Polisi
wakiwatawanya na kuwakamata baadhi ya waandamanaji hao katika
manispaa ya Songea baada ya wakazi wa manispaa hiyo wengi wao wakiwa
madereva wa pikipiki kuandamana hadi ofisi ya kamanda wa polisi mkoa
wa Ruvuma kupinga mauaji ya watu yanayoendelea kwa kasi mjini humo
ambao hadi sasa jeshi la polisi halijafanikiwa kuwakamata wauaji.
Mtu mmoja ambae Jina lake halija fahamika mapema akiwa amepigwa Risasi na Polisi na Kufariki Papo hapo mapema jana.
Watu
watatu wameuawa kufuatia vurugu kati ya polisi na raia mkoani Ruvuma
ambapo kati yao wawili waliuawa kwa kupigwa risasi na Jeshi la polisi na
mmoja ameuawa kwa ajali ya pikipiki na wengine 41 wamejeruhiwa.
Katika
vurugu hizo wananchi walikuwa wakitoa lawama kwa Jeshi hilo kushindwa
kukabiliana na mauaji ya watu ambapo miili yao ilikuwa ikikutwa
imenyofolewa baadhi ya viungo vya mwili.
Kutokana
na hali hiyo leo hii Jeshi la polisi mkoani humo limewashikilia askari
wake wanne kwa mahojiano zaidi kutokana na kusababisha vifo vya watu
wawili kupitia vurugu hizo.
Awali
kabla ya vurugu baadhi ya madereva wa pikipiki na wananchi wa mtaa wa
Lizaboni walianza kujikusanya na kuanza maandamano kuelekea kituo kikuu
cha polisi kilichopo karibu na uwanja wa majimaji mjini songea huku
wakiimba nyimbo za kulilaumu jeshi la polisi kushindwa kudhibiti mauaji
ya zaidi ya watu kumi na tatu huku mmiili yao ikinyofolewa baadhi ya
viungo.
Baada
ya vurugu hizo Mkuu wa wilaya ya Songea Thomas Ole Sabaya amesema
Serikali inalishughulikia suala hilo na kwamba wananchi wanatakiwa
kushirikiana kwa karibu na Jeshi la polisi katika kudhibiti matukio hayo
kutokana na vitendo hivyo kufanywa kwa usiri mkubwa, pia watendeji wa
matukio hayo ni miongoni mwa wanajamii wenyewe.
No comments:
Post a Comment