Mji
wa Homs nchini Syria imekuwa ukitikiswa na mashambulio mazito ya
silaha, wakati majeshi ya Syria yakiongeza nguvu za kushambulia mji
huo. Wanahabari
waliyeko huko wanasema kuna milio inayofuatana, katika shambulio kali
zaidi katika kipindi cha miezi 11 ya maandamano. Rais
wa Marekani Barack Obama amesema ni muhimu kumaliza mzozo huo bila
kuingilia kijeshi. Wakati huohuo, Urusi na Uchina zimetetea kura yao ya
veto katika muswada wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, hatua ambayo
imewakasirisha mahasimu wa Rais Bashar al-Assad. Mji wa Homs, moja ya ngome kubwa zinazopinga utawala wa Bw Assad, umekuwa ukishambuliwa na majeshi ya serikali kwa siku kadhaa. Waasi wanadai kuwa mashambulizi ya majeshi ya serikali yameteketeza hospitali katika wilaya ya Baba Amr na kusababisha vifo.
No comments:
Post a Comment