Samaki aina ya Sangara tayari kwa kukatwakatwa vipande soko la kimataifa Mwaloni kirumba jijini Mwanza.Wafanyabiashara
wakipanga vichwa vya samaki vilivyokaushwa almaarufu 'Mapanki' kwaajili
ya kufungwa marobota kwa biashara nchi za afrika mashariki na kati.Mapanki katika mpangilio madhubuti....Kayabo
ni samaki aina ya sangara aliyesindikwa kwa chumvi nyingi maarufu sana
na soko kubwa liko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako ni chakula
kinacholiwa na matajiri.Kayabo uhamishaji toka sehemu moja hadi kwenye madaraja ya viwango.Wafanyabiashara
wakichambua makayabo yaliyokauka yenye ubora yanayopaswa kuingia kwenye
hatua ta uwekwaji kwenye marobota njiani kwenda sokoni.Mwananchi akigeuza vipande vya samaki vilivyokatwa almaarufu kama 'chips' kwaajili ya kukauka vizuri juani.Maranyingi
samaki wanaosafirishwa kwa soko la nje ni minofu tu iliyokatwa kiufundi
ambayo huifadhiwa kwenye makasha maalum yenye barafu, vichwa, mifupa,
mikia na mabaki mengine toka viwandani hukusanywa kwaajili ya kukaushwa
kama hivi kwa chakula cha walaji wengine na masalia mengine
yasiyohitajika hufanywa chakula kwa kuku.Uanikaji soko la Mwaloni Kirumba Mwanza Tanzania.Mabaki
haya ya mifupa ya samaki anikoni kwaajili ya kuchanganywa na dagaa
kisha husagwa kutengenezwa kama sehemu ya chakula cha kuku.Oda maalum ya Mwanamuziki maarufu Kongo mkongwe mwenye bahati ya kupata mialiko mingi nchini...Wanajulikana
sana kwa jina la Ndege Mwarabu wakiranda kwa makundi katika meza
zilizowazi za kuanikia samaki wa biashara sokoni Mwaloni Kirumba jijini
Mwanza hakika ni utalii tosha.
No comments:
Post a Comment