Mgombea
anayepigiwa upatu kushinda uteuzi wa urais wa chama cha Republican
katika uchaguzi mkuu wa mwezi novemba nchini Marekani, ameshinda uteuzi
wa chama hicho katika jimbo la Michigan alikozaliwa. Romney alishinda uteuzi huo baada ya kinyanganyiro kikali dhidi ya mpinzani wake wa karibu Rick Santorum. Ushindi
huo katika jimbo la Michigan umeonekana kuwa muhimu kwa bwana Romney
kujikatia tikiti ya chama hicho kupambana na rais Barrack Obama. Ameshukuru waliompigia kura na kuahidi kuendelea na juhudi zake za kutafuta uungwaji mkono. Wachanganuzi
wa masuala ya kisaisa wanasema ushindi wa Romney utampa nguvu zaidi
hasa kwa kuwa kura za maoni zilikuwa zimeashiria kuwa mgombea mwenzake
Bw Santorum huenda angeshinda. Mitt Romney vile vile ameshinda uteuzi wa chama hicho katika jimbo la Arizona.
No comments:
Post a Comment