti la Dira ya Mtanzania mbele ya Kamati
ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) wakati kesi hiyo
iliyoendeshwa jijini Dar es Salaam.
Mhariri
wa Habari wa gazeti la Dira ya Mtanzania, Ponsian Rwechungura
akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari
Tanzania (MCT) wakati wa usikilizwaji wa shauri la Katibu Mkuu wa
Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Joyce Mapunjo dhidi ya gazeti la
Dira ya Mtanzania.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya MCT Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akiahisha shauri hilo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Joyce Mapunjo (kulia)
wakiwa na Mhariri wa Habari wa gazeti la Dira ya Mtanzania, Ponsian
Rwechungura wakifuatilia maamuzi Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari
Tanzania (MCT) wakati wa usikilizwaji wa shauri lao.
Wasikilizaji wakifuatilia shauri.
Kamati
ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania wakati wa usikilizwaji wa
shauri la Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Joyce
Mapunjo dhidi ya gazeti la Dira ya Mtanzania.
Kesi
ya udhalilishaji wa kihabari iliyofunguliwa na Katibu Mkuu wa wizara
ya Viwanda, Biashara na Masoko Joyce Mapunjo dhidi ya gazeti la Dira ya
Mtanzania, imeahirishwa mpaka wakati mwingine baada ya uongozi wa
gazeti hilo kushindwa kumleta mhusika halisi wa kujibu tuhuma
zinazolikabili gazeti hilo, mbele ya Mahakama ya usuruhishi ya Baraza
la Habari nchini MCT.
Akizungumza
mara baada ya kuahirisha kesi hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya
MCT Jaji Mstaafu Thomas Mihayo aliutaka Uongozi wa gazeti hilo
kuhakikisha unamleta kiongozi husika anayefahamu vizuri chimbiko la
tuhuma hizo, ili kuepusha matatizo zaidi endapo katibu mkuu huyo
atapewa ruhusa ya kulifikisha suala hilo mahakani.
Katika hatua nyingine Baraza hilo limeahirisha kesi nyingine ya udhalilishaji iliyofunguliwa na Waziri mkuu mstaafu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Edward Lowasa dhidi ya gazeti hilo kutokana na Kiongozi huyo kuwepo bungeni mjini Dodoma.
Katika hatua nyingine Baraza hilo limeahirisha kesi nyingine ya udhalilishaji iliyofunguliwa na Waziri mkuu mstaafu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Edward Lowasa dhidi ya gazeti hilo kutokana na Kiongozi huyo kuwepo bungeni mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment